Habari zenu.
Nasema hivi. Mwanaume yeyote rijali hawezi kuoa mwanamke single mother. Ninaposema single mother namaanisha wewe mwanamke uliyezaa kabla ya kuolewa.
Na ninaposema rijali namaanisha mwanaume mwenye akili sawa sawa au bara bara anayefikiri kwa usahihi asiyeendeshwa na mihemko bali hutumia akili yake kutafakari mambo. Hii ina maana mwanaume chizi au mwenye ugonjwa wa akili sio rijali. Ili uwe rijali ni lazima uwe na akili timilifu. Ushahidi ni kwamba mwanaume hanithi anapungukiwa pia akili. (Sitaki kulizungumzia hili) na ukishapungukiwa akili wewe sio rijali.
Ukweli ni kwamba mama zetu ( sisi wanaume) wanafurahi zaidi kama utampa taarifa kuwa unamuowa bint ambaye hajawahi kuzaa. Achilia mbali bikra ambayo hata hivyo wanatamani uwaambie unamuowa bikra. Ni heri uwaambie unamuowa bint uliyezaa naye wewe mwenyewe mtoto wake wa kwanza kuliko kuwaambia wamama eti....eti...unamuowa Lilian single mother!!! Nyoyo husononeka ingawa hawawezi kusema wazi wazi. Utasikia tu mama akisema "Kama umempenda na mnapendana sawa" Tafakari sana haya maneno kijana unayetaka kumuowa single mother.
Ni uzembe wa hali juu sana kuzaa kabla ya ndoa. Ni mwanamke ndiye unayeamua ushike mimba au usishike. Sisi wanaume huwa tunatandika tu.....sasa kama you don't take care about yourself....who else will? Halafu unamlaumu mwanaume kakutia mimba na hajakuowa.
Asikulaghai kwa maneno matamu yoyote yale eti beba mimba kabla hajakuowa. Usikubali. Na mwisho wa siku uamuzi unao wewe wa kubeba mimba au lah. Sasa mnakwama wapi? Be smart.
"Asiponioa ntalea mwenyewe!" Huo ni uzembe.....tunajua mna vipato vyenu....mna pesa zenu, mnayamudu maisha....mnaweza kulea watoto wenu. Nikuulize, hivi kuna raha gani kulea mtoto peke yako? Mnapojitosheleza kiuchumi na kijamii (kutokuwa single mother), machaguo yanaongezeka. Hamuoni? Basi someni. Baadaye mnasema kuolewa bahati. Kuolewa sio bahati. Kuolewa mna haki wala msiite bahati....we unadhani wanangu mi ntalea na nani? R.I.P Ngwea
Jamaa akuzalishe huko halafu mi nije nikuoe? Acheni masihara nyie. Mi hakuna niliyemzalisha bila ndoa nikampiga chini sina sababu ya kuowa single mother.
Na wewe single mother uliyekaa chini ukaona ulikosea wapi na sasa umekuwa RAIA mwema, good luck. Ukimpata anayeeleweka mwambie akuoe. Kijana haukatazwi kuoa single mother. Ukimpata oa......yajayo ni yako.
Hakuna mwanaume RIJALI anayeweza kuowa single mother, kwa sababu za kimaadili. Period.
Meraki