Wakili wa Mwabukusi amuangukia Rais Samia, aingilie kati, watuhumiwa kucheleweshwa Mahakamani

Wakili wa Mwabukusi amuangukia Rais Samia, aingilie kati, watuhumiwa kucheleweshwa Mahakamani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Wakili wa Wakili Boniface Mwabukusi na Mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mpaluka Nyagali maarufu kwa jina la Mdude Nyagali wanao shikiliwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za Uhaini, amemuomba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala la watuhumiwa hao Ili waweze kupelekwa mahakamani na haki iweze kutendeka.

Akizungumza na waandishi wa habari Wakili Philip Mwakilima amesema bado kumekua na vikwazo kwa watuhumiwa Balozi Dkt Wilbroad Slaa, Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali, kufikishwa mahakamani licha ya kukaa zaidi ya siku tano mahabusu tangu walipokamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Pamaoja na hayo Wakili Mwakilima amemuomba Rais Dkt Samia kuingilia kati kwa kutoa amri ya watu hao kufikishwa katika vyombo vya utoaji haki Ili waweze kutoa hakiyao ikiwemo ya matibabu kutokana na wateja wao kua na maradhi mbalimbali.
 
Wakili Mwakilima anayewatetea Dr Slaa,. Mwabukusi na Mdude amesema ni Rais Samia Pekee anayeweza kutatua sintofahamu iliyopo kwa kuwa Polisi wanatikia mamlaka na kupokea maagizo

Mwakilima amesema katika Swala hili kuwalaumu Polisi au Mwendesha mashtaka ni kuwaonea

Naye Kamanda Msaidizi afande Mkwawa amesema kuna turatibu zinaendelea na zikikamilishwa itatolewa Taarifa rasmi

Source: Mwananchi
 
Back
Top Bottom