Wewe nae kidogo umenichanganya, au mimi ndo sijaelewa, unasema kaka ako alioa miaka 5 iliyopita, alafu hapo hapo tena unasema hawajaoana, which is which? Back to the main point, Huyo kaka ako ana matatizo gani? kakamilika kiume? i mean kiuchumi na kimaungo, yuko sawa? dunia ya leo hii watu wanatafuta wanaume wa kuwaoa mpaka wanakesha makanisani wakifunga na kuomba na wengine wanabadilisha waganga kila siku wapate ndoa, cha ajabu yeye ameng'ang'ania kwa mwanamke wa hivyo? Mzazi mwenzie kwenda kumuona mtoto mpaka ana lala hapo hapo? ya wapi hiyo? eti ameshindwa kwenda kwa huyo dada kisa mzazi mwenzie yupo? hiyo inaingilia akilini kweli kwa mwanaume aliekamili? hata hao majirani siwana shangaa nani mume hapo kati yao wawili, na hali ilivyo kaka ako ndo anaonekana mwizi, hebu tueleze vzr, au kaka ako mariooo alafu huyo dada ndo mwenye mkwanja mrefu anamtunza jamaa ndo mana amegeuzwa bushoke. Kama utaniambia kaka ako yuko kamili, kiuchumi, kiakili na kimaumbile, basi ntaamini UCHAWI UPO, mana sio kwa kufanywa zezeta kiasi hicho