Wakili Mwambukusi huenda akashidwa kwenye kura uchaguzi wa TLS

Ila kama hawa ni wengi si ndio Demokrasia yenyewe ? Au wameshawishiwa kwa Mlungula and if that is the case hata Taasisi yenyewe itakuwa haina legitimacy....
Walivyokata jina lake tu kwenye hukumu ya mahaka jaji kahoji hivi nyinyi TLS mnajitambua kweli?
 

Mbona unahaha sana ndugu Boi Manda?

Kwani cha ajabu ninini hata ikitokea ameshindwa?

Si ndiyo maana ya uchaguzi kwamba kuna options nyingi za kuchagua?

Mimi nafikiri, lililo muhimu kwa sasa ni kuhakikisha kuwa mchakato wote wa uchaguzi (kuanzia uteuzi wa wagombea, kampeni, upigaji kura, uhesabuji kura na kutangazwa kwa matokeo) lazima uwe FAIR and JUST ili kila mgombea ashinde au ashindwe kwa haki kwa maamuzi ya wapiga kura wenyewe.

Na kama transparency itatawala ktk uchaguzi huu, mimi sijaona mgombea mwingine miongoni mwa watano ambaye aggresive and vibrant kupambana na utawala huu wa kihuni chini ya CCM anayeweza kumshinda Mwabukusi.

Hawa wengine wote watano ukiwasikiliza na kuwatazama usoni wanapokuwa wanaongea unaona waziwazi kuwa wananunulika na wanaweza kuiuza TLS kirahisi tu kwa tamaa ya fedha. Lakini si Boniface Mwabukusi ambaye yeye si kwa kusema mdomoni tu bali amethibitisha hili kwa vitendo!

Na mimi nikuhakikishie jambo moja ndugu Boi Manda figisu figisu anazopitia na kufanyiwa Wakili Boniface Mwabukusi kwa sababu ya misimamo yake mikali dhidi ya wahalifu wa sheria na katiba, ni za kitoto sana ukilinganisha na alizopitia na kufanyiwa Tundu Lissu mwaka 2017 na bado alishinda uchaguzi huo kwa kishindo..!!

Wao watumie kila aina ya silaha walizonazo kuzuia ushindi wake. Wachote na kumwaga pesa zote kwa mawakili. Jambo moja ni hili, tutachukua na kuzitumia fedha hizo lakini, yet kura zote ni kwa Boniface Mwabukusi!!

Take it or throw it , but always remember this, that, Adv. Boniface Mwabukusi iwe jua au mvua ndiye Rais wa TLS kwa miaka mitatu ijayo 2024 - 2026. Cha kumzuia Boniface Mwabukusi kushinda uchaguzi huu ni kifo pekee ambacho Mungu hajakiruhusu kwa sasa!!

TLS inahitaji kichwa ambacho ni vibrant and aggressive cha mtu kama Adv. Boniface Mwabukusi ktk kupambana na hayawani wa CCM waliozoea kuvunja sheria na katiba ya nchi bila hatua kuchukuliwa dhidi yao!
 
Kushindwa kihalali siyo kosa wala dhambi.
 
Siyo tu wao kuna mawakili wengi zaidi ni vichwa ukielewa dhana ya demokrasia na uwajibikaji utaelewa kwanini watu wanataka katiba mpya na utawala bora. Huhitaji kufungua Whatsapp group kuchagua watu wakati kuna utaratibu wa kidemokrasia wa kupiga kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…