Father Kitima ni campaign manager wa Lissu mwaka 2020, Samia alikuwa na haki ya kumshambulia kwani alichangia kuweka upinzani kwenye suala la DP World mwaka juzi akiwa hana uelewa wa kipi kinachokwenda kufanyika.
Father Kitima alisambaza barua ya chuki makanisani akiita waraka, aliongelea mikataba huku akiandika habari za kupotosha umma, mkataba ulivyoweka wazi na ufafanuzi ukatolewa hadharani ikiwa aibu ya Father Kitima.
Juzi ameita press akijua kesho yake Rais anakwenda kuongea na umma, kimaadili yale ni makosa ni ukosefu wa heshima kwa mkuu wa nchi. Father Kitima pia ameongea kwa kutumia maneno yanayohamasisha vijana waingie mitaani kumbuka huyu ni mtu wa karibu wa Lissu kwa miaka mitano.
Samia amekwazwa na Father Kitima kwa muda mrefu alikuwa na haki ya kumkumbusha anachokifanya hakina afya kwa mustakabali wa muda mrefu wa TZ.
Samia kaamua kupita njia ile ile ya hayati JPM bila ya kuangalia wala kusikiliza mtu mmoja mmoja. Unataka kuniambia Father Kitima angeweza kuyatenda haya ingekuwa Rais ni hayati JPM?.
Natambua ukweli kwamba aliwahi kushambuliwa na watu pale Kurasini.