Wakili wa Fei Toto asema wamepokea hukumu lakini Fei hana mpango wa kurudi Yanga

Wakili wa Fei Toto asema wamepokea hukumu lakini Fei hana mpango wa kurudi Yanga

Kabisa solution ni kwamba Azam wakae mezani na Yanga SC wamalizane nao wamchukua Feisal wao.
Kwan mmeambiwa Azam ndo wanamtakaa fei? Ushahidi ni upiii?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] malizaneni na fei wenu.

Mmevurugwaaaa vibayaaaa khaaaah
 
Kama hayuko tayari kurudi Yanga basi ana options zifuatazo:

1. Akatafute shughuli nyingine ya kumuingizia kipato mpaka mkataba wake na Yanga utakapokwisha.
2. Akacheze mpira wa ridhaa.
3. Amuombe huyo anayemrubuni aongee na Yanga ili Yanga imuuze. Yanga ikipewa mzigo wa maana inamwachia Fei Toto.

Kwenye kanzidata ya mawakili wa Tanzania, hakuna wakili anayeitwa Salum Nduruma. Ndo maana dogo anaingizwa machaka.
Hee punguzeni uwongo
 
Rudi kasome kanuni na sheria za FIFA kuhusu kuvunjwa kwa mkataba.
Hivyo ndivyo vipengele anavyapaswa kufuata.
Usisumbue watu
Wee uliyesoma ndo ulipaswaa uje na hizo kanuni hapa, nisumbue watu kwa lipiiii? Km mna haha na fei hizo shida zangu,

Afu sikua nakujibu wee, huo usumbufu unajipaa mwenyeweee.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mmevurugwaa vibayaaa, poleeeni
 
Kushindwa kuona hoja za Fei ni lazima uwe na roho ya kichawi.
Nawatahadharisha kuwa kuna wachezaji wengine wazawa wanaumia jinsi mnavyomchukulia Fei muda huu,na wanawaona hamna maana.
Subirini siku yenu ambayo maji mtaita "mma"

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Kwa bahati mbaya sana Feisal alisain extension ya mkataba wake 2020, na akasaini wa miaka mi4 ila kabla ya miaka mi3 thaman yake imepanda na hakuna kipengere chochote alichokalisk katika mkabata kuwa kama akifanya vizuri zaidi bas mkataba urejewe upya atakama haujaisha, au mshahara upande kwa % fulan ila akiboronga pia akatwe kwa % kadhaa!
 
Siwezi kukuelewesha Kwa sababu umekuwa mgumu kuelewa mchezaji anaomba kulinda kipaji chake wakati kesi inasikilizwa.
Kesi Haina muda maalumu wa kuisha sijazungumzia kesi ya Okwi ilikuwa inahusu nini
Kulinda kipaji chake kwani Yanga wamemfukuza? Je hawamlipi mshahara?
 
Moyo wa mtu kichaka jamani..kama kweli anataka kwenda CAS maybe ana ushahidi wake ..mnaweza shupaza shingo anashindwa anashindwa kumbe ana ka video kake ka ukatili huko Avic town alikasevu 😆
 
Kwan mkataba wa fei na aziz ki uko sawaa? Fei ametumia kipengele ktk mkataba wake. Sasa tatizo nn? Mbna utaratibu wenyewee hawausemi ni upi wadau wa michezo waka tathimini??
Mikataba ya kazi yote iko sawa, tofauti ni baadhi ya vipengele tu. Utaratibu aliouvunja ni kwamba mkataba wake unasema anaweza kuvunja mkataba kwa kununua kwa 100m + mishahara ya miezi mi3= 12m. Lakini kabla hajafanya hivyo
1. Anapaswa kujadiliana na club yake na
2. Anapaswa kutoa sababu za kuvunja mkataba e.g hapati namba, halipwi mshahara wake, ananyanyaswa nk
Kwa fei haiko hivyo ndio maana sababu zake hazijambeba.
 
Kwan mmeambiwa Azam ndo wanamtakaa fei? Ushahidi ni upiii?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] malizaneni na fei wenu.

Mmevurugwaaaa vibayaaaa khaaaah
Msemaji wa Azam alishasema Fei ni mchezaji mzuri wangependa kuwa nae, unataka ushahidi gani zaidi.
 
Kwan mmeambiwa Azam ndo wanamtakaa fei? Ushahidi ni upiii?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] malizaneni na fei wenu.

Mmevurugwaaaa vibayaaaa khaaaah
Fei anatakiwa abinywe pumbu aache uhuni😁
 
Siwezi kukuelewesha Kwa sababu umekuwa mgumu kuelewa mchezaji anaomba kulinda kipaji chake wakati kesi inasikilizwa.
Kesi Haina muda maalumu wa kuisha sijazungumzia kesi ya Okwi ilikuwa inahusu nini
Ataombaje kulinda kipaji chake wakati kati ya masuala yanayoitwa "Extraordinary" hakuna hata moja linalomkumba kwa kipindi cha mkataba wake?
 
Kwan mmeambiwa Azam ndo wanamtakaa fei? Ushahidi ni upiii?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] malizaneni na fei wenu.

Mmevurugwaaaa vibayaaaa khaaaah
Hahaha Fei tushamalizana nae ,TFF washamaliza kazi ,kama anakimbilia CAS ajiandae kulipa 2m kufungua kesi na pili akae benchi muda wote mpaka kesi iishe ,tatu akishindwa aandae 230m kuilipa yanga.

Endeleeni kumdanganya huyo Fei wenu mtampoteza.

Ushahidi wa Azam upo DUBAI ,Boss wa azam aliyemlipia ticket,hotel na trainer.
 
Una tatizo lakutoelewa haraka ndugu!!, Ili Fifa ikupe hiyo options inategemeana na tatizo lako la msingi ni lipi!!. Kuongezeawa mshahara haijawahi kuwa tatizo la msingi kwa mchezaji tena Fifa sijui CAS watamfukuza😅.., yaani eti aende akasema nataka kuvunja mkataba kwakuwa wamekaataa kuniongezea mshahara??. Mane alitaka waongezewe mshahara na timu yake liver wakagoma, lakini mane bado alikuwa mtiifu na kuendelea kutumika Kama mchezaji wa liver, amesubir mkataba wake umeisha ameondoka...... Huyu mtoto ambaye hajacheza hata ligi ya Kenya ndio aisumbue CAS?. Tz tunachangamoto ya wanasheria wa mpira ndio maana wanampoteza....
Hata Ismail Aden Rage (Mwenyekiti wa Zamani wa Simba) amemwambia ukweli Feisal kuwa, sababu anazotumia Kuvunja mkataba na Yanga hazina mashiko hata akienda CAS ataangukia pua. Hivyo, amemshauri awe mpole ili akae mezani na Yanga kwa ajili ya kulimaliza suala lake.
 
Kama hayuko tayari kurudi Yanga basi ana options zifuatazo:

1. Akatafute shughuli nyingine ya kumuingizia kipato mpaka mkataba wake na Yanga utakapokwisha.
2. Akacheze mpira wa ridhaa.
3. Amuombe huyo anayemrubuni aongee na Yanga ili Yanga imuuze. Yanga ikipewa mzigo wa maana inamwachia Fei Toto.

Kwenye kanzidata ya mawakili wa Tanzania, hakuna wakili anayeitwa Salum Nduruma. Ndo maana dogo anaingizwa machaka.
Mkuu options namba 1 na 2 hazitekelezeki Yanga watamlima barua ya Kuvunja Mkataba. Hivyo, wataomba walipwe fedha kwa ajili ya suala hilo.
 
Mkuu options namba 1 na 2 hazitekelezeki Yanga watamlima barua ya Kuvunja Mkataba. Hivyo, wataomba walipwe fedha kwa ajili ya suala hilo.
Watamlima barua sawa, ila itakuwa ni kwa ajili ya kutimiza utaratibu tu kwamba Yanga walichukua hatua kuhusu hilo.

Lakini Yanga haiwezi kupoteza muda kumdai Fei Toto pesa.

Yanga ilichokuwa inasubiria (au itakachokuwa inasubiria kama atagoma kurudi) ni kuona Fei Toto ataibukia timu gani ya mpira wa kulipwa. Hiyo timu ndo Yanga itaidai.

Kwenye kesi za madai busara ni kumfungulia kesi mtu mwenye hela. Kumdai maskini ni kupoteza muda. Unaweza ukashinda kesi lakini maskini hana hela ya kukulipa kwa hiyo ushindi wako unakuwa hauna maana.

Hata hivyo, kwa weledi ilioonesha TFF katika kushughulikia suala hili ina maana Fei Toto hataweza kusajiliwa na timu yoyote ya mpira wa kulipwa. Maana ili asajiliwe nchini Tanzania ni lazima asajiliwe kwenye mfumo wa TFF. Kwa kuwa TFF imeshasema ni mchezaji halali wa Yanga, ni dhahiri kuwa haitaweza kumbadilishia usajili na kukiuka hukumu iliyotoa.

Na ili akacheze nje ya nchi kwenye soka la kulipwa ni lazima apate kibali cha TFF ili kulinda maslahi ya taifa (kwamba aweze kuitwa kwenye timu ya taifa akihitajika) na maslahi ya kilabu anayotokea hapa nchini. Hapo tena ni dhahiri kuwa atakwama. TFF haiwezi kumpa hicho kibali wakati imeshasema ni mchezaji wa Yanga. Ni lazima timu ya nje ya mpira wa kulipwa itakayomtaka imalizane kwanza na Yanga.

Kwa hiyo utaona kwamba mazingira ya yeye kuendelea kucheza mpira wa kulipwa bila ya timu anayotaka kuchezea kumalizana na Yanga hayapo. Ndo maana nasema aidha atafute shughuli nyingine ya kufanya au akacheze mpira wa ridhaa. Huko Yanga itamlima barua tu lakini haitahangaika kwenye kesi.

Shida ya yote haya ni kwamba kama kuna timu iliyokuwa inamtaka, hiyo timu ilimtaka kwa njia za panya. Badala ya timu hiyo kumalizana na Yanga, yenyewe ikaamua kutumia njia za uchochoroni ili impate kwa bei nafuu.

Kitu ambacho kinapaswa kulaaniwa na wapenda mpira wote. Hii sio ishu ya uSimba na uYanga. Ni ishu ya ustaarabu wa mpira kuhakikisha kwamba timu zinavuna matunda ya uwekezaji kwa wachezaji.
 
Yanga, achaneni na huyo kirusi Fei Toto, piga chini, mpigeni faini na aondoke zake, ila faini apigwe na aondoke zake, Yanga tunajidhalilisha sana kuhangaika na kitoto hiki
 
Kwani FIFA wanasikiliza tena kesi au wanasoma hukumu ya TFF kuona kama inamapungufu tu basi? Maana navyojua maana ya rufaa siyo kusikiliza tena ushahidi! Lakini mimi simshangai wakili wake maaana wakili hawezi kwambia kwamba hapa hutoshinda siku zote atakwambia hii tunatoboa hata kama ulikamatwa live unachinja mtu.
Mlemle mie nawafahamu sana mawakili wakiona mwanya wa kupiga hawanaga dini kabisa. Wanakupeleka chaka wapige mpunga wawapeleke watoto zao Fedha School
 
Kwanza tujiulize... Kile kipengere kinachohusu kuvunja mkataba na kurudisha pesa ya usajili na mshahara... Kwa nini kiliwekwa kwenye mkataba? Na kiliwekwa Kwa madhumuni yapi??
 
Watamlima barua sawa, ila itakuwa ni kwa ajili ya kutimiza utaratibu tu kwamba Yanga walichukua hatua kuhusu hilo.

Lakini Yanga haiwezi kupoteza muda kumdai Fei Toto pesa.

Yanga ilichokuwa inasubiria (au itakachokuwa inasubiria kama atagoma kurudi) ni kuona Fei Toto ataibukia timu gani ya mpira wa kulipwa. Hiyo timu ndo Yanga itaidai.

Kwenye kesi za madai busara ni kumfungulia kesi mtu mwenye hela. Kumdai maskini ni kupoteza muda. Unaweza ukashinda kesi lakini maskini hana hela ya kukulipa kwa hiyo ushindi wako unakuwa hauna maana.

Hata hivyo, kwa weledi ilioonesha TFF katika kushughulikia suala hili ina maana Fei Toto hataweza kusajiliwa na timu yoyote ya mpira wa kulipwa. Maana ili asajiliwe nchini Tanzania ni lazima asajiliwe kwenye mfumo wa TFF. Kwa kuwa TFF imeshasema ni mchezaji halali wa Yanga, ni dhahiri kuwa haitaweza kumbadilishia usajili na kukiuka hukumu iliyotoa.

Na ili akacheze nje ya nchi kwenye soka la kulipwa ni lazima apate kibali cha TFF ili kulinda maslahi ya taifa (kwamba aweze kuitwa kwenye timu ya taifa akihitajika) na maslahi ya kilabu anayotokea hapa nchini. Hapo tena ni dhahiri kuwa atakwamba. TFF haiwezi kumpa hicho kibali wakati imeshasema ni mchezaji wa Yanga. Ni lazima timu ya nje ya mpira wa kulipwa itakayomtaka imalizane kwanza na Yanga.

Kwa hiyo utaona kwamba mazingira ya yeye kuendelea kucheza mpira wa kulipwa bila ya timu anayotaka kuchezea kumalizana na Yanga hayapo. Ndo maana nasema aidha atafute shughuli nyingine ya kufanya au akacheze mpira wa ridhaa. Huko Yanga itamlima barua tu lakini haitahangaika kwenye kesi.

Shida ya yote haya ni kwamba kama kuna timu iliyokuwa inamtaka, hiyo timu ilimtaka kwa njia za panya. Badala ya timu hiyo kumalizana na Yanga, yenyewe ikaamua kutumia njia za uchochoroni ili impate kwa bei nafuu.

Kitu ambacho kinapaswa kulaaniwa na wapenda mpira wote. Hii sio ishu ya uSimba na uYanga. Ni ishu ya ustaarabu wa mpira kuhakikisha kwamba timu zinavuna matunda ya uwekezaji kwa wachezaji.
Mkuu una akili sana
 
Back
Top Bottom