Wakili Mwabukusi ni Mchanganyiko wa Mdude + Lissu. Je Alikuwa Wapi Wakati wa Hayati Magufuli?

Wakili Mwabukusi ni Mchanganyiko wa Mdude + Lissu. Je Alikuwa Wapi Wakati wa Hayati Magufuli?

Mkuu 'Huihui', ningependa sana kujadili hilo la "...watu wenye mawazo yao makubwa na wamekuzidi tafsida" kama tutakubaliana muda wa kufanya hivyo kikamilifu zaidi. Kwa hiyo, hili amua wakati na wapi unataka tufanye hivyo.

La muhimu zaidi hapa ni hili suala la "wakili na Magufuli".

Wewe unaona maumivu na mauti aliyosababisha Magufuli pekee; kana kwamba hiyo ndiyo sifa pekee iliyomhusu.

Nataka usinielewe vibaya, kwamba mimi sikuyaona hayo mambo na kuyalaani vikali kabisa. Maandishi yangu hayajifichi humu JF kuhusu hilo.; na nitaendelea kulaumu Magufuli siku zote na kumnyima heshima ambayo angeistahiri kwa mambo mengine aliyoyasimamia, kama hili la mali za taifa letu.

Lakini nataka nirudi nyuma kukumbusha hili la Samia unalosema atakapoondoka na DP World itakuwa imeondoka kama hatuihitaji.
Unachosahau wewe na wengi wa aina yako ni madhara yanayotokana na hilo sasa hivi hadi hapo Samia atakapokuwa ameondoka.

Unachoona wewe, na hata mimi nakiona, ni kupotea kwa Ben, na kuumizwa kwa Tundu Lissu, mambo ambayo sote tunayasikitikia sana. Lakini kwa upande wako, unaonyesha kufifisha akili yako kuhusu matatizo makubwa zaidi, na hata vifo vinavyotokana na hujuma hizi za DP World, tena kwa watu wengi zaidi, kwa vile tu, akili yako haikuwezeshi kufika huko.

Inatosha. Kama huelewi, huelewi, na kama hutaki tu kuona hivyo, hutaki tu kwa utashi wako.

F niliyotoa inabaki palepale.
Ukipewa F na mtu mpumbavu wala haina shida.
 
Labda alikuwa anaona anavyofanya magufuli mi sahihi.

Kwenye Maisha kila MTU anakipaombele chake. Na vile MTU anavyo-react itategemea na vipaombele vyake.

Mwingine Mali ni Bora kuliko Kitu chochote. Yaani kipaombele chake ni Mali( zikiwemo Rasilimali)

Mwingine utu ndio kipaombele chake. Hapa tunazungumzia Haki, Uhuru, uadilifu, ukweli n.k.

Hivyo kila MTU anapiga kelele pale kipaombele chake kinapokanyagwa. Hili ndio jibu
 
Huyu ni wakili by professional yaani mwanasheria!!

Hatujui kwenye mhimili wa nchi na viunga vyake yeye ni nani hadi awe na uwezo wa kuukosoa wazi wazi bila kificho !!!

Huyu ni wakili na nusu,hiyo nusu hatuijui hata kidogo!!
 
We unaona huyu ni mwanasiasa? Huyu ni mtetezi wa rasilimali za taifa, kitu ambacho Magu alikipigania hadi anakufa.

Mambo sijui ya demokrasia aliwaachia wanasiasa.
Amekuja wakati sahihi. Jambo hili ni la kisheria na ndio maana anaonekana kung'ara nalo
 
we ulitaka awe karibu na wewe pamoja na majizi wenzako ccm

Sasa unajua kabisa huyo bi mdude sijui ni mraibu wa madawa ya kulevya na wewe unamfanya kuwa ni rafiki Yako watu watafikiriaje kama siyo wote ni wale wale tuh.
 
Labda alikuwa anaona anavyofanya magufuli mi sahihi.

Kwenye Maisha kila MTU anakipaombele chake. Na vile MTU anavyo-react itategemea na vipaombele vyake.

Mwingine Mali ni Bora kuliko Kitu chochote. Yaani kipaombele chake ni Mali( zikiwemo Rasilimali)

Mwingine utu ndio kipaombele chake. Hapa tunazungumzia Haki, Uhuru, uadilifu, ukweli n.k.

Hivyo kila MTU anapiga kelele pale kipaombele chake kinapokanyagwa. Hili ndio jibu
Umeliweka vizuri mkuu, asante
 
Umeona eeh!! Hata ujenzi wa daraja la Busisi na Chato Airport haukuwa na baraka za Bunge. Aliufyata pia
Daraja la Busisi ni BARAKA kubwa aliyotuachia Magufuri atakumbukwa mpaka kizazi cha nne lakini Ukodishwaji wa Bandari kwa DP World utalalamikiwa vizazi na vizazi mpaka mwisho wa dunia.
 
Ni wazi hakuna ubishi Man of The Moment (MOTM) kwa sasa ni Wakili Boniface Mwabukusi kutokana na namna alivyolibeba suala la Bandari/DP WORLD kwa mabega mawili. Wanasiasa na Wanaharakati wengi wameongea kama kina Lissu, Mbowe, Slaa, Tibaijuka, Shivji, Binti Sarungi, Madeleka na Nshala. Lakini ni Wakili Boniphace Mwabukusi ndiyo maneno yake na haiba yake yana mvuto kuliko mtu yeyote. Mwabukusi ana uwezo wa kuwasilisha mada kwenye hadhara kama Wahubiri wa Kilokole akina Mwamposa/ Gwajima, ana maneno makali kama Mdude na ana uwezo kuchambua sheria kama Lissu.

Swali:
Je, huyu Bwana alikuwa wapi wakati wa Dikteta Magufuli 2015-21? Alipobana kabisa uhuru wa maoni na kukanyaga katiba

Je, kwa huu ubingwa wake, nini ingekuwa hatma yake kipindi cha Magufuli?
Je na wewe ulikuwa wapi!
 
JPM hakuuza nchi Kama huyu mpemba, alibadilisha sheria kulinda rasilimali za nchi which is Good ,huyu kibwetele anataka kuzibadilisha Tena wachache wakwapue maliasili za nchi.
 
Back
Top Bottom