Hapa JF, hata ulete swali la namna gani, hukosi jibu la kukufikirisha na kukuchangamsha akili!
Naweza kusema, karibu ni sawa na mwalimu na wanafunzi wake darasani.
Mwalimu mzuri anayewapa fursa wanafunzi wake watumie akili zao kutafuta jibu la tatizo lililo mbele yao, hakosi kupata aina fulani ya jibu lililo karibu sana na utatuzi wa jambo husika.
Mkuu 'Sheiza', ningekuwa ni Profesa wako, huu mtihani ungeambulia alama ya A, bila ya maneno mengine yoyote.
Niseme hapa, katika jambo hili la mali za Tanganyika, na mwelekeo mzima wa anayoyafanya Samia, ni kinyume kabisa na yale aliyokuwa akiyapigania Magufuli.
Ingetokea leo hii akarudi hata kwa saa moja na kushuhudia anayofanya aliyekuwa msaidizi wake wa karibu, sina shaka kabisa, kati ya Samia na wakili; mMagufuli angemteua wakili kuwa msaidizi wake na kumsweka ndani Samia, tena akitoa kelele nyingi sana juu ya huyu mama.