Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 482
sasa kwa nini u-date matatizo wakati wanawake wasio na watoto ni wengi sana?
Siongle mama for single baba, angalau wana common story ya kuongelea.
Nao wana shida pia ingawa sio wote!
Kunakuwa kuna competition ya aina fulani ambayo huendeshwa kisirisiri kiasi kuwa mmoja huona mtoto wake ndo bora zaidi.
Kuna pia mifano!
Rafiki yangu ana watoto kadhaa! Kwa kuona kuwa watoto wake wanaweza kupata shida akaamua kuoa single mother! Alimweleza ukweli kuwa ana watoto kadhaa!
Yule mama alikuwa na mtoto 1 wa ka miaka 6 hivi. Mwanaume alimchukua mtoto kama wake kabisa! Anampeleka shule anaenda kumchukua hasa ikizingatiwa kuwa huyu mtoto alikuwa wa kike!
Watoto wa huyu mwanaume walikuwa nearly the same age na wakati baba yao anaoa walikuwa boarding school. So maisha raha tu. Shida pale binti alipomaliza darasa la 7! Alipelekwa shule ileile ya wale watoto wa mwanaume walikuwa wanasoma.
Wakiwa shule binti wa mama anakuwa na vitu vingi tofauti na wale wa mwanaume! Anakuwa na pocket money kuliko wale wa mwanaume. Anaye lipa ada ya watoto watatu wote ni mwanaume! Watoto wakajiuliza huyu mwenzetu kulikoni na tunatoka nyumba moja. Wakaweka wazi kwa wazazi likizo moja! Hapo ndo waliaribu kabisa! Mama hawataki ooooooh wanamwonea wivu as mtoto wake anajua kutunza vitu hata hela anazopewa anahifadhi so wanamwonea wivu tu! Baba akaanza kujumlisha 2 na mbili! Suluisho alilooona (sijui kama alikuwa sahihi) naye akaanza kuwaongezea watoto wake kwa siri! Mashindano yakaendelea mwisho wenyewe kwa wenyewe watoto wakaanza kutimuana! Mapenzi yamezidi kwa watoto na wameamua kukosana kisa more attention to kids! Silikatai hilo ila nafasi ya baba/mama nayo inatakiwa ipewe priority!
Hivi niongeavyo kuna mpasuko mkubwa sana kwa hawa wanandoa! watoto wa baba wanataka mtoto wa mama aende kwa baba yake. Najiuliza wanafikiri watabakia salama wakibakia na huyu mama peke yao!