Wakili Mwakubusi: Vyama vya Upinzani kazi yao ni kufukuzia tu ubunge na ruzuku, haviwezi kulikomboa Taifa

Mnasema people's power,hizi story za dora unatoa wapi?Tukiwa na upinzani imara hao polisi sio kitu. Tuna upinzani wa ovyo ndio maana mnakuja na story za oooh polisi mara dora.Mwaka 2007 Dora ilitumika Kenya kuzima nguvu ya umma na ikashindwa na mwisho wakapata katiba mpya. Huku tuna upinzani unaoleta porojo za maridhiano mara oooh ccm inatumia dora. Dora si kitu kwa upinzani serious. Again,Mbowe na genge lake sio wapinzani tena na katu Hawawez kulivusha Taifa toka mikononi mwa nyang'au ccm
Anzisha chama Cha upinzani kifanye upinzani kwa mtazamo wako. Hao wapinzani wakifanya unachosema sio ndio mnakimbilia humu kujiliza kuwa amani ya nchi inaharibiwa kwa uchu wa madaraka?
 
Dude kubwa kwenye nini?.labda kupora mali za umma na kufisadi nchi.Kama ni hivyo sawa.ila Ccm haina ukubwa wowote zaidi ya kujimilikisha serikali iliyorithi toka uhuru.
Huko kujimilikisha ndio ukubwa ninao uzungumzia
 
Mnasema people's power,hizi story za dora unatoa wapi?Tukiwa na upinzani imara hao polisi sio kitu. Tuna upinzani wa ovyo ndio maana mnakuja na story za oooh polisi mara dora.Mwaka 2007 Dora ilitumika Kenya kuzima nguvu ya umma na ikashindwa na mwisho wakapata katiba mpya. Huku tuna upinzani unaoleta porojo za maridhiano mara oooh ccm inatumia dora. Dora si kitu kwa upinzani serious. Again,Mbowe na genge lake sio wapinzani tena na katu Hawawez kulivusha Taifa toka mikononi mwa nyang'au ccm
Anzisha chama Cha upinzani kifanye upinzani kwa mtazamo wako. Hao wapinzani wakifanya unachosema sio ndio mnakimbilia humu kujiliza kuwa amani ya nchi inaharibiwa kwa uchu wa madaraka?
Upinzani inataka maslai ya wananchi yawe mbele.Leo wananchi tunalia peke yetu utasema hatuna upinzani. Ukweli lazima usemwe, hatuna upinzani bali genge la wahuni
Hao wananchi wao wamekufa wanasuburiwi kusemewa tu? Hao wananchi wakiambiwa Leo wajitokeze kushinikiza tatizo la umeme lipatiwe ufumbuzi wa kudumu, si ndio husema wanajali amani kuliko umeme?
 
Anzisha chama Cha upinzani kifanye upinzani kwa mtazamo wako. Hao wapinzani wakifanya unachosema sio ndio mnakimbilia humu kujiliza kuwa amani ya nchi inaharibiwa kwa uchu wa madaraka?
Mwenyekiti aache kulinda mahusiano na watawala waliomuwezesha kukomba malimbikizo ya ruzuku ya 2 billion kwa sababu Tanesco wanaboresha miundombinu ?

Tuachane na Kamanda Mbowe, wewe ungekuwa na fursa kama yake ungetishia usalama wa ruzuku ya Chama kwa sababu ya tanesco?
 
Mazombi km nyie ndio mtaji wa wanasiasa matapeli.
Hakuna upinzani Tanzania wote matapeli tu,
Ndio maana Ccm wanafanya wanavyotaka. Upinzani ulikuwepo angalau 2005-2015.
Kama wanafanya wanavyotaka na nyie wananchi mmeridhia msiwalaumu chadema ambao mnawaita matapeli
Tulieni sindani iwaingie ikiwemo ya mgao wa umeme
 
Anzisha chama Cha upinzani kifanye upinzani kwa mtazamo wako. Hao wapinzani wakifanya unachosema sio ndio mnakimbilia humu kujiliza kuwa amani ya nchi inaharibiwa kwa uchu wa madaraka?

Hao wananchi wao wamekufa wanasuburiwi kusemewa tu? Hao wananchi wakiambiwa Leo wajitokeze kushinikiza tatizo la umeme lipatiwe ufumbuzi wa kudumu, si ndio husema wanajali amani kuliko umeme?
Hii nchi ina watu wa hovyo sana chadema wameaanza kufanya mikutano ya hadhara wanalaumiwa wanatukana, wanataka wananchi waandamane hawataki, wamekaa kimya ni kosa, mbowe katuhumiwa kwamba ni gaidi wananchi kimya sasa chadema wanalaumiwa kwa lipi
 
Nilishangaa sana kwanini ule moto wa bandari Chadema walikua nyuma nyuma sana?Watu wanapewa kesi ya UHAINI wao wapo wapo tu,mtu aseme Chadema ni chama cha SIASA?No,hili ni genge la wahuni.
Walikuja kuuzima Kiaina. Fuatilia yote, walivyojikita tu na 255, pakavurugika, pakaja mambo ya Udini, Uzanzibari, mara "special interest' halafu ikawa 'nyie wapinzani'-ndio mnaoleta fyoko fyoko. Yote kuzima mijadala ya Bandari na DPW.

Sasa wanawatolea nje Kina Dr Slaa!
 
"Vyama vyetu vya siasa nadhani aidha vimechoka sana vyote vinahitaji kupumzika au viongozi wake wamechoka sana wanahitaji kupumzika, na ndio maana wanapoteza ile hamu ya kulikomboa na kulisimamia taifa, wanakuwa watu wa kufukuzana na tuvyeo, ubunge, ruzuku, kugawana, kukaa kaa mezani.

Kila mmoja yuko bize, wanachotaka ni kugawana tu sio kupambana kwa ajili ya wananchi. Lakini kikubwa ninachojaribu kusema kwamba inawezekana katiba kupatikana bila wanasiasa.” – Wakili Boniphace Mwabukusi

Chanzo: Swahili Times
Sawa.lakini kukiondoa chama madarakani should be a process angalau ya 10 years. Unaanza na kuwa na wabunge wengi ,then ndipo unaipata Kura nyingi za uraisi!!huwezi kusema utachukua Nchi bila ya kuwa na wabunge wengi
 
Watanzania sio manyumbu wa kurndeshwa kwa mihemko ya siasa za kikabila kama Kenya , Watanzania wana imani na serikali ya CCM ndio maana hata aje mtu gani hawezi kuwashawishi watanzania waandamane wavuruge amani, hata akifufuka mwendazake awaambie waandamane hatapata watu labda huko kwao Chato
Lakin wanaishi kwa maumivu makali sana mioyoni mwao
 
Walikuja kuuzima Kiaina. Fuatilia yote, walivyojikita tu na 255, pakavurugika, pakaja mambo ya Udini, Uzanzibari, mara "special interest' halafu ikawa 'nyie wapinzani'-ndio mnaoleta fyoko fyoko. Yote kuzima mijadala ya Bandari na DPW.

Sasa wanawatolea nje Kina Dr Slaa!
Mabadiliko sio swala la chadema acha uzwazwa ni swala la kila mtu mfano umeme unavyosumbua unasumbua kwa watu wote bila kujali ni chadema, hauna chama au ccm

Kama we ni mwanaume uliyekamilika alafu unataka mwanaume mwenzako akupiganie kwa niaba yako tunasafari ndefu sana kama nchi
 
Walikuja kuuzima Kiaina. Fuatilia yote, walivyojikita tu na 255, pakavurugika, pakaja mambo ya Udini, Uzanzibari, mara "special interest' halafu ikawa 'nyie wapinzani'-ndio mnaoleta fyoko fyoko. Yote kuzima mijadala ya Bandari na DPW.

Sasa wanawatolea nje Kina Dr Slaa!
Hivi kwa nini Slaa na Mwabukusi wasiungane na kuunda chama cha siasa kama kweli wana agenda ya maana?
 
"Vyama vyetu vya siasa nadhani aidha vimechoka sana vyote vinahitaji kupumzika au viongozi wake wamechoka sana wanahitaji kupumzika, na ndio maana wanapoteza ile hamu ya kulikomboa na kulisimamia taifa, wanakuwa watu wa kufukuzana na tuvyeo, ubunge, ruzuku, kugawana, kukaa kaa mezani.

Kila mmoja yuko bize, wanachotaka ni kugawana tu sio kupambana kwa ajili ya wananchi. Lakini kikubwa ninachojaribu kusema kwamba inawezekana katiba kupatikana bila wanasiasa.” – Wakili Boniphace Mwabukusi

Chanzo: Swahili Times
Naunga mkono hoja 👍👏
 
Unaangalia mambo kwa namna mbaya unayoitaka wewe.kama ukuona agenda za maana zilizozungumzwa kwenye ile mikutano wewe ndiye utakayekua na shida sio chadema.ndo maana Umeangaika na porojo za watu badala ya agenda ndo maana ukaondoka na porojo ukaacha mambo ya msingi.
Sijakataa walikuwa na Agenda. Na sijasema kulikuwa hakuna Agenda za Maana.... Nimezungumzia The Original campaign ya 255 ambayo walikuwa nayo na agenda zote, mfano Katiba Mpya, Maridhiano, Tume ya Uchaguzi n.k n.k lakini ikabuma and that is a fact.

Hii ya pili wakaja kuongezea Okoa bandari! Lakini badala ya kuokoa Bandari, kitu ambacho kilikuwa na vuguvugu kubwa sana, wao wakazima, wakaanza kugombana na kaburi. That is a fact.

Ndugu, sijahangaika popote ndugu, taarifa na habari zote zimo hapa hapa JF. Kubali tu yaishe.

Na kama hutaki, nitajie hayo mambo ya msingi niliyoyaacha ili niweze kuangalia kwa namna nzuri Please. Tunaelimishana
 
Mwenyekiti aache kulinda mahusiano na watawala waliomuwezesha kukomba malimbikizo ya ruzuku ya 2 billion kwa saba
Mwenyekiti aache kulinda mahusiano na watawala waliomuwezesha kukomba malimbikizo ya ruzuku ya 2 billion kwa sababu Tanesco wanaboresha miundombinu ?

Tuachane na Kamanda Mbowe, wewe ungekuwa na fursa kama yake ungetishia usalama wa ruzuku ya Chama kwa sababu ya tanesco?
Ruzuku gani boss, huo uchafu nayo ni ruzuku?
 
Sijakataa walikuwa na Agenda. Na sijasema kulikuwa hakuna Agenda za Maana.... Nimezungumzia The Original campaign ya 255 ambayo walikuwa nayo na agenda zote, mfano Katiba Mpya, Maridhiano, Tume ya Uchaguzi n.k n.k lakini ikabuma and that is a fact.

Hii ya pili wakaja kuongezea Okoa bandari! Lakini badala ya kuokoa Bandari, kitu ambacho kilikuwa na vuguvugu kubwa sana, wao wakazima, wakaanza kugombana na kaburi. That is a fact.

Ndugu, sijahangaika popote ndugu, taarifa na habari zote zimo hapa hapa JF. Kubali tu yaishe.

Na kama hutaki, nitajie hayo mambo ya msingi niliyoyaacha ili niweze kuangalia kwa namna nzuri Please. Tunaelimishana
Unajua ccm kamwe hawawez ruhusu katiba nzuri na bora, na tume huru sababu wakikubali tu ndo mwisho wao

Unajua mbadiliko yanahitaji support ya wananchi mfano angalia odinga kenya akisema kesho tunaandamana support wanakuja kwa wingi

Swala la katiba bora au tume huru sio swala la chadema huu ndo ujinga ambao wewe na watanzania wengi mnao mfano kwenye ripoti ya CAG watu wamekula hela mpaka leo wapo ofisini hio ni kwa sababu ya katiba mbovu na mambo mengine mengi ya hovyo yanayofanya lakin huo mzigo kabebeshwa chadema pekee yake tena analaumiwa as if sisi wengine hayatuhusu hii nchi tuna safari ndefu sana
 
Hivi kwa nini Slaa na Mwabukusi wasiungane na kuunda chama cha siasa kama kweli wana agenda ya maana?
Hayo maswali kuhusu kuundwa kwa Chama ni mazuri Ukiwauliza Daktari Slaa au Mwabukusi.

Ukija kwenye agenda, naona unachanganya mambo, unataka kuminimise. manake Ukisema agenda yao ya Kutafuta haki kwa Wamasai ndugu zetu na kulinda Rasilimali(Bandari) sio za maana, ina maana hata ile 255 okoa Bandari sio ya maana. Nafikiri suala lipo wazi, DK Slaa na Mwabukusi wapo zaidi kuumulika Mkataba wa Bandari. Hao wengine wapo wanafanya Jogging na wengine kwenye Maridhiano. Yani wapo hawapo.
 
Back
Top Bottom