Wakili wa Mwabukusi amuangukia Rais Samia, aingilie kati, watuhumiwa kucheleweshwa Mahakamani

Wakili wa Mwabukusi amuangukia Rais Samia, aingilie kati, watuhumiwa kucheleweshwa Mahakamani

Ushauri mzuri tukiachie chombo cha kutoa Haki
 
Mama akilisamehe lile dokta uchwara sisi tutaandamana hadi ikulu kuomba lirudishwe tena ndani.

Lile ndo limewashawishi na kuwalaghai wenzake kwamba wakifanya mapinduzi na kuwa raisi litamteuwa mwabukusi kuwa jaji mkuu wa Tanzania na mdude atapewa cheo cha kusimamia askari magereza ili alipe kisasi kwa waliompa kipondo jela enzi za Magufuli.
Huwezi kumsaliti Mwamba Mbowe na Karma ikakuacha salama Babu anyongwe tu hakuna namna

Hebu sikiliza hapo cheka yake ya kinafiki alipomalizia kupigilia huo msumari dhidi ya Mwamba

DR SLAA NI MHAINI MPAKA MAHAKAMA ITAKAPOAMUA OTHERWISE
 
Siamini hata wewe umekua mtu wa hovyo? Ama kweli. Utakua ndugu ktk imani si bure.

Hapana mkuu nawasapoti huko twita space 🤣

WhatsApp Image 2023-08-17 at 9.20.12 AM.jpeg
 
Hivi wakati wanamnyaka Dakta Slaa walimruhusu achukue dawa zake za Presha na za Kisukari?

Asije huyu Mzee akapigwa na Stroke huko Mahabusu
 

Wakili wa Wakili Boniface Mwabukusi na Mwanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mpaluka Nyagali maarufu kwa jina la Mdude Nyagali wanao shikiliwa na jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za Uhaini, amemuomba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuingilia kati suala la watuhumiwa hao Ili waweze kupelekwa mahakamani na haki iweze kutendeka.

Akizungumza na waandishi wa habari Wakili Philip Mwakilima amesema bado kumekua na vikwazo kwa watuhumiwa Balozi Dkt Wilbroad Slaa, Wakili Boniface Mwabukusi na Mdude Nyagali, kufikishwa mahakamani licha ya kukaa zaidi ya siku tano mahabusu tangu walipokamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Pamaoja na hayo Wakili Mwakilima amemuomba Rais Dkt Samia kuingilia kati kwa kutoa amri ya watu hao kufikishwa katika vyombo vya utoaji haki Ili waweze kutoa hakiyao ikiwemo ya matibabu kutokana na wateja wao kua na maradhi mbalimbali.
Nani kaomba Mwakilima au Mwabukusu
 
Watake kumpindua Rais afu wanamuomba rais huyo huyo kuingilia kati? Wonders shall never seize. Wanajikaanga kwa mafuta yao.
Ni kwa sababu rais Dkt Samia siyo tabia yake kubambika watu kesi, yaani hapo kuna watu anawavutia kasi ataruka nao very soon.
 
Hilo ndio tatizo lenu kuu basi tumweke kibatala akaamue au una maoni gani?
Tunafahamu mfumo wetu wa haki ulivyo, na nini huwa kinaendelea nyuma ya pazia. Ukiona mtu ana imani na mfumo wetu wa kutoa haki, huyo ujue ni mfaidika wa huo mfumo, au hajui lolote. Ndio maana wawekezaji hawako tayari mashauri yao kupeleka kwenye hizi mahakama zetu.
 
order from above! Ila kale ka kibatali kanakozungushwa vyumba vyote vya boma yetu , ndo kakulaumiwa sana, maana kanatufanya tuwe tumezubaa zubaaa na kutokujielewa. zaidi tunabaki kupiga keyboard mitandaoni tu Basi.
 
Back
Top Bottom