Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Wakinamama wanaolea watoto bila baba (single mothers): Sababu, athari kwa mtoto, changamoto na mitazamo ya jamii

Kiukweli hata wengi ya waliolelewa na baba na mama ni kama wamelelewa na single mothers tu maana wengi baba inaweza mlikua mnawaona tu nyumbani lakini uhusikaji wao kwenye malezi ilikua zero labda ashiriki kwenye kukupiga na kutoa pesa. Wanawake wengi wa zamani (mama zetu) ukiwauliza atakujibu alibaki na baba yako sababu alikua na watoto na sio upendo.
 
Zaman nilkuwa nawahurumia sana singo maza lakin kuna kijiji npo kwasasa nmegundua asilimia kubwa ya wadada wanaona poa kuwa singo mum maana vibinti vingi vmezaa hovyo hovyo tu hata 18 yrs bado,NAWASHAURI WANAUME WENZANGU singo mama sio wa kuoa kabisa hasa wale ambao wamekuwa singo mum kwenye usichana wao
 
sun wu,
Mtoto aliyelelewa na mama peke yake ana ubora wa hali ya juu sana ukilinganisha na yule aliyelelewa na Baba na Mama walio katika mazingira ya "Polgamy", (kwa kiswahili hili neno silifahamu), yaani mme mmoja mwenye wake wawili, halafu ikatokea kwa bahati mbaya kuwa mama mmoja alikuwa hapendwi kuliko yule mwingine.

Mama ambaye huwa anakuwa kwenye disadvantage side ya kutokupendwa zaidi na mume, watoto wake huwa wanakuwa the worst, wakati mwingine unaweza kusema bora hata mtoto wa mtaani aliyekulia kwenye mitaro.

Huwa wako psychologically destroyed kwa kiwango cha ajabu muno, na wanakuwaga the most inferior hata kama waliishi katika maisha ya utajiri wa pesa nyingi.

Na mbaya zaidi ni kwamba iwe waliishi katika mazingira ya pesa au hapana, wanakuwaga na tabia ya kutafuta pesa kwa njia yoyote ile. Jaribuni kufanya utafiti katika hili halafu mtanipa mrejesho
 
Zile nyuzi zimeanza tena!mods wekeni jukwaa basi,ila kiuhalisia kuna mafunzo mazuri sana kwenye hizi nyuzi,hata kama zinamgusa mtu au zinakuumiza penda kusoma,kuna kitu cha kusaidia na kufundisha...
hili ni kaburi wamefukua mkuu, uzi wa 2013 huu
 
Unaamini sisi wazalishaji hovyo watoto na kutokuwahudumia kwa chochote huwa wote tunafikiria mtoto akitoboa kimaisha tutamfata kwa namna moja ama nyingine?
Na hilo ndo linaninyima kumpokea mtoto wa mwingine ati mimi ndo babake. Thubutu yako. Nani asojua kuwa kesho tu akifanikiwa weye babake ndo unakuja kujikomba kuwa ni mamake tu alifanya haraka kukimbilia kwa limtu flan. Leo, mwanangu nimekupata sikuachii
 
Na hilo ndo linaninyima kumpokea mtoto wa mwingine ati mimi ndo babake. Thubutu yako. Nani asojua kuwa kesho tu akifanikiwa weye babake ndo unakuja kujikomba kuwa ni mamake tu alifanya haraka kukimbilia kwa limtu flan. Leo, mwanangu nimekupata sikuachii
Bahahaha! Ngoja nikuthibitishie jambo wazazi hao sasa hivi hawapo tena na mimi ni mmoja wao tumeshapotea hata awe na kiwanda kama cha Lamborghini ni chake i better die poorly.

Mzazi anayefanya jambo ili aje kumtegemea mtoto wake baadae huyo ni loser mkubwa. (Akili za kimasikini)
 
Nina mwanamke ambae tuna mtoto, ila hatukuweza kuoana kutokana matatizo yaliyojitokeza wakati huo. Baadae alioolewa na sasa ni zaidi ya miaka mitano tangu aolewe, mtoto alimwaacha nyumbani kwao, nilimuomba baada ya kuolewa tukatishe mawasiliano kwa afya ya mahusiano yetu, tukawa hatusiwasiliani tena, mawasiliano pekee yakabaki kwa mamaake mzazi na mdogo wake wa kike.

Baadae nilimchukua mtoto nikampeleka Kenya [emoji1139] kusoma, ikawa wakati wa likizo nampeleka kwa bibi yake maana ndiko alikokuzoea, sasa hivi karibuni nilimfuata mtoto nimpeleke shule, nikamkuta huyu mzazi mwenzangu yupo kwao, akaniambia kuwa alikuwa ananisubiria mimi ana mambo muhimu ya kuniambia. Akasema mazungumzo hayo yatafanyika mjini na vile vile alitaka kumfanyia mtoto wake shopping, tukaondoka mpaka mjini, lakini cha ajabu alitupeleka kwenye nyumba ambayo amejenga akasema amemjengea akanipa na documents zote, baadae akanionesha dukani ambalo amefungua na faida ataiweka kwenye akaunti ya mtoto.

Baadae tukaenda kupata chakula ili tuendelee na safari ya shule, tukiwa kwenye chakula nilimuuliza amewezaje kujenga na kufungua duka kubwa vile, akaniambia anamuibia mme wake, kwamba yeye ndie msimamizi wa biashara za mme wake na pesa zote anachukua, alinionesha akaunti yake imenona.

Mbaya zaidi kilichonifanya niandike hapa aliniomba usiku huo tuwe pamoja na kesho yake ndio tuendelee na safari, baada ya ombi hilo, nikamfikria jamaangu (simfahamu) jinsi anavyoibiwa na huyu mwanamke halafu na mimi nimuibie? Nikaona nikikataa moja kwa moja angejisikia vibaya, nikamdanganya nimeisha kanyaga miwaya, akaishia kunishukru na kunipongeza kwa kumuokoa.
huna to
Baada ya hapo nimefikria sana kuhusu hawa single mothers, hivi wanakwama wapi? Wanakumbuka nini kwa wanaume waliowazalisha?
KESI 1

Mkuu Molembe.

habari yako! Jawabu hili limenifanya nitoe fikra zangu kidogo kwanini hiko kitu kimekutokea ...Nadhani nimepata bahati ya kusikia hili jawabu lako ambalo linafanana kabisa na jambo lililomtokea rafiki wangu wa karibu sana.

Naye ilikuwa hivi:- Alipata kuwa na mahusiano na mwanamke fulani..Hata wakapata mtoto mmoja wa kike. (pasi na kuwa wameoana tayari). sasa jamaa akapata hudhuru akaenda zake Dar mara moja. Baada ya kurudi akakuta mshike mshike hata ukapelekea kuachana.

Jamaa akapata Mwanamke mwingine akaoa akaweka ndani. na sasa ana mtoto mwingine na huyo mwanamke aliyemuoa. Kumbuka na yule mwanamke amepata kuolewa na Mwanajeshi.. Basi kila mtu akawa anaendelea na maisha yake huku wakiwasiliana kwenye masuala yanayohusu mtoto tu.

mwezi december mwaka jana jamaa akiwa katika mizunmguko yake hapa mjini (sio Dar) akakutana na hoyo mwanamke wake wa kwanza. Ikabidi wakae pembeni kidogo huku wakipata kinywaji. kilichotokea Mwanamke akamwambia mshikaji kuwa amemmisi na wakakumbushie enzi zao.

Mshkaji baada ya kuambiwa hivyo akaona anatakwa kuingizwa mkenge, yaani atembee na mke wa Mjeshi na isitoshe Jamaa (Mjeshi ndio anayesomesha hata mtoto wake) akaona isiwe tabu, akamwambia jioni hiyo wakutane pahala fulani. Lakini jamaa yangu akutokea mazima maeneo hayo. na hata akionana na mwanamke huyo njiani huwa anakimbia na kujificha.


KESI .

Binafsi niliwahi kuwa na mahusiano na mshichana fulani kutoka high school 2011. Bila shaka tulikuwa tunapendana sana. Ila mazingira yalitutenganisha bila kupenda. Ikabidi mimi niendelee na kitabu kwingine na yeye aendelee na mengine.

Baada miaka 5 baadaye nikapata taarifa kuwa ameolewa na ana watoto 2.

Kwa bahati mbaya au nzuri nilipata safari kuelekea mkoa ambako nimesoma high school. nikakutana na mmoja wa rafiki zake na akanipa namba yake.

Nikaona sio tabu ngoja nimtafute nimsalimie.

Kumpigia tukangea sana. hata tukaona tuonane ili tupige stori zaidi za maisha. (ofcourse kila mtu alikuwa na hamu ya kumuona mwenzake). Tukapata kinywaji sehemu flani huku stori zikiendelea. But cha kushangaza usiku alikuja pahala ambapo nime rent pakulala. Tukalala usiku mzima pale.

Ikawa ndio tabia sasa. kila nikienda mkoa hule lazima tuspend night usiku pamoja.

Kuna nyakati nikaona sio poa ngoja niache hizi habari za kutoka naye. Mpaka sasa nimekata mawasiliano naye. Nimemuongopea niko Zambia kikazi.

HITIMISHO:

Mimi nadhaani hawa watoto wakike huwa kuna watu wao ambao wako ndani ya mioyo yao! Hata ukioa na kumuweka ndani na kuzaa nae. Yupo Jamaa somewhere mwenye uwezekano mkubwa wa kutembea na mkeo muda na wakati wowote ule aupendao.

"wengi wana watu wao, wengine toka zamani." - MWANA FA
 
Kwahyo huyo mwanaume ambaye ana akili akiamua kumuoa huyo single maza anakua hajafanya maamuzi sahihi sabahu ww tu unaona sio sahihi?
Kwani unamlisha?
Unamsaidia kutafuta pesa?
Unajua furaha yake in life?r u part of t?
Kwann tunapangiana maisha aisee
Kama yeye anaona huyo single maza anamfaa why ww ambaye huna hta msaada na maisha yake umuone hana kili?
Unadhan hajawaona hao wasio na watoto?
Listen guys kila mtu anajua nn anataka kwenye maisha yake to be specific standards gani anahtaj kwenye maisha yake
Sasa wht if hizo standards huyu single mza anafit ila hao ambao hawana watoto hawazifikii?asioe sababu ww tu unayejiona una akili unaona sio sahihi?
Tuache madharau kuna sisi wengine baba zetu walioa single mothers ni kwamba hawakua na akili??sikujui hunijui ila m.se.nge ww hao single mother ni nani anawap mimba kama sio sisi wenyewe?
Gerari hiaaa
Wakuu Habarini za Leo,

Nimegundua mwanamme mwenye akili hawezi kuoa single mom

Kwanza kabisa mwanamme mwenye akili ni yupi? Ni mwanamme mwenye uwezo wa kufanya maamuzi chanya kwa kutumia akili yake vizuri bila kujali hisia zinasemaje.

Kwa hivyo mwanamme mwenye akili anao uwezo wa kuchakata mambo kwa kutumia ubongo.

Nimemalza Uzi wangu.

Swali kwa dada zangu,
Kaka yako au mwanao akikupa Habari kuwa anaoa single mom utajisikiaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zaman nilkuwa nawahurumia sana singo maza lakin kuna kijiji npo kwasasa nmegundua asilimia kubwa ya wadada wanaona poa kuwa singo mum maana vibinti vingi vmezaa hovyo hovyo tu hata 18 yrs bado,NAWASHAURI WANAUME WENZANGU singo mama sio wa kuoa kabisa hasa wale ambao wamekuwa singo mum kwenye usichana wao
kijiji gani hicho?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1) You cannot be her top priority simply because you are dating. You aren't her
Binafsi nimekuzwa na kulelewa na mzazi mmoja ambaye ni mama, sijawahi pata hata mapenzi ya baba nilipokuwa mwana.

Kulea mtoto binafsi bila msaada wowote ilikua ngumu sana kwa mzazi wangu lakini alijifunga shuka kiunoni na kutosalimu amri ya uvivu.

Kwakweli malezi ya mzazi mmoja pekee yana changamoto nyingi sana kwani kila jukumu la mtoto linasimamiwa na mzazi huyo huyo tu haswa haswa wakati ambapo mzazi huyo hana uwezo wa kumlea mwana huyo.

View attachment 1340537
Mara nyingi huenda mzazi huyo akakumbwa na huzuni ambayo inaeza mwathiri mtoto wake kisaikologia. watoto huwa na tabia ya kufanya na kutii wanachokiona. Basi tabia ya mzazi inaeza mdhuru mwanawe.

Kwa sana mzazi yule anaenda kutoa hasira zake kwa mtoto, wakati mtoto huyo hana hatia. Hii huleta huzuni nyingi kwa mwana na kumpa mafikira ya kuwa hapendwi, ama hua anahisi kama yatima.

Wewe kama mzazi unayelea mwana wako ukiwa peke yako, mbali na sababu zake huna ruhusu kumfokea mwanao bila sababu au kumchapa ovyo ovyo. Na wakati huyo mtoto amefika umri wa kubalighi basi unaweza mweleza sababu zilizofanya akuwe mtoto wa kulelewa na mzazi mmoja tu.

Zaidi ya watoto milioni 320 ni watoto wa mzazi moja, hii inaonyesha kuwa wazazi wengi wanalea watoto wao peke yao, huenda ikawa ni sababu ya talaka ama kifo cha mzazi mmoja ama ni mwanaharamu(mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa).

Wala haimaanishi kuwa mtoto aliyekuzwa na mzazi mmoja hatapata malezi bora, La hasha, mtoto anaweza kukuzwa na malishe bora pia na maadili hata kushinda mwenye wazazi wake wawili. Jambo la kusikitisha ni kwamba, watoto wengi wa mzazi mmoja wanakuwa wakubwa bila kupata mapenzi ya baba… hii huenda pia ikafanya mtoto yule, iwapo ni wa kike awe mwenye mapenzi na wanaume wenye umri kumshinda kwa sana.

Sababu zinazopelekea mtoto kulelewa bila baba

1. Kufariki kwa baba
Hii hutokea pale ambapo mzazi wa kiume wa mtoto/watoto akafariki na mzazi aliyebaki kutofunga ndoa/ kuingia kwenye mahusiano tena au akaingia kwenye ndoa na mtu asiyekubali kubeba jukumu la kuwa baba kwa watoto hao.

2. Kutelekezwa
Hii hutokea mzazi wa kiume wa mtoto anapotelekeza familia na kuacha jukumu lote kwa mama.

3. Baba kukataa ujauzito
Mwanaume anaweza kukataa ujauzito kwa sababu mbalimbali kama kutokuwa tayari na malezi, kuwa na mahusiano mengine, kuhisi amesingiziwa ujauzito huo au kutotaka kuwa na mtoto na mwanamke husika.

4. Baba kufungwa
Uamuzi wa Mahakama unaweza kusababisha mzazi wa kike kubaki na jukumu la kulea watoto au mtoto peke yake.

5. Mama kubakwa
Vitendo vya ubakaji hususani kwa mabinti wadogo husababisha watoto kulelewa na mama pekee aidha kwa sababu ya kutomjua mhusika au kuogopa kumtaja au baada ya baba kuhukumiwa kwa kosa la ubakaji

6. Maamuzi binafsi
Siku za karibuni kumekuwa na wimbi la wadada kutaka kulea watoto bila msaada wa wanaume kwa sababu ya nguvu ya kiuchumi hivyo kupelekea kufanya maamuzi ya kubeba ujauzito na kukataa kuendelea na mahusiano na mhusika au kumficha au kuamua kubeba ujauzito wa mume wa mtu akijua fika kuwa atakataa kuhusika na malezi.

Faida za mtoto kulelewa na baba na mama

Watoto huhitaji malezi ya pande zote mbili bila kujali wazazi wao wako pamoja au la. Wanaume wengi wamekuwa wakisahau hili na kuhisi mama ndie mwenye jukumu pekee la kulea watoto. Mara kadhaa hurudi usiku na kukuta watoto wamelala na hutoka asubuhi sana kabla hawajaamka pengine bila hata kujua wameamka vipi. Zifuatazo ni sababu kadhaa kwa nini watoto wanahitaji malezi ya baba:

Utashangaa lakini sehemu ya kwanza ya mtoto kujua mwanaume ni mtu gani, anaonekana vipi na tabia zake ni kupitia baba. Unavyoishi na familia yako ndio hivyo mtoto atajua wanaume wote wako hivyo!

Akina baba hucheza kwa namna tofauti kidogo na watu wengine

Mara kadhaa utasikia mama akigombana na baba pengine tu baba anatumia nguvu nyingi akiwa anacheza na mtoto akihisi atamuumiza! Akina baba hucheza kwa nguvu zaidi na hucheza na mtoto kwa muda mrefu zaidi hii humfanya mtoto ajihisi salama na mwenye furaha.

Utafiti unaonyesha kuwa watoto wanaolelewa na baba huwa na tabia bora zaidi kuliko watoto wanaolelewa na mama pekee

Hakuna kitu mtoto huhitaji akiwa mdogo kama rafiki wa karibu. Watoto wadogo hasa wa kike hupenda sana kuwa karibu na baba yao, kwan huhisi salama zaidi akiwa na baba nan i mtu atakayemtetea kwa mama.

Uwepo wa baba katika maisha ya mtoto humfanya ajenge hali ya kujiamini kwani huhisi siku zote kuna mtu nyuma yake kwa ajili ya kumtetea.

Kujua namna ya kuwa baba bora/namna ya kuishi na mume

Zile tabia njema anazoziona kwa baba na mama ndio hivyo hivyo atafanya kwa mpenzi wake. Wazazi husahau kuwa Watoto hujiskia vizuri sana wanapoona hali ya mawasiliano mazuri kati ya wazazi wao hata wanapokua wametengana.


Mtoto anaelelewa na mama tu huwa na njia moja tu! Nayo ni ya mama, ni vema mtoto kupata upendo wa wazazi wote wawili ili ajue ni njia ipi sahihi kwake.

Kukaa na baba nyumbani humsaidia mtoto namna ya kuheshimu mamlaka mbalimbali za mahali husika. Mfano atajifunza kuwahi kurui nyumbani, kuvaa vizuri nk.

Wanaume wana uzoefu mwingi zaidi na maisha ya kawaida hasa kuishi na watu uvumilivu nk. Ni kawaida kumkanyaga bahati mbaya mwanaume, ukamuomba msamaha na akakuelewa, lakini kwa wanawake wengi hadithi huwa tofauti. Hapa utaona ni jinsi gani busara hii anavyoihitaji mtoto kuoka kwa baba.

Kufanya kazi kwa nguvu na bidii

Wanaume pia ni watu wanaofanya kazi kwa bidii sana hii humfundisha mtoto kutokata tamaa .


Madhara ayapatayo mtoto anayelelewa na mzazi mmoja

1. Chuki na kupunguza upendo kwa mzazi mmoja

Wazazi wanapoachana daima watoto hugawanyika, huenda wakaishi kwa baba au kwa mama, au mmoja akaishi kwa baba mwingine kwa mama, hii hupelekea chuki upande mwingine, wazazi wengi hupenda kushirikisha ugomvi wao na watoto hupenda kuzungumza kwa hasira na huenda mpaka kusema sababu ya kuachana kwao.
(mara nyingi sababu ya watu kuachana si nzuri na ni aibu kuiweka wazi hasa kwa watoto)

Baba huweza kumwambia mtoto mama yako mpuuzi sana, mama yako hana akili, mama yako malaya tabu unazopata hapa kwasababu ya umalaya wake au mama humwambia mtoto hasa anapokosea, yani unaakili kama za baba yako, usiwe chizi kama baba yako, usiwe mjinga kama baba yako.

Katika hali ya kawaida haya ni maneno machache lakini yenye ujumbe mzito na usio na busara mbele ya watoto , watoto huanza kujenga chuki kwa mzazi mmoja maana anayesema hayo ndio mzazi anayemuhudumia kwa kila kitu, mtoto lazima ataamini na kumfuata baba/mama kwa kauli zake hivi inapendeza mtoto kumuona baba/mama yake hana akili au malaya? si kauli au malezi ya kiuungwana kesho mtoto atakutusi wewe utaridhia?

2. Mawazo / Mgogoro wa nafsi

Umri wa mtoto ni tofauti na mkubwa, hakuna mtoto anayependa kuona wazazi wake wanakosana, kupigana mpaka kufikia hatua ya kuachana, hatua ambayo humuumiza zaidi mtoto kuliko wazazi, wazazi wanaamini kwamba kwakuwa wanapesa au wanauwezo wa kumuhudumi/kuhudumia mahitaji yote kwa mtoto basi anaweza kulea, (Wazazi wengi bado hawajui maana ya malezi na haki za mtoto).

Mgogoro wa nafsi unaweza ukawa wa nje au wa ndani, yani kama mzazi unaweza kumuona mwanao hana raha na akakuleza kinachomsibu au asikueleze( unaweza kumsaidia au usiweze) lakini watoto wengi huwezi kuwakuta wanakaa chini kuwaza ila yale mawazo yanawatafuna wakiwa wamelala, wanakuwa wanafikiria sana na kuumia nafsi, mtoto anaweza kula vizuri, kulala sehemu nzuri na unahakikisha unampa kila anachohitaji lakini humuoni akiwa na afya nje au kunenepa vizuri.

Hofu, mashaka na woga ndio unakuwa sehemu ya maisha yake, anaweza kuwa mjinga na asiwe mwenye kuhoji sana, hasa utakapozidi kutaka kuilazimisha furaha yake au kila atakapomuulizia baba/mama yake nawe kumpa majibu yasio faa, Akili yake inadumaa.

3. Mabadiliko ya kitabia

Tabia ya mtoto hujengwa na pande tatu, baba, mama na jamii inayowazunguka lakini tabia kuu ambayo mtoto ndio sura yake inatoka kwa baba na mama, wazazi wanapoachana na tabia za watoto pia hubadilika huenda zikawa nzuri au mbaya, lakini kwa asilimia kubwa tabia za watoto hao huegemea zaidi upande mmoja, upande ambao anapokea malezi, kwa mama au kwa baba.

Kama ni mtoto wakiume na anaishi na mama, kuna baadhi ya tabia za baba hasa za kiume anazikosa, kama vile ujasiri, uvumilivu njia za kutafuta pesa na hata baadhi ya mambo ya mahusiano na mabadiliko ya mwili, mama hawezi kuwa huru kumueleza mtoto wa kiume mambo ya kiume, na hata mtoto wa kiume akipatwa na ugonjwa wa siri hawezi kumueleza mama na hata kama atamueleza basi ni dhahiri amefikiria sana na amekosa msaada na ugonjwa tayari utakuwa umemtafuna

Vile vile kwa mtoto wa kike akiishi na baba ni hivyo hivyo, lakini pia huenda mtoto wa kiume akawa na tabia za kike kulingana na kuishi na mama yake muda mrefu, na mtoto wa kike akawa na tabia za kiume kulingana na kuishi na baba yake muda mrefu.

Kikubwa ni kushindwa na kudhitibi mihemko yao, kama mtoto wa kiume anaishi na mama yake, mara nyingi anajikuta huru kutoka na kufanya mambo mengine bila kujua anachokienda ni sahihi au si sahihi na kwa wakati husika au sio, na kwa mtoto wa kike ni rahisi kuwa huru maana baba ndio mtafutaji, muda mwingi anashinda kwenye mihangaiko au kazini muda wa kumchunga na kumlea mtoto anakosa.

Yote hayo ukijumuisha lazima tabia za watoto zibadilike na haziwezi kuwa sawa na walioishi na baba zao na mama zao pamoja mpaka wanakwenda kujitegema, huenda zikabadilika zikawa hasi au chanya tabia hizo inategemea na kujitambua kwa mzazi na mtoto husika.

4. Kukosa matunzo bora iwapo mzazi aliebeba jukumu la malezi hana uchumi imara

Hayo ni baadhi ya madhara tu ambayo mtoto humkumba baada ya wazazi kutengana ila yapo mengi zaidi kuliko hayo, ewe mzazi mambo ya kuzingatia,


Michango ya wadau

Lawama isitupwe kwa wanawake pekee



--------------------




=====================

Changamoto wanazopata wanaume walio kwenye mahusiano na single mothers


---------------------------



Changamoto wanazopata single mothers walio kwenye mahusiano na wanaume wengine / ndoa na wanaume wengine

Kuolewa au kuingia kwenye mahusiano mapya hali ya kuwa ulishawahi kuzaa mtoto au watoto kuna changamoto nyingi sana mwanamke hupitia akiwa ndani ya hayo mahusiano mapya, nitaelezea baadhi ya changamoto hizo
  • Mwanaume kukataa kubeba jukumu la ubaba kwa watoto wasio wa kwake, kama kuwaonesha upendo kama watoto wake au kuwapa huduma stahiki kama elimu bora na mahitaji muhimu, hali hii hujitokeza hasa kwa kuona anamsaidia mwenye jukumu ambaye ni baba wa mtoto hivyo kutokuwa tayari kufanya hivyo.
  • Wanawake kuwa na hofu ya watoto wao kufanyiwa vitendo vya kikatili na baba zao wa kufikia hasa kulingana na kuongezeka kwa matukio kama hayo katika jamii
  • Mama kuona kama baba wa kufikia hutoa adhabu kali kwa watoto wake hasa wanapokuwa wamekosea, na mama kutotamani mtoto kupata adhabu ya kiwango hicho na kuhisi anampa adhabu hiyo kwa kuwa si mtoto wake wa kumzaa
  • Wanaume kukataa kuishi na mtoto aliomkuta naye mwanamke, hivyo kumlazimu kuwapeleka kwa ndugu zake na kusababisha mtoto kuishi bila upendo wa wazazi
Asante sn mtoa mada nilikue
Wa naisubir kwa hamu sn hii topic mm nimelelewa familia ya wanawake watupu mama na dada zangu wawili wakubwa ambao wana baba zao kila mmoja na baba ake mtoto wa 3 nina baba yangu ambae ndie alikuwa tegemez ata kwa wale dada wasio wanae ila alikuwa ameoa mke mwengine ambae aljkuwa anaish nae nyumban alikuwa anakuja mara chache sn aisee usiombe kuzaliwa familia ya hii balaa lipo hv

1.mama alitumia nguvu nyingi kunidanganya km bawa dada zangu tumezaliwa baba mmoja
2.nilitumika km kitega uchumi mama alikuwa akimuandikia baba barua juu ya matumiz yangu lkn pesa zilipoletwa zilitawanywa na sikupata ata punje
3.mama hataki kukosolewa na anachotaka ufanye kile anachokuagiza utasikia nasema ivyo km mama io ni amri
4.dada zangu hawakuwa na upendo ni full vijembe mipasho na matusi mama yupo apo anaangalia
5.baba akija kutembea wanabadilika wanajifanya wananipenda
6.ukipata matatizo au ukilia wanashangilia tena wanacheka kabisa niliwah kuwakuta dada na mama wanashangilia hii ni baada ya kunisingizia kwa baba kuwa nimempiga mama
7.unalazimishwa kuvaa nguo wanazotaka

Naomba tuishie apo wadau maana nikisema nijaze utawachukia wanawake wote WANAWAKE NI WANAFIKI i hate them siku nikipata mda ntakuja ma thread
 
Bahahaha! Ngoja nikuthibitishie jambo wazazi hao sasa hivi hawapo tena na mimi ni mmoja wao tumeshapotea hata awe na kiwanda kama cha Lamborghini ni chake i better die poorly.

Mzazi anayefanya jambo ili aje kumtegemea mtoto wake baadae huyo ni loser mkubwa. (Akili za kimasikini)
Khudos to yu
 
Back
Top Bottom