Haya yote yanatokea kwa sababu utopolo sio wana michezo bali kundi la wahuni waliobahatika kupata pesa .Wakili Salum Nduruma ambaye anamuwakilisha mchezaji Feisal Salum katika mgogoro wake wa kimkataba dhidi ya Yanga amesema wamepokea nakala ya maamuzi ya Kamati na mteja wake hana mpango wa kurejea Yanga kuendelea kuichezea timu hiyo.
“Feisal Salumu mpaka sasa hivi hana mpango wa kurudi na kuichezea Yanga na msimamo wake ni uleule kwamba anataka kuendelea kupinga hayo maamuzi kwa sababu anaona hayakumtendea haki… njia iko nyeupe kwenda CAS,” amesema na kuongeza:
“Hukumu tuliyopewa haina tofauti na kile kilichotolewa wiki iliyopita na Kamati. Tunataka kuwaandikia FIFA kuwaelezea mazingira yote yalivyokuwa ili kama inawezekana wakati Fei anaendelea na rufaa aweze kusajiliwa katika dirisha moja."
Kwani yanga haiwezi bila Fei?Kama jibu sio,kwa nini kumkomalia kijana aliyewapa heshima uwanjani mara nyingi badala ya kumwacha aende kutafuta malisho ya kijani sshemu nyingine?Ama mpeni japo milioni 16 ili atulie kuliko kumlazimisha acheze kwa milioni 4 tu wakati Aziz analipwa milioni 25 kwa mwezi.
Huko utopoloni watu wenye akili ni wawili tu ila nao si viongozi.
Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app