Wakili Mwabukusi ni Mchanganyiko wa Mdude + Lissu. Je Alikuwa Wapi Wakati wa Hayati Magufuli?

Hilo ni swala jingine, ambalo hata mimi ningependa kujua.

Hapa linazungumziwa hili la mali za waTanzania kunadiwa, au umesahau mada inasemaje?

Na kwa bahati nzuri mleta mada ni wewe mwenyewe!

Ni katika mtiririko huo huo wa mawazo niliyotoa kuhusu jibu alilotoa mkuu 'Sheiza'; wewe hapo kama mwanafunzi wangu ungeambulia F moja kwa moja, kwa kuchanganya mambo yasiyohusika.

Sasa sijuiutasemaje?
Wewe unajikuta mwalimu wa kugawa F kwa watu wenye mawazo yao makubwa na wamekuzidi tafsida??

Hakuna nilicho changanya sema ubongo wako ni mdogo kugundua tafsida yangu.

Bandari "iliyouzwa" kama mnavyodai itarudishwa mara moja baada ya Samia kutoka madarakani. Lakini huwezi kurudisha maisha ya wale Magufuli aliwaua na kuwajeruhi. Tundu Lissu hawezi kutembea kama zamani.

Ndiyo hapo nauliza je huyu Bingwa wa kutetea raslimali za Taifa Mwabukusi, alikuwa hamuoni Magufuli aliua na kuteka watu? Au akijenga miundombinu mikubwa bila ruhusa ya Bunge kwao Chato?
 
Labda kungewekwa mikataba wazi kama huu angeweza kuibuka.
Kuna mtu hata akisaini mikataba gizani huwezi kuwa na shaka lakini kuna mtu hata akisaini mikataba mbele yako unapata mashaka.

Mikataba ya Magu karibia yote ilisainiwa nchini. Hata Museven alitoka UG hadi Chato kwa ajili ya kusaini mkataba. Na usisahau mikataba yote ilisainiwa kitaifa. Yaani tulishuhudia live na tuliambiwa malengo ya mikataba na sisi tunanufaikaje.

Ndio maana hata wapinzani wa Magufuli hawakuwa na hoja tena juu ya mikataba. Hata utiaji wa saini wa kampuni tuliyoambiwa tutashtakiwa MiGA ulifanyika hadharani.

Na Lissu mwenyewe amethibitisha kuwa hakuna mkataba wenye mashaka kuhusu nchi.

Huyu mama ako kwa siku moja alisaini mikataba ishirini Dubai. Hadi inaonekana ilifika mahali hajui anasaini nini.
 
Ni wazi hakuna ubishi Man of The Moment (MOTM) kwa sasa ni Wakili Boniface Mwabukusi kutokana na namna alivyolibeba suala la Bandari/DP WORLD kwa mabega mawili. Wanasiasa na Wanaharakati wengi wameongea kama kina Lissu, Mbowe, Slaa, Tibaijuka, Shivji, Binti Sarungi, Madeleka na Nshala. Lakini ni Wakili Boniphace Mwabukusi ndiyo maneno yake na haiba yake yana mvuto kuliko mtu yeyote. Mwabukusi ana uwezo wa kuwasilisha mada kwenye hadhara kama Wahubiri wa Kilokole akina Mwamposa/ Gwajima, ana maneno makali kama Mdude na ana uwezo kuchambua sheria kama Lissu.

Swali:
Je, huyu Bwana alikuwa wapi wakati wa Dikteta Magufuli 2015-21? Alipobana kabisa uhuru wa maoni na kukanyaga katiba

Je, kwa huu ubingwa wake, nini ingekuwa hatma yake kipindi cha Magufuli?
Magufuli hakuwa na tofaoti na kagame kila anao mkusoa jela au kuzikwa tu huyu mama mpole bhana
 
Najuwa Magufuli hakupenda Bagamoyo Port na alitoa pumba nyingi tu. Lakini pia Magufuli alikuwa na UHAYAWANI wake kama kulidhibiti Bunge, Kuitisha Mahakama, kuvibana vyombo vya habari na kuua wakosoaji kama kina Ben Saanane au kumjeruhi Tundu Lissu.

Sasa huyu Mwabukusi alikuwa wapi hayo yakitendeka?
Unaviongea ni vitu vya kufikirka tu .na umeandika huvyo kuneutriliz mambo na kuonyesha kuwa saa100 ni bora kuliko jpm
.aliyedhibiti bunge ni huyu wa dp au yule jpm
 
We unaona huyu ni mwanasiasa? Huyu ni mtetezi wa rasilimali za taifa, kitu ambacho Magu alikipigania hadi anakufa.

Mambo sijui ya demokrasia aliwaachia wanasiasa.
Magu alivunja katiba na mama kaivunja katiba swali wakati wa magu alikuwa wapi?
 
Ni wazi hakuna ubishi Man of The Moment (MOTM) kwa sasa ni Wakili Boniface Mwabukusi kutokana na namna alivyolibeba suala la Bandari/DP WORLD kwa mabega mawili. Wanasiasa na Wanaharakati wengi wameongea kama kina Lissu, Mbowe, Slaa, Tibaijuka, Shivji, Binti Sarungi, Madeleka na Nshala. Lakini ni Wakili Boniphace Mwabukusi ndiyo maneno yake na haiba yake yana mvuto kuliko mtu yeyote. Mwabukusi ana uwezo wa kuwasilisha mada kwenye hadhara kama Wahubiri wa Kilokole akina Mwamposa/ Gwajima, ana maneno makali kama Mdude na ana uwezo kuchambua sheria kama Lissu.

Swali:
Je, huyu Bwana alikuwa wapi wakati wa Dikteta Magufuli 2015-21? Alipobana kabisa uhuru wa maoni na kukanyaga katiba

Je, kwa huu ubingwa wake, nini ingekuwa hatma yake kipindi cha Magufuli?
Kipindi cha Magufuri alikuwa Mbeya.
Swali lako la pili; Hakumpinga Magufuri kw sababu Magu hakuingia mkataba wowote wa namna hii na akina Dpw. Nafikiri hata Magufuri angekuwa leo kafanya hivi angempinga kutokana na maelezo aliotoa
 
Sidhani kama angefungua mdomo wake
 
Ni moja ya watu vilaza sana, kesho mtamsikia anaongea tofauti... Wanaomjua huyo jamaa wanacheka tu, chadema wenyew hawawez kumpa backup wanajua ni kilaza tu
 
Kuna mtu hata akisaini mikataba gizani huwezi kuwa na shaka lakini kuna mtu hata akisaini mikataba mbele yako unapata mashaka.

Mikataba ya Magu karibia yote ilisainiwa nchini. Hata Museven alitoka UG hadi Chato kwa ajili ya kusaini mkataba. Na usisahau mikataba yote ilisainiwa kitaifa. Yaani tulishuhudia live na tuliambiwa malengo ya mikataba na sisi tunanufaikaje.

Ndio maana hata wapinzani wa Magufuli hawakuwa na hoja tena juu ya mikataba. Hata utiaji wa saini wa kampuni tuliyoambiwa tutashtakiwa MiGA ulifanyika hadharani.

Na Lissu mwenyewe amethibitisha kuwa hakuna mkataba wenye mashaka kuhusu nchi.

Huyu mama ako kwa siku moja alisaini mikataba ishirini Dubai. Hadi inaonekana ilifika mahali hajui anasaini nini.
Kinachosikitisha zaidi ni kuwa taasisi ya urais ni nyeti sana na ina wasaidizi ndio maana tunasikia waziri wa nchi ofisi ya rais nk. sàsa inakuwaje mama anakuwa kama yuko peke yake??!!
 
Wewe unajikuta mwalimu wa kugawa F kwa watu wenye mawazo yao makubwa na wamekuzidi tafsida??

Hakuna nilicho changanya sema ubongo wako ni mdogo kugundua tafsida yangu.

Bandari "iliyouzwa" kama mnavyodai itarudishwa mara moja baada ya Samia kutoka madarakani. Lakini huwezi kurudisha maisha ya wale Magufuli aliwaua na kuwajeruhi. Tundu Lissu hawezi kutembea kama zamani.

Ndiyo hapo nauliza je huyu Bingwa wa kutetea raslimali za Taifa Mwabukusi, alikuwa hamuoni Magufuli aliua na kuteka watu? Au akijenga miundombinu mikubwa bila ruhusa ya Bunge kwao Chato?
Mkuu 'Huihui', ningependa sana kujadili hilo la "...watu wenye mawazo yao makubwa na wamekuzidi tafsida" kama tutakubaliana muda wa kufanya hivyo kikamilifu zaidi. Kwa hiyo, hili amua wakati na wapi unataka tufanye hivyo.

La muhimu zaidi hapa ni hili suala la "wakili na Magufuli".

Wewe unaona maumivu na mauti aliyosababisha Magufuli pekee; kana kwamba hiyo ndiyo sifa pekee iliyomhusu.

Nataka usinielewe vibaya, kwamba mimi sikuyaona hayo mambo na kuyalaani vikali kabisa. Maandishi yangu hayajifichi humu JF kuhusu hilo.; na nitaendelea kulaumu Magufuli siku zote na kumnyima heshima ambayo angeistahiri kwa mambo mengine aliyoyasimamia, kama hili la mali za taifa letu.

Lakini nataka nirudi nyuma kukumbusha hili la Samia unalosema atakapoondoka na DP World itakuwa imeondoka kama hatuihitaji.
Unachosahau wewe na wengi wa aina yako ni madhara yanayotokana na hilo sasa hivi hadi hapo Samia atakapokuwa ameondoka.

Unachoona wewe, na hata mimi nakiona, ni kupotea kwa Ben, na kuumizwa kwa Tundu Lissu, mambo ambayo sote tunayasikitikia sana. Lakini kwa upande wako, unaonyesha kufifisha akili yako kuhusu matatizo makubwa zaidi, na hata vifo vinavyotokana na hujuma hizi za DP World, tena kwa watu wengi zaidi, kwa vile tu, akili yako haikuwezeshi kufika huko.

Inatosha. Kama huelewi, huelewi, na kama hutaki tu kuona hivyo, hutaki tu kwa utashi wako.

F niliyotoa inabaki palepale.
 
Ni wazi hakuna ubishi Man of The Moment (MOTM) kwa sasa ni Wakili Boniface Mwabukusi kutokana na namna alivyolibeba suala la Bandari/DP WORLD kwa mabega mawili. Wanasiasa na Wanaharakati wengi wameongea kama kina Lissu, Mbowe, Slaa, Tibaijuka, Shivji, Binti Sarungi, Madeleka na Nshala. Lakini ni Wakili Boniphace Mwabukusi ndiyo maneno yake na haiba yake yana mvuto kuliko mtu yeyote. Mwabukusi ana uwezo wa kuwasilisha mada kwenye hadhara kama Wahubiri wa Kilokole akina Mwamposa/ Gwajima, ana maneno makali kama Mdude na ana uwezo kuchambua sheria kama Lissu.

Swali:
Je, huyu Bwana alikuwa wapi wakati wa Dikteta Magufuli 2015-21? Alipobana kabisa uhuru wa maoni na kukanyaga katiba

Je, kwa huu ubingwa wake, nini ingekuwa hatma yake kipindi cha Magufuli?
Angejitokeza wakati wa awamu ya tano usingemjua wakati huu wa awamu ya sita.
 
We unaona huyu ni mwanasiasa? Huyu ni mtetezi wa rasilimali za taifa, kitu ambacho Magu alikipigania hadi anakufa.

Mambo sijui ya demokrasia aliwaachia wanasiasa.
Hana utetezi wowote anatafuta kuonekana ili apate pesa zitakazolipia madeni yote aliyonayo haswa zile kesi anazoshindwa na kutakiwa alipe fidia.

Anacheza na maneno ya kisheria haswa vifungu vichache vitakavyompa umaarufu, hawezi kuusoma mkataba mzima kwani kuna vifungu vitamuumbua.
 
Back
Top Bottom