Wakili Sweetbert Nkuba kupinga ushinda wa Wakili Boniface Mwabukusi kuwa Rais wa TLS

Wakili Sweetbert Nkuba kupinga ushinda wa Wakili Boniface Mwabukusi kuwa Rais wa TLS

Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa chama cha Wanasheria nchini TLS, Wakili Sweetbert Nkuba amekataa kutambua ushindi alioupata mpinzani wake wa karibu Mwabukusi kwa madai ya ukiukaji wa mwenendo wa uchaguzi.

Pia soma: Uchaguzi wa TLS 2024: Boniface Mwabukusi ashinda Urais, apata kura 1274

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Nkuba amesema ameshawasiliana na wanasheria wake ili kwenda kupinga ushindi wa Mwabukusi mahakamani.

"Mojawapo ni kuona karatasi za kupigia kura kuisha na kwenda kuchapishwa zingine, kufanyiwa vurugu na kusambaa taarifa mitandaoni ushindi wa mpinzani wangu kabla ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi," amesema Nkuba

Katika uchaguzi huo uliofanyika Jana na matokeo yake kutangazwa usiku, Wakili Nkuba alizidiwa zaidi ya kura 400 na mpinzani wake Wakili Mwabukusi ambaye alitangazwa kuwa mshindi.

View attachment 3060290
Anaitwa "Sweet"!Si kosa lake.
 
Kama kura zilikuwa hazijapigwa hayo hayawezi kuitwa matokeo ya uchaguzi bali uvumi. Pia mbona uvumi wa nani kashinda na nani kashindwa uwa upo siku zote kwenye kipindi cha chaguzi zote hata kabla kura hazijahesabiwa. Uvumi ndiyo uhalalishe jambo?
Yeah ni maneno ya mfamaji.
Yaani ni sawasawa timu ziingie uwanjani halafu waanze kupoteza muda kuwanyamazisha mashabiki wasishangilie badala ya kuzingatia mpira unavyochezwa uwanjani
 
Mwaka 1 tu.

Na shamrashamra huwa ni siku ya uchaguzi tu. Baada ya hapo huwasikii tena.
😀😀😀😀😀hivi wanakuwaga wapi baada hapo?Na kwenye huo muda wanatumikia kuna mshahara au ruzuku huwa wanalipwa?au ni kazi ya kujitolea?
 
Attachments

  • IMG-20240803-WA0115.jpg
    IMG-20240803-WA0115.jpg
    56.5 KB · Views: 2
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Rais wa chama cha Wanasheria nchini TLS, Wakili Sweetbert Nkuba amekataa kutambua ushindi alioupata mpinzani wake wa karibu Mwabukusi kwa madai ya ukiukaji wa mwenendo wa uchaguzi.

Pia soma: Uchaguzi wa TLS 2024: Boniface Mwabukusi ashinda Urais, apata kura 1274

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Nkuba amesema ameshawasiliana na wanasheria wake ili kwenda kupinga ushindi wa Mwabukusi mahakamani.

"Mojawapo ni kuona karatasi za kupigia kura kuisha na kwenda kuchapishwa zingine, kufanyiwa vurugu na kusambaa taarifa mitandaoni ushindi wa mpinzani wangu kabla ya kutangazwa na msimamizi wa uchaguzi," amesema Nkuba

Katika uchaguzi huo uliofanyika Jana na matokeo yake kutangazwa usiku, Wakili Nkuba alizidiwa zaidi ya kura 400 na mpinzani wake Wakili Mwabukusi ambaye alitangazwa kuwa mshindi.
Ametumwa na huenda jaji ametayarishwa, hivi sasa anapewa maelekezo kama aliyopewa Msigwa mhamiaji.
 
Nkuba kasoma Korogwe Primary School pale Kahama, ikafuatia Wigehe Secondary School halafu Ujiji Seminary.

Haya tuambie ulichotamani kusema mkuu.
Ni kweli katelekeza familia kisa miss Tanzania ?
 
Hayo machapisho yaliyofanyika mitandaoni sio kutangaza huko.

Au unafikiri kutangaza ni mpaka mtu ashike mic 🎤 aongee.
Kama ambavyo Wakili Msomi Julius Mtatiro alivyompongeza ni tangazo pia!
 
amesema Nkuba

Sweetbert Nkuba wakili msomi, ametumwa na chama dola kongwe kupinga matokeo ya uchaguzi.

Uchaguzi huu wa TLS iwe rejea jinsi ya kuandaa mchakato mzima wa uchaguzi wa nchini Tanzania 2024 / 2025 uwe huru na haki.

Na haki hii ya kada Nkuba kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi TLS ni somo zuri la uraia kuhusu wafanye nini raia wapiga kura 2024 / 2025 katika uchaguzi unaosimamiwa na makada wa CCM kupita kofia yao ya Mkurugenzi wa Halmashauri DED.
 
Back
Top Bottom