Wako wapi wale waliokuwa wanatetea umeme wa maji utakuwa bei rahisi?

Huenda unachanganya au huelewi lolote
Gharama zipo chini kwenye kuzalisha umeme kwa maji kuliko vyanzo vingi. Sasa kwa nn bei kwa unit anayonunua mwananchi ipungue au isipungue hili unapaswa kuwa mpole kwanza maana ndio mradi unakamilika bado haupo kwa 100% megawatt kwa sasa zinazoingua grid ya taifa bado ni chache, subiri uishe kabisa uingize megawatt zote tunazotumia 1800mw

Bado kwa asilimia kubwa tunatumia umeme wa gesi, subiri mradi uishe uende kureplace umeme wa gesi ndio uje na hili swali
 
Unaijua initial cost ya solar system?
Hata maintenance tu ya hizi solar panel gharama ni kubwa sana
Watu wanajiandikia tu wala hawajifunzi na kufanya tafiti. Mm sio mtaalamu wa umeme, lakini mtu hawezi kuniongopea kuhusu vyanzo vya nishati
 
Nakujibu kwa ufasaha
Kwa nchi kama Tanzania ni hatari kutegemea umeme wa gesi sababu gesi ni non renewable, gesi inaisha. Matumizi ya umeme yanapanda kila mara, fikiria matumizi yetu yamefikia mw 2500+ na gesi imepungua, hapo unajua nn kitatokea?

Maji ni renewable, lakini pia uzalishaji wa umeme ni cheap kulinganisha na gesi.

Mwisho kwa nn tunapaswa kuwa na vyote ni sababu gesi sio yetu Ila bwawa ni letu. Gesi tunayozalisha umeme tunainunua kutoka kwa mwekezaji ambae anaweza kuamua kuja kupandisha Bei per unit
 
Hata maintenance tu ya hizi solar panel gharama ni kubwa sana
Watu wanajiandikia tu wala hawajifunzi na kufanya tafiti. Mm sio mtaalamu wa umeme, lakini mtu hawezi kuniongopea kuhusu vyanzo vya nishati
Mimi sijaongelea umeme wa solar kwa ajili ya matumizi ya serikali/uwekezaji wa serikali! Ninaongelea kwa matumizi ya mtu binafsi.

Kwa mfano solar ya watt 100! Unachobadilisha ni betri yake tu ya N 100 kavu, kila baada ya miaka 2-3. Na bado utapata taa, utachaji simu, utaangalia tv, nk. Nimefanya hiki kitu kijijini, na kimezaa matunda.
 
Hapa ilikuwa inazungumzwa uzalishaji wa umeme tanesco, ndio lengo la hii post. Sasa sijui we ya mtu mmoja imekuwaje ukaileta
Pia mtu angejuwaje unazungumzia wa mtu mmoja?
 
Kwani tumeacha kuwekeza kwenye gasi?
 
Hapa ilikuwa inazungumzwa uzalishaji wa umeme tanesco, ndio lengo la hii post. Sasa sijui we ya mtu mmoja imekuwaje ukaileta
Pia mtu angejuwaje unazungumzia wa mtu mmoja?
Sidhani kama mada inamfunga mtu kutoa maoni tofauti. Badala ya kulalamikia changamoto lukuki za umeme wa Tanesco, siyo mbaya mtu/watu akiamua/wakiamua kutumia umeme wa jua. Na sababu nimezitoa.
 
Mkuu bora umelileta hili, kilichokuwa kinahubiriwa kuwa bwawa la stiglaz litashusha bei ya umeme ili walau watu wa mjini waanze kupikia majiko ya umeme kiko wapi? ndo kwanza ukiweka umeme wa elfu 20 haumalizi wiki......hii ni hujuma kubwa kwa watanzania, na bado tozo zinaendelea kuwekwa kila mahala. Vijana wa nchi hii wakiendelea kulala wataishia kuwa watumwa kwenye vizazi vyao.​
 
Sidhani kama mada inamfunga mtu kutoa maoni tofauti. Badala ya kulalamikia changamoto lukuki za umeme wa Tanesco, siyo mbaya mtu/watu akiamua/wakiamua kutumia umeme wa jua. Na sababu nimezitoa.
Bado unapiga chenga, ilikua ngumu kujua unazungumzia individual level
 
Kuna uzi mmoja nilichangia kuwaambia Watanzania wajiandae kulipia umeme zaidi. Watu hawakuelewa.

Juzi kuna mdau kafukua kakubali utabiri wangu.
 
Watetezi nahisi wanauchungulia uzi Na kuupita kama vile hauwahusu......nje ya siasa mbovu tuliyonayo inayowalea Na kuwakumbatia walafi umeme ulipaswa ushuke bei Na si kuupandisha kama walivyofanya hawa mabazazi
 
Naomba nikuulize swali, kwa nn unasema umeme ulipaswa kushtuka Bei?
 
Ina maana wewe ni mgeni namna mwendazake alikuwa anaongoza nchi? Sasa huu ujinga unaoendelea sasa si ni utashi wa aliyeko madarakani na genge lake?

Mbona unajizima data. Hii nchi haina mipango na hata hiyo tume ya mipango ipo geresha.
Lione hata bunge letu, hivi utasema tuna bunge kweli?
Tanzania tulihitaji mtu mwenye uzalendo na utashi,maamuzi chanya ya kikatili.
Tulimpata bahati mbaya akaenda zake kabla hajamaliza aliyoyakusudia.
Ndio maana nasema angekuwepo watanzania tungekuwa na furaha sana kwakuwa huzuni zilipotea,zimeanza kurudi baada ya yeye kufariki.
Katuacha yatima. Leo hii hakuna kiongozi hata mmoja anayewapigania wananchi.
 
Kila kitu kilifia pale ile siku ya March 17.
Tukisema hii ilikuwa siku mbaya kwa watanzania muwe mnaelewa.
Yaliongelewa hayo kwakuwa nchi ilikuwa inaongozwa na mwanaume wa shoka.

Unategemea hawa wajinga waliobaki watafanya nini?
 
CCM NI MAJAMBAZI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…