Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA , Tundu Lissu akielezea sababu zilizomfanya arudi nyumbani Tanzania baada ya miaka 5 akiishi ugenini. Hii ni hatua njema hususani katika kuimarisha demokrasia nchini, Rais Samia Suluhu Hassan wakati anaingia madarakani alisema matamanio yake ni kujenga nchi mmoja yenye mshikamano bila kujali tofauti zetu za kiitikadi.
Katika kufanikisha hayo aliamua kuja na nguzo nne za uongozi wake ambazo ni Uvumilivu, Ustahamilivu, Maridhiano na Kujenga Upya.