Wakili Peter Madeleka akamatwa na polisi baada ya Mahakama Kuu kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP

Wakili Peter Madeleka akamatwa na polisi baada ya Mahakama Kuu kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP

Mbinu batili za kuwazuia watanganyika wasidai bandari zao walizopewa waarabu milele, Samia ni mwongo na msaliti mkubwa sana kwa watanganyika, na ni kiongozi dhaifu pia, kwani anachokisema hakitekelezwi na watendaji wake na hawafanyi kitu.
Eti wale wa "plea bargain" wote walimaliza madeni yao ?!!!
 
Kuna wale wanatishia watu kuwakabidhi kwa machief!

Hii inadhihilisha kuwa, ccm, uovu wao wanaulinda kwa uovu! Wanatuma mapolisi kuwadhibiti watu ili wautetee uovu kwa nguvu zao zote! Na sisi kama watanganyika,

Watu wema wanaotetea haki, tutawakabidhi kwa Mungu mkuu wa haki na mwenye hukumu za haki dhidi ya uovu!

Nijualo ni moja tu! Jambo lenye haki, halilindwi kwa njia haramu!

Rudisheni bandari na ama mboreshe mkataba
Eti wale watuhumiwa waliomalizana" kupitia "plea bargaining" wote walimaliza madeni wanayodaiwa?!!!
 
Ni sarakasi tu za wenye mamlaka.

Ina maana walikuwa wanaachiwa hata kwa mali kauli?

Nini kimebadilika hadi waanze kukamatwa tena?

Ni yeye pekee hajalipa?
 
Hatari sana juzi ripoti ya Haki Jinai aliyotoa jaji mstaafu Mohamed Othman Chande na baadaye kauli ya mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. Samia Suluhu Hassan kuwa taasisi na viongozi waliopo katika mfumo wa haki jinai wabadilike bado haijaweza kuwafikia watendaji waliopo katika kuhakikisha haki ndani ya mfumo wa haki jinai Tanzania

View attachment 2690768
Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 15 July 2023 amepokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai kutoka kwa Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Othman Chande, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Hii ni Vita kamili
 
Sasa chawa ayashikiwaje akili kwani zipo sasa?
20230620_204309.jpg
 
Unamkamata kisa tu kakwambia ukweli kwamba DP World ni kampuni ya kitapeli. 🙂
 
Hata mkimkamata Bandari haiuzwi,kauzeni ya Zanzibar
wazanzibar wanashirkikiana kuuza mali za Tangayika, hili tumewagomea - yes wakauze za kwao. afu na nyie wapemba mmezagaa tanganyika raha mustarehe, sasa tunasemajeeee - mjiandae mkabananiane huko kwenu. 😀😀
 
wazanzibar wanashirkikiana kuuza mali za Tangayika, hili tumewagomea - yes wakauze za kwao. afu na nyie wapemba mmezagaa tanganyika raha mustarehe, sasa tunasemajeeee - mjiandae mkabananiane huko kwenu. 😀😀
Propaganda hizo zimegonga mwamba.😂
 
Unamkamata kisa tu kakwambia ukweli kwamba DP World ni kampuni ya kitapeli. 🙂
Madeleka kutoka Polisi alifungua kampuni yake ya UWAKILI. Halafu kumbuka Mrs Madeleka alikuwa ni Mtumishi wa IMMIGRATION Mkoa wa Arusha akiwa kitengo kinachohusiana na wahamiaji haramu.

Kesi zote ambazo Peter Madeleka alikuwa anashinda zilikuwa zinaharibiwa na mkewe ofsini. Na wahamiaji haramu wengi alikuwa anawasukuma kwa mumewe kwa ajili ya kutetewa mahakamani.

Hivyo Madeleka na mkewe walihujumu sana jeshi la Immigration Arusha hadi baadaye uongozi wa Makao Makuu ukagundua.

Kilichofuata ni mke wa Madeleka kuhamishwa kitua na hatimaye kuacha kazi Immigration.

Na hiyo ndiyo sababu kubwa ya bifu la Madeleka dhidi ya Makakkala, CG wa Immigration.

Madeleka siyo msafi hata kidogo, ndiyo maana alikubali kusaini "plea bargaining"
 
Watu wengi wanashindwa kuelewa jambo moja, kilichotokea kwa Madeleka kukamatwa ni sawa sababu faili lake limerudishwa polisi wao warudishe kwa DPP alafu kesi iendelee pale ilipoishia.

Sasa mambo ya Tume ya kuchunguza haki jinai hapa yanaingia kwa udogo sana sababu Madeleka hajashinda kesi ya msingi bali ni ombi tu linalorudisha ile kesi ya msingi.

Kwa ufupi sana ni kwamba Madeleka ni mtuhumiwa kwa sasa, na ni mtuhumiwa kwa ile ile kesi yake ya awali ambayo kimsingi yeye mwenyewe ndio ameona sasa bora akapambane na ile kesi ya awali kwa kupinga alichokubaliana na DPP.

kwa ufupi sana jambo lake limekaa hivyo.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha leo tarehe 17 Julai 2023 imefuta Plea Bargain iliyoingiwa Kati ya DPP na PETER MADELEKA. Hata hivyo RCO Arusha ametuma Askari Wanikamate nikiwa Mahakamani. Bado sijatoka Kwa Jaji.

Hukumu iliyosomwa leo na Mahakama Kuu ya Tanzania Arusha mbele ya JAji Bade, licha ya Kufuta Plea Bargain Kati ya DPP na PETER MADELEKA, ilikuwa imeshajulikana Kwa Polisi na DPP Kabla ya kusomwa na Mahakama ikasaidia Mazingira ya Mimi kukamatwa.

Ameandika Wakili Peter Madeleka, Twitter
Plea bargain inafutwaje na Mahakama?

Amandla...
 
Back
Top Bottom