Mkuu 'Huihui', ningependa sana kujadili hilo la "...watu wenye mawazo yao makubwa na wamekuzidi tafsida" kama tutakubaliana muda wa kufanya hivyo kikamilifu zaidi. Kwa hiyo, hili amua wakati na wapi unataka tufanye hivyo.
La muhimu zaidi hapa ni hili suala la "wakili na Magufuli".
Wewe unaona maumivu na mauti aliyosababisha Magufuli pekee; kana kwamba hiyo ndiyo sifa pekee iliyomhusu.
Nataka usinielewe vibaya, kwamba mimi sikuyaona hayo mambo na kuyalaani vikali kabisa. Maandishi yangu hayajifichi humu JF kuhusu hilo.; na nitaendelea kulaumu Magufuli siku zote na kumnyima heshima ambayo angeistahiri kwa mambo mengine aliyoyasimamia, kama hili la mali za taifa letu.
Lakini nataka nirudi nyuma kukumbusha hili la Samia unalosema atakapoondoka na DP World itakuwa imeondoka kama hatuihitaji.
Unachosahau wewe na wengi wa aina yako ni madhara yanayotokana na hilo sasa hivi hadi hapo Samia atakapokuwa ameondoka.
Unachoona wewe, na hata mimi nakiona, ni kupotea kwa Ben, na kuumizwa kwa Tundu Lissu, mambo ambayo sote tunayasikitikia sana. Lakini kwa upande wako, unaonyesha kufifisha akili yako kuhusu matatizo makubwa zaidi, na hata vifo vinavyotokana na hujuma hizi za DP World, tena kwa watu wengi zaidi, kwa vile tu, akili yako haikuwezeshi kufika huko.
Inatosha. Kama huelewi, huelewi, na kama hutaki tu kuona hivyo, hutaki tu kwa utashi wako.
F niliyotoa inabaki palepale.