Tuweni wakweli na msema kweli ni kipenzi cha Mungu.
Unaposema utaiangusha serikali ya Tanzania chini ya mwevuli wa CCM ikiongozwa na Mh.Samia Suluhu au kusema Utaishinda serikali ya Tanzania chini ya mwevuli wa CCM ikiongozwa na Mh Samia Suluhu.
Sasa waliosema tuseme wakubali tu kuwa wameteleza sio lengo lao ili yaishe.
" Kusema utaitisha maandamano ya nchi nzima yasio na ukomo tena mtahakikisha mpaka serikali ya Tanzania chini ya Mheshimiwa Samia suluhu mnaiondosha madarakani kabla ya muda wake"
Ingependeza kusema mpaka inajiuzulu na sio kusema mnaiondoa madarakani.
Kuondoa madarakani inaweza kuwa kwa hayo maandamano yatakayokuwa hayana mwisho mwema yenye lengo la kufanya mapinduzi baridi au ya moto kuiondoa serikali madarakani ,tumeona maandamano ya aina hio yakitokea Misri / Egypty (maarufu Arab Spring).
Maandamano yao hayakuwa na mwisho mwema.
Yalikuwa ni kama hayo yaliotajwa na Chadema kuipinga serikali iliyopo madarakani yalikuwa ni maandamano yaliyokuwa na lengo moja tu kuipinduwa serikali ndani yake walikuwemo waasi wenye silaha na yalienea nchi nyingi za kiarabu yalianzia Tunisia 2010 .
Maandamano hayo yalifanikiwa kuipindua Serikali ya Tunisia,Algeria Jordan Misri ila Yeman na Libya yalisababisha mtafaruku wa vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi leo bado hizo nchi hazijakaa sawa.
Hio ndivyo Historia inavyotuambia ,leo hii viongozi wa Chadema wameonekana majukwaani wakitaka kuirudia historia hio kuanzia hapa Tanzania.
Waliotiwa hatiani wana kesi ya kujibu tusijikite upande mmoja,nasema tu wajiteetee kama kuku anaekaribia kutaga kuwa waliteleza na sio lengo lao.