Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa

Sio kweli

Huu uzi ni wa kuanzia Jumamosi sijui wameshaunganisha nyuzi karibia nne humu. Hadi umepoteza maana

Ila walishanirekebisha pia mkuu kwamba Rais ni Nyaisonga kwa sasa. Shukran
 
Ndo mana sometimes mimi naona Mungu haexist.... mbona matendo ya kibaguzi namna hii yanatokea, tena yanafanywa na wapakwa mafuta, yet Mungu yupo kimya.. he must be very unfair
Haya mambo tumejiwekea watu tu.

Na mtu akifariki, amefariki.

Hata akisaliwa na Papa, anabaki amefariki tu.

Siyo kwamba akisaliwa na Askofu au Papa atafufuka, kwa hiyo tulilie asaliwe na Papa ili uwezekano wa kufufuka uwe mkubwa zaidi.

Kulilia watu fulani wa hali ya chini wasaliwe na Askofu ni ujinga tu.

Kwa sababu ni sawa na kusema mimi mtumwa, nimekubali utumwa. Lakini napinga matabaka, sitaki kuchapwa fimbo na mnyapara, nataka kuchapwa fimbo na bwana mkubwa mwenyewe anayemiliki watumwa.

Sasa wewe ushakubali ni mtumwa, umeukubali utumwa, halafu unapinga matabaka? Wakati utumwa ni mfumo wa matabaka!

Unasema hupendi wengine wakifanya makosa wanachapwa na bwana mkubwa, wewe ukifanya makosa unachapwa na mnyapara tu?

Kitu cha msingi hapa ni kwamba dini zinaweka misingi ya utumwa na matabaka, sasa kama wewe hutaki habari za utumwa na matabaka, kataa dini iweze kujifikiria kama mtu huru.

Ukishakubali dini, umeshakubali utumwa.

Sasa utapingaje matabaka wakati ushakubali itumwa tayari?

Ndipi hapo unajikuta hata kupinga kwako matabaka kunakuwa kichekesho.

Unapinga matabaka kwa kusema nataka kuchapwa na bwana mkubwa, sitaki kuchapwa na mnyapara.
 
Hivi kuna utofauti gani kati ya Askofu na Padre/Padri ? Itakuwa vyema zaidi kama mtanipa maana ya wawili hawa.

Ahsanteni.
askofu ni mkubwa kuliko padre yeye anaongoza jimbo na huyu mwingine parokia lakini wote ni mapadre. sielewi vizuri sana
 
askofu ni mkubwa kuliko padre yeye anaongoza jimbo na huyu mwingine parokia lakini wote ni mapadre. sielewi vizuri sana
Askofu anaruhusiwa kuoa lakini Padri haoi...!! Walutheri tuna Askofu no Mapadri..
 
Levels baby...ipo world wide hiyo sio kwenye dini peke yake.
Umejibu vizuri mkuu, lakini pia kwa cheo alichokuwa nacho marehemu anafahamika na amefahamiana na watu wengi mpaka hata kwa kutembeleana na wakawa marafiki. Kwa mantiki hiyo maaskofu kama mwanadamu wa kawaida anamarafiki na mmoja wapo ni huyo marehemu anayemsema.
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.

Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?

Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie
Ni suala la simple management logic.
Watu wakitaka wazikwe na maaskofu, itabidi waajiriwe maaskofu wengi sana kuwahudumia na kuendesha mazishi.
Na vile vile watu wakitaka Rais awepo kwenye kila msiba si itabidi tuwe na marais wa kuzika tu?
Principle ya management, unakuwa na kiongozi ambaye wasaidizi wake wataendesha shughuli kwa niaba.
Na wasaidizi nao watakuwa na wasaidizi na hali kadhalika hadi mtu wa chini kabisa amehudumiwa.
Hii inaitwa pyramid ya management, ambayo ni halisia na natural na vile vile hata taasisi nyeti kama majeshi vile vile wanazo structures kama hizo.
Na structure hiyo iko hivi:

1596116963716.png

Unaweza iandika hivi:
CEO----------------------------------------ASKOFU
EXECUTIVES---------------------------MAPADRE
MIDDLE MANAGEMENT----------MASHEMASI
EMPLOYEES-------------------------------WAUMINI
 
chukulia mfano msiba wa Mengi au Komba angekuwa mtu kapuku asingezikwa kwa kukiuka taratibu za kanisa
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.

Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?

Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie

Elewa kwamba pale altareni padre na askofu wanakuwa na hadhi sawa upadre ni sacramenti na uaskofu ni kama cheo tu. Kwa hiyo misa ya mazishi inapoendeshwa na askofu au padre inabaki kuwa na hadhi ile ile.....

Simple logic ni kwamba aliyefariki ni Raisi mstaafu hivyo ana hadhi ya tofauti mbona hukujisikia vibaya makapuku kutoagwa uwanja wa uhuru au hili umeona ni jambo la kawaida
 
Sijawahi ona Masheikh wakiunda jopo la kuongoza ibada. Waislamu wanaweza kujibu vzr zaidi
Jopo la mapadre au maaskofu kuongoza ibada ni kawaida si tu kwenye mazishi bali hata ibada za kawaida za Dominica . Wanaweza kuongoza ibada wote kwa kuachiana sehemu fulani fulani ,mfano moja anaweza akaanzisha ibada mpaka kwenye neno (masomo) halafu akahubiri mwingine baada ya hapo kwenye mageuzo wanaweza kushiriki wote kwa pamoja halafu mwingine akahitimisha. Misa iliyofanyika pale Uhuru siku ya juma pili haikuwa misa ya mazishi bali misa ya Dominica (Misa za kawaida ya jumapili)
 
Elewa kwamba pale altareni padre na askofu wanakuwa na hadhi sawa upadre ni sacramenti na uaskofu ni kama cheo tu. Kwa hiyo misa ya mazishi inapoendeshwa na askofu au padre inabaki kuwa na hadhi ile ile.....

Simple logic ni kwamba aliyefariki ni Raisi mstaafu hivyo ana hadhi ya tofauti mbona hukujisikia vibaya makapuku kutoagwa uwanja wa uhuru au hili umeona ni jambo la kawaida
Hii aya ya mwisho haikuwa na haja ya kumshushua. Ulishanena vyema katika aya ya kwanza.
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.

Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?

Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie

Ni swala la ki protokali tuu! Akifa Padre hata RC au DC wanaweza wasishiriki maziko yake! Akifa Askofu Rais wa nchi anashiriki maziko na akishindwa anatuma mwakilishi!
 
Ndo mana sometimes mimi naona Mungu haexist.... mbona matendo ya kibaguzi namna hii yanatokea, tena yanafanywa na wapakwa mafuta, yet Mungu yupo kimya.. he must be very unfair
Akili za Mungu sio sawa na binadamu hata wewe kitendo cha ku fikilia ha- exist angekufutilia mbali basi ni rehema zake tu
 
Kuna Afisa mmoja wa kitengo nyeti alipata msiba wa Mzee wake huko kijijini, lakini ndugu wakamtaarifu kwamba hata Katekista tu amegomea Misa ya mazishi kisa marehemu alikuwa hashiriki jumuiya.

Alichofanya ni kusafiri na Padre wake pamoja na wasaidizi kutoka parokia aliyokuwa anasali town hadi kijijini wakamaliza kazi.

Infact,kama hakuna anayekujua kwenye haya madhehebu ni kisanga.
 
Naomba kuuliza wakristo wenzangu kuhusu taratibu za msiba. Akifariki mtu wa kawaida basi Padre tu husimamia ibada. Lakini akifariki mtu maarufu au tajiri basi huja Askofu tena akiwa na viongozi wengine kuendesha hiyo ibada.

Kwanini Askofu asiendeshe hiyo misa hata angalau kwa msiba wa kapuku mmoja ili kuondoa hii hali ya kuonekana Askofu yuko kwa ajili ya watu fulani tu?

Kimsingi kama itawezekana Wakristo tujitafakari upya taratibu zetu zote za mazishi. Kuna mambo hayako sawa.
Karibuni tuchangie
Na huu utaratibu wa kumuanika maiti mmeutoa wapi?
 
Utaratibu wa kumuweka marehemu watu wapite wamuangalie nao umekaaje? Mantiki yake nini hasa!
 
Back
Top Bottom