Wakili Mwakubusi: Vyama vya Upinzani kazi yao ni kufukuzia tu ubunge na ruzuku, haviwezi kulikomboa Taifa

Wakili Mwakubusi: Vyama vya Upinzani kazi yao ni kufukuzia tu ubunge na ruzuku, haviwezi kulikomboa Taifa

Mbowe angekua mpinzani wa kweli asingekaa ndani miezi 8 na raia wakawa kimya tu.Kitendo cha raia kupuuza Mbowe kukaa ndani maana yake hawana imani naye. Hapo Kenya unafikiri Odinga anaweza kaa ndani hata siku 1 na Raia wakawa kimya?Ukweli ni kwamba Mbowe na genge lake hawana ushawishi tena wa kuleta mabadiliko Tanzania. Nenda Kenya kajifunze upinzani unavyofanya kazi.Watu wanapigwa na polisi, Rais anatia mikwara mara IGP lakini watu wanaandamana. Swala ni upinzani kuwa na ushawishi. Huwez kuwa na ushawishi kama unapuuza mambo ya msingi ya raia. Tunalala giza, upinzani upo kimya tu then kesho utegemee Raia wakuunge kutafuta tume huru ya uchaguzi we uingie madaraka hahahahhah
Endeleeni kuiamini CCM basi mnawaongelea ongelea nini fisimaji nyie?
 
Mbowe kachoka sana. Na hata alipokuwa na nguvu, uwezo wake wa kuongoza ulikuwa mediocre sana. Sema wanazi wa CDM hawataki kukubali huu ukweli.
Sasa akitoka Mbowe pale kuna nini kama sio kugawana mbao za jahazi ?

alipokuwa Mahabusu uliona Luna lolote la maana walilofanya waliokuwa uraiani zaid ya design tishert za picha ya Mbowe

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Sawa lakini kama Lissu ataendelea kuwa chini ya Mbowe ataweza kufika potential yake.
Lissu kua chini ya Mbowe,sidhani kama inamzuia asionyeshe potentiality yake,we angalia Mbowe kakaa na mama kwenye suala la maridhiano,Lissu alivyoona ni mazingaombwe,akalipuka... akasema hayana maana.Angekua mwingine,angehofia reaction ya mwenyekiti.
 
Lissu kua chini ya Mbowe,sidhani kama inamzuia asionyeshe potentiality yake,we angalia Mbowe kakaa na mama kwenye suala la maridhiano,Lissu alivyoona ni mazingaombwe,akalipuka... akasema hayana maana.Angekua mwingine,angehofia reaction ya mwenyekiti.
Inamzuia sana unless huelewi vyama vya siasa vya Tanzania vinafanya kazi kwa muundo upi.
 
"Vyama vyetu vya siasa nadhani aidha vimechoka sana vyote vinahitaji kupumzika au viongozi wake wamechoka sana wanahitaji kupumzika, na ndio maana wanapoteza ile hamu ya kulikomboa na kulisimamia taifa, wanakuwa watu wa kufukuzana na tuvyeo, ubunge, ruzuku, kugawana, kukaa kaa mezani.

Kila mmoja yuko bize, wanachotaka ni kugawana tu sio kupambana kwa ajili ya wananchi. Lakini kikubwa ninachojaribu kusema kwamba inawezekana katiba kupatikana bila wanasiasa.” – Wakili Boniphace Mwabukusi

Chanzo: Swahili Times
Mtamalizana sasa, kumbe ndo zenu.
 
Lissu kua chini ya Mbowe,sidhani kama inamzuia asionyeshe potentiality yake,we angalia Mbowe kakaa na mama kwenye suala la maridhiano,Lissu alivyoona ni mazingaombwe,akalipuka... akasema hayana maana.Angekua mwingine,angehofia reaction ya mwenyekiti.
Lis ni mbwabwajaji tu.
 
Mapovu ya machawa wa vyama vya siasa yataanzabkumwagwa
 
Sasa akitoka Mbowe pale kuna nini kama sio kugawana mbao za jahazi ?

alipokuwa Mahabusu uliona Luna lolote la maana walilofanya waliokuwa uraiani zaid ya design tishert za picha ya Mbowe

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Watu wote wa maana walioweza kufanya kazi nzuri wameondoka sababu ya mwenyekiti kung'ang'ania madaraka. Waliobaki ni ndiyo mwenyekiti.
 
Tatizo la wanasiasa ni hilo, hawashangai kipindi cha uchaguzi wanapata kura zaidi ya idadi ukilinganisha na wanachama wao walio hai. Wanashindwa kujiuliza au wanajua ila sema uroho wanatupuuzia sisi tusio na vyama tunawapigia kura, mijadara mingi ya katiba ni jinsi gani katiba iwape madaraka zaidi sio inayohusu kuwatua mizigo iliyowaelemea wananchi. Wanajadili serikali tatu wakati hizo mbili zenyewe ni mzigo kwa wananchi. Hatusikii kujadili mgombea binafsi ambaye hatakuwa na mikutano sekretarieti ya chama wala mkutano mkuu, zaidi ya vikao vya bunge na vikao madiwani kujadili maendeleo ya wananchi na kisha kuwa na mikutano na wananchi kuwapa mrejesho wa walichomtuma kuwasemea. Suruhu ya matatizo ya nchi hii ni serikali moja na mgombea binafsi, akizingua wananchi wanaitisha kikao kisha wanapiga kura kama aendelee au la, tofauti na sasa vyama vyama vinatuletea wawakilishi Mazezeta wanaenda kulala kwenye vikao kisha kusaini posho hawajui wapo pale kwa ajili ya wananchi sio wenyeviti wao wa vyama. Maana wenyeviti kazi yao kubwa ni kupiga simu kwa wateule kutaka maokoto, ukiwa kaidi mwenyekiti atakuundia zengwe kwa wajumbe ili uchaguzi ujao usipite kwa wale wateule wanaojua wapo pale kwa niaba ya wananchi, hatima yao inaishia hapo. Uhai wa chama ni vikao ila uhai wa mgombea binafsi ni kuwaletea wananchi maendeleo sio ahadi zisizo tekelezeka.
 
"Vyama vyetu vya siasa nadhani aidha vimechoka sana vyote vinahitaji kupumzika au viongozi wake wamechoka sana wanahitaji kupumzika, na ndio maana wanapoteza ile hamu ya kulikomboa na kulisimamia taifa, wanakuwa watu wa kufukuzana na tuvyeo, ubunge, ruzuku, kugawana, kukaa kaa mezani.

Kila mmoja yuko bize, wanachotaka ni kugawana tu sio kupambana kwa ajili ya wananchi. Lakini kikubwa ninachojaribu kusema kwamba inawezekana katiba kupatikana bila wanasiasa.” – Wakili Boniphace Mwabukusi

Chanzo: Swahili Times
Kuna ukweli ndani ya maoni yake.
Viongozi wengi ndani ya vyama hivi vya upinzani hawana tofauti kubwa na hao walioko ndani ya CCM, wengi ni wachumia tumbo tu.

Mategemeo waliyo nayo baadhi ya watu na kuyaweka kwa baadhi ya vyama hivi, kwa mfano CHADEMA, ni matumaini tu ya kwamba labda inawezekana, hawa CHADEMA wakiweka juhudi kidogo, uwezekano mkubwa upo wa kuwaondoa CCM madarakani.

Kwa hiyo, pamoja na kutokuwa na uongozi unaoonyesha moto ndani ya matumbo yao kuhusu ukombozi wa kweli wa nchi hii, ajenda muhimu ni kuwaondoa CCM madarakani kwa sasa, ili nchi iweze kuanza kujipanga upya, bila ya CCM kuwafanya waTanzania wote kuwa mateka wao.

Hii ndiyo kazi muhimu tunayowakabidhi CHADEMA kwa sasa, kuwaondoa CCM; Tanzania ipate Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi; kuondoa uchafu wote unaofanyika chini ya CCM.
Hasa huko kung'ang'ania kubaki madarakani kwa ghara yoyote ile; na kujiapiza kuwa itakuwa hivyo milele!

Tukifanikiwa kulifanya hilo, kwa msaada wa CHADEMA, hapo sasa taifa letu linaweza kujipanga upya, na kuwa na matumaini kwamba viongozi wenye Dira na Maono juu ya taifa letu watapatikana.

Kwa hiyo, kwa sasa hivi, kwa maoni yangu, tuwatie moyo hawa CHADEMA, ili waweze kutuongoza na kuratibu kazi za kuwaondoa CCM madarakani.

Anayosema Wakili Mwambukusi, pamoja na kuwa na ukweli ndani yake, kutokuwepo na chama cha upinzani tunachoweza kukitegemea kusimamia mapambano yetu na kutekeleza mipango yetu, ni vigumu sana kwa wakati huu kupata kundi lingine nje ya vyama vya siasa, linaloweza kufanya kazi hiyo muhimu kwetu sote.
 
Yupo sahihi 100%.Umesikia upinzani ukiongelea mgao wa umeme unaondelea?Umesikia upinzani ukipinga vikali mkataba wa bandari?Hii serikali ni ya ovyo kuwahi kutokea lakini upinzani upo kama haupo.
Naongezea.
Wakati suala la mkataba wa uwekezaji wa Bandari umezuka, na nipo tayari kusahihishwa, Mbowe et al walikaa kimya kwa mda mrefu kweli, nadhani, walitegemea vuguvugu lile liishe na mambo yaendelee kama kawa. Haikuwa hivyo!

Sasa baada ya kuona yale majaribio yao kujitambulisha tena kwa Wananchi(operation 255) yamekufa, manake yale maigizo-Kurukaruka na helikopta, mara kupigiwa saluti na Askari, mara mtoto wa miaka 9 kumlilia Mbowe, mara kutembelea kaburi la mwanasiasa mkongwe, mara yupo Ikulu kupiga picha n.k n.k kubuma Ikabidi waanze upya.

...na kuanza huko walibidi wateke headlines, ndio akatokea mbowe na kauli yake ile ya "Uzanzibari" after the fact

Kilichfanyika ni kufunika kabisa mijadala ambayo kwa wiki chache kulionekana uwepo wa Umoja, yaani ulikuwa hauwezi kuotofautisha uzalendo au itikadi za kichama, uwe CCM au chama kingine chochote au usiwe na chama, watu wengi walionekana wakitetea Rasilimali yao, Bandari.

...255, imebuma, Lissu kakimbilia kutomaswa(massage therapy) ubeligiji huku kukiwa na tetesi za mgawanyiko ndani ya CHADEMA, CHADEMA walikuwa wamekosa headlines chanya!

Opportunity ikatokea, wakabidi waingie kwenye reli pamoja na wanaharakati, lakini hawakuingia kuendeleza mjadala, hapana, waliingia kuufunika. Wakaanza kukimbizana na Kaburi la Hayat, mara Katiba, mara Uchaguzi na vimbwanga vingi tu kuwachanganya Wananchi kama walivyopaswa na masharti ya Maridhiano yao ya awali- Toka jela, Kula Ruzuku, Sifia SSH, kandamiza legacy and so forth badala ya kukalia papo tu, yaani, KUSITISHA mkataba, Urudishwe Bungeni uwe kalas.

Wameniudhi, wametuudhi, na ndio katika mlolongo huo wa kutuchanganya ndipo wananchi sasa wanaanza kuona Mbadala haueleweki, hususani ukija upande wa Upinzani, pamoja na kwamba nimeishikia bango CCM ijivue tu madaraka, Wanachama warudishe kadi, lakini sidhani kama CHADEMA wapo na Dhamira ya kutuvusha tulipo. Na kama ilivyosemwa huko juu, wapo kutaka kugawana madaraka 2025.

.... wapo lakini hawapo.
 
Wakiitisha maandamano mtatoka?au mnataka Mbowe na familia yake wawapiganie mkiwa kwenye keybord? Wajinga nyie
Akili zako zinafikiri maandamano yanaweza kukukomboa, poor brain, maandamano ni upuuzi na kuharibu taifa hasa yule mnaetaka aondoke atakapokomaa, what's follow up!, dumb!
 
Kazi ya Wakili imekwisha kamilika.

Tunashukuru Wakili Msomi kwa kupeleka Mjadala ule wa Bandari kwa namna ile hadi kufikia hitimisho lile

najivunia kuwa CCM ambayo tangu kuanza kwake imekuwa mbele ya muda kwny mijadala yote inayotishia umoja na mshikamano wa Taifa

Chadema pia inathamini sana amani kwa kuwa inajua bila ya amani hakuna ruzuku

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
Ruzuku ndiyo mpango mzima, sasa ikikosekana amani kutakuwa na ruzuku?
 
Upinzani serious lazima uwe na backup ya wananchi
Upinzani serious lazima uanze kutengeneza backup ya wananchi na hii ni kwa kuzungumza mattz yanayowagusa wananchi direct. Ni maajabu leo tuna shida ya umeme lakini upinzani uko busy kuwaambia tunataka tume huru, unafikiri watapata backup yoyote toka kwa wananchi?Mwanasiasa serious Anaweka maslai ya wananchi mbele then kidogo kidogo anachomekea agenda zake.Sasa hawa wa kwetu daily wako busy na agenda zao za kutaka washinde uchaguzi.
 
Back
Top Bottom