Mkuu options namba 1 na 2 hazitekelezeki Yanga watamlima barua ya Kuvunja Mkataba. Hivyo, wataomba walipwe fedha kwa ajili ya suala hilo.
Watamlima barua sawa, ila itakuwa ni kwa ajili ya kutimiza utaratibu tu kwamba Yanga walichukua hatua kuhusu hilo.
Lakini Yanga haiwezi kupoteza muda kumdai Fei Toto pesa.
Yanga ilichokuwa inasubiria (au itakachokuwa inasubiria kama atagoma kurudi) ni kuona Fei Toto ataibukia timu gani ya mpira wa kulipwa. Hiyo timu ndo Yanga itaidai.
Kwenye kesi za madai busara ni kumfungulia kesi mtu mwenye hela. Kumdai maskini ni kupoteza muda. Unaweza ukashinda kesi lakini maskini hana hela ya kukulipa kwa hiyo ushindi wako unakuwa hauna maana.
Hata hivyo, kwa weledi ilioonesha TFF katika kushughulikia suala hili ina maana Fei Toto hataweza kusajiliwa na timu yoyote ya mpira wa kulipwa. Maana ili asajiliwe nchini Tanzania ni lazima asajiliwe kwenye mfumo wa TFF. Kwa kuwa TFF imeshasema ni mchezaji halali wa Yanga, ni dhahiri kuwa haitaweza kumbadilishia usajili na kukiuka hukumu iliyotoa.
Na ili akacheze nje ya nchi kwenye soka la kulipwa ni lazima apate kibali cha TFF ili kulinda maslahi ya taifa (kwamba aweze kuitwa kwenye timu ya taifa akihitajika) na maslahi ya kilabu anayotokea hapa nchini. Hapo tena ni dhahiri kuwa atakwama. TFF haiwezi kumpa hicho kibali wakati imeshasema ni mchezaji wa Yanga. Ni lazima timu ya nje ya mpira wa kulipwa itakayomtaka imalizane kwanza na Yanga.
Kwa hiyo utaona kwamba mazingira ya yeye kuendelea kucheza mpira wa kulipwa bila ya timu anayotaka kuchezea kumalizana na Yanga hayapo. Ndo maana nasema aidha atafute shughuli nyingine ya kufanya au akacheze mpira wa ridhaa. Huko Yanga itamlima barua tu lakini haitahangaika kwenye kesi.
Shida ya yote haya ni kwamba kama kuna timu iliyokuwa inamtaka, hiyo timu ilimtaka kwa njia za panya. Badala ya timu hiyo kumalizana na Yanga, yenyewe ikaamua kutumia njia za uchochoroni ili impate kwa bei nafuu.
Kitu ambacho kinapaswa kulaaniwa na wapenda mpira wote. Hii sio ishu ya uSimba na uYanga. Ni ishu ya ustaarabu wa mpira kuhakikisha kwamba timu zinavuna matunda ya uwekezaji kwa wachezaji.