Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Yule Ngalekumtwa wa Iringa ndo mkuu wa Baraza la maaskofu TEC ( Sijui anaitwa Rais wa TEC/mwenyekiti)

Kwa maana hiyo ndio kiongozi wa Maaskofu wote wa Katoliki Tanzania
Hapana Rais sasa ni Askofu Mkuu Gervais Mwasikwabhila John Nyaisonga, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mbeya. Yeye leo alikuwa kule Lupaso. Jamani mnatala Rais azikwe na Padre tu bila Askofu?
 
Soma comment vizuri kaka
 
Hapana Rais sasa ni Askofu Mkuu Gervais Mwasikwabhila John Nyaisonga, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mbeya. Yeye leo alikuwa kule Lupaso. Jamani mnatala Rais azikwe na Padre tu bila Askofu?
.... wanasahau hata kuapishwa aliapishwa urais na askofu. Ni sawa na rais mstaafu mwislamu azikwe na shehe wa kijiji haiingii akilini. Sioni Sheikh Mkuu akikosa unless ana udhuru wa ajabu.

Madaraja katika jamii hayaepukiki ndio maana Mkapa alipigiwa mizinga 21 wakati akina sisi hata manati hairuhusiwi.
 
Kipindi cha ukabaila kule Ulaya, maaskofu walikuwa wananeemeka sana huku mapadri wakiisoma namba.

So tangu na tangu maaskofu wamekuwa kwenye tabaka fulani la kibepari


Askofu na padri ni akina nani hao???
 
... daraja lake ni nini/lipi?
Mkuu.

Daraja yake ni Upadri. Lakini Upapa ni cheo tuu.

Mfano: Kwa Tanzania kila Waziri ni Mbunge sio ndio? Kwenye Kanisa ndio ilivyo kila Askofu au Papa au Monsyori woote ni mapadri kwanza Kisha ndio wanapewa ivyo vyeo kadili ya tartibu za Kanisa.
 
Sio mapadri tuu mbona ata kwenye mazishi tuu mengine masikini akifa mwenyekiti kitongoji au balozi anatangaza kuwakilisha serikari lakini akifa mtu mashuhuri au tajiri utakuta viongozi was just ndo watoa taari kutonga ngazi ya wilaya au mkoa au kata kiongozi
 
Aaah, ndivyo unavyoelewa? Kwanza nakubaliana na wewe kwamba Sakramenti za kanisa Katoliki ziko 7: Ubatizo, Ekaristi takatifu, Kipaimara, Kitubio, Mpako wa wagonjwa, Daraja takatifu na Ndoa. Sasa kwenye daraja takatifu kuna madaraja matatu ambayo ni: Ushemasi, Upadri na Uaskofu. Nakubaliana na wewe kwamba Upapa siyo daraja takatifu.
 
Reactions: dtj
Mleta Maada ana hoja ya msingi sana, Muumini wa kawaida sana akifariki hata Padri unaweza usimuone kwenye ibada, akifa muumini aliekuwa ba jina basi Padri utamuona, akifa muumini mzito kabisa utamuona askofu.

Hii ni kwa makanisa yote ukitoa Waislam
 
Asante nimejiridhisha. Upo sahihi.
 
Mleta Maada ana hoja ya msingi sana, Muumini wa kawaida sana akifariki hata Padri unaweza usimuone kwenye ibada, akifa muumini aliekuwa ba jina basi Padri utamuona, akifa muumini mzito kabisa utamuona askofu.

Hii ni kwa makanisa yote ukitoa Waislam
Hapana siyo kweli! Ukiona muumini umegomewa kuja kuzikwa na Padre basi ujue ulikuwa na vikwazo yaani ulikuwa umefungiwa masakramenti. Mazishi ya muumini ni kazi ya Padre na siyo ya katekista. Hao wote unaoona wanzikwa na makatekista walikuwa na matatizo kanisani!
 
Labda huko kwenu (sijajua dhehebu gani). Lakini kwa hali ya kawaida, Askofu wa Kanisa Katoliki ndiye mwenye mamlaka ya kutoa sakramenti ya Kipaimara, hivyo ni mara nyingi tu huwa wanafika (hata kwa hao unaowaita makapuku), ingawa mara chache anaweza kutoa kibali kwa Padri (hasa katika ukatukumeni) kuitoa sakramenti hiyo. Misa ni ile ile, ya kawaida, sikukuu, ndoa, kipaimara, mazishi etc, isipokuwa vipengele mahususi ndio vinatofautiana
 
Mleta Maada ana hoja ya msingi sana, Muumini wa kawaida sana akifariki hata Padri unaweza usimuone kwenye ibada...
Kama hukumuona Padri kwenye ibada ujue huyo marehemu alikuwa ana vikwazo ambavyo kwa makusudi hakutaka kuviondoa wakati alipokuwa hai, mfano kuishi kama mke na mume bila ndoa, kuishi bila ubatizo, kutoshiriki jumuiya (ingawa hii Paroko hutoa uamuzi ). Kwa hiyo si kila mtu, chukua fursa hii uwaeleze wenzako watimize wajibu huo kabla hawajalalamika kama wewe
 
Nikusahihishe kidogo. Katekista wa Kikatoliki hawezi kwenda kuendesha ibada au misa ambayo imekosa vigezo vya kuendeshwa na Padri. Kwa ufupi Padri akiwa na ratiba ngumu, anaweza akamtuma Katekista. Kama muumini ana vikwazo, si Katekista wala Padre atakayekwenda kuendesha misa/ibada. Sana sana labda amejitokeza mtu tu kuongoza sala za mazishi, ambazo hata hivyo ni nje ya utaratibu wa Kanisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…