Basima Ogenze
JF-Expert Member
- Aug 14, 2015
- 786
- 881
Tatizo kuna wengine uko nae lakini bado analiwa na baba Wa wale watoto.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ila single mother aisee wana changamoto sana. Mimi nilipotezewa kwa muda mrefu alikuwa hana hata habari na mimi. Nikaona its OK kwa sababu maisha ni yake na maamuzi ni yake. Baada ya miaka kupita nikakutana naye tena. Nipo cool tu na kila mtu na wala sina chuki, akaniletea tena mazoea na hatimaye akanitongoza na kuniambia ananipenda kwa dhati.
Kidume nikaona huyu binti aje mbona imekuwa kwa ghafla hivyo. Baadae kuja kugundua kumbe tayari ameshazalishwa na mshikaji ambaye alimfanya hawezi kunifikiria mimi. Nikajifikiria nikasema huyu binti ananifanya Mimi ni mjinga(?)
Akatoa samahani nyingi na machozi ya hapa na pale na ahadi lukuki kwamba atakuwa muaminifu kwangu. Nikaona siyo mbaya nitabeba majukumu. Kwa ghafla jamaa aliyemzalisha akasema anataka arudi wayamalize kwa wazazi, naye anataka kumlea na kumuona mtoto wake. Drama zikaendelea mwisho wa siku nami nikawa miongoni mwa hiyo drama yao. Baadaye hizo issue na jamaa yake mara Maza wa jamaa aliyemzalisha anapiga simu kuhusu mjukuu wake. Nikaona daaaamn! Jamaa mara anamsumbua binti anampigia pigia simu anatumia kigezo mtoto wake. Mara mama wa huyo mshikaji anataka kumuona mjukuu.
Nikamwambia mama lengo langu na ahadi zangu zilikuwa na nia njema lakini hii hali kadri inavyozidi kwenda inaniumiza sana. Hii drama nayo inaonekana ni endelevu na moyo wangu sidhani kama utakuwa na uwezo wa kuvumulia hiyo mikiki. Nikamwambia tuachane. Alining'ang'ania sana, binafsi nikamwambia siwezi.
Tangu niachane naye mpaka sasa hivi yapata ni miezi 7. Nilimpenda lakini hiyo mikiki yake kiukweli hapana. Ila yeye mpaka sasa hivi ananipigia simu na kunitumia msg. Sijibu chochote katika hivyo na wala sijam' block.
Ma single fathers huwa hawapo? Au mimba hizo za ma single mothers huwa wanazipata kwa uwezo wa roho mtakavitu?
Kweli halafu hawa wavulana ni waoga wa maisha wanachokimbia sio single mother wanakimbia majukumu ni wakina uchebe hawa ila mi naona mwanamke ni mwanamke akikupenda mkapendana weka ndani watoto leaMwanamke yeyote single mother hawezi kuolewa na mwanaume asiyejitambua au kuolewa na mvulana
Wewe huna mtoto why upo Interested Na mwenye mtoto?kuna Agenda gani ya siri.(japo hakuna ubaya ila kwa jinsi ulivyoisisitizia kwenye heading yake.Nna umri wa miaka 36. Natafuta single mother aliye na mtoto mmoja tu. Sababu ya kuwa single iwe ni baba mtoto wake kufariki ama alizalishwa bahati mbaya na mme wa mtu. Sifa zake
1.Age 20-28yrs.
2. Maji ya kunde ama mweupe.
3.Awe na elimu at least ya form four.
4.Awe na mawazo ya kufanya biashara.
5.Awe tayari kuishi Mwanza
6.Kabila lolote
7.Dini yeyote ila mimi ni mkisto na sipo tayari kubadili dini yangu
8.Asiwe mnene wala mwembamba sana. Awe na shape kiasi kwamba nkiwa nae nsiogope kumtambulisha kwa friend na ndugu.
9. Asiwe mtu wa kuendekeza starehe kupita kipato.
Mimi nafanya kazi inayonipatia kipato cha kulisha familia, naweza kusomesha n. k.
Sijaoa na wala sijabahatika kuwa na mtoto.
Swala la kupima HIV kwangu ni la msingi endapo atatokea ambaye tume match.