Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Wakristo wengi wamekuwa wakishangilia maumivu, vita na vifo vinavyosababishwa na majeshi ya Israeli, kwa kisingizio cha kuiunga mkono au kulibariki taifa la Israeli. Je, msimamo huo unaendana na mafundisho ya Yesu Kristo? Karibu tudadavue jibu la swali hilo kwa pamoja.
Kwanza kabisa, Yesu hakufundisha kushangilia mateso ya adui. Yesu alisema wazi: “Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.” (Mathayo 5:44). Hii ina maana Mkristo hapaswi kufurahia maangamizi ya watu, hata kama ni “maadui.” Badala yake anatakiwa kuwaombea.
Kwa hiyo, kushangilia mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza, Lebanon, Syria, Iran na Yemen ni kinyume kabisa na mafundisho ya Kristo.
Pili, Yesu alikataza matumizi ya upanga kama njia ya kukabiliana na adui. Wakati ule watu walipoenda kumkamata Yesu, Petro aliuchomoa upanga wake akamkata sikio mtumishi wa Kuhani mkuu. Yesu alimwambia Petro: “Rudisha upanga wako mahali pake; maana wote waushikao upanga wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?” (Mathayo 26:52)
Hapo Yesu ametupa fundisho: Mkristo wa kweli hapaswi kumwaga damu wala kufurahia damu ya mtu inapomwagika.
Tatu, kulipiza kisasi sio jukumu la Mkristo. “Msijilipize kisasi… kisasi ni changu, asema Bwana.” (Warumi 12:19)
Mkristo hatakiwi kulipa kisasi wala kushangilia mtu anapolipa kisasi dhidi ya adui yake. Badala yake Mkristo anapaswa kuwa mpatanishi kati ya mtu na adui yake. “Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.” (Mathayo 5:9)
Hivyo badala ya kushabikia vita, Mkristo anapaswa kuombea amani na mapatano kati ya wanaopigana.
Shetani ndiye anayefurahia damu ya wanadamu inapomwagika, kwa sababu yeye ni muuaji tangu mwanzo (Yohana 8:44). Tumkatae anapotushawishi kujiingiza kwenye mijadala ya kuishangilia Israeli inapowapiga majirani. Tumpinge shetani, kwa Jina la Yesu, aache pia kuwashawishi watu kuuana (Yakobo 4:7).
Baada ya kujifunza yote hayo, bado unayo sababu ya kuendelea kushabikia mauaji yanayofanywa na IDF?