Wakristo waliotokea mikoa isiyo na Waislam wengi wana uelewa potofu juu ya Uislam na Waislam

punguza chuki, hakuna kitu km hicho, waislam ni watu pisi sana
Hawa wapuuzi wana chuki na dini ya wenzao,lengo na madhumuni kuoandikiza chuki kwa jamii,sielewi ni huko kwenye nyumba zao za ibada wanafundishwa kuwachukia hao waislam au la
 
Hata mimi hili suala la mabikira 72 na jua kuzama kwenye matope linanifikirisha sana.
 
Duuuh
 
Humu wakristo ndio wanaongoza kwa mada za chuki zidi ya waislam,na lengo wavuruge amani ya nchi halafu wao wakimbilie kwa wayaudi watuachie machafuko nchini, acheni udini na chuki
 
We ndio kiongozi wakueneza chuki za kidini humu mtandaoni,mnadhani nchi ikichafuka mtabakia salama,mnataka mambo ya kishenzi kama ya rwanda na ukabila wao, kila mtu apambane na dini yake ilimradi asivunje sheria za nchi
Uko sahihi mkuu 😎
 
Hapo kwenye swala tano hapo. Binafsi naona ni kusababisha noise polution kwa wakazi wanozunguka misikiti. Wee wanaanza kuita na ma loudspeakers lugha ambayo wala jamii inayozunguka hawaijui. Wanarudia maneno yale yale kwa muda wa nusu saa. Wanaharibu usingizi wa watu. Yaani mkiwa na watoto au wazee karibu na msikiti ni janga. Wanapiga kelele muda ambao kisheria siyo reasonable hours yaani kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni.
Sijui ni aya gani ambayo inawaambia mkiwasumbua wengine kwa makelele ya kurudia rudia kwa lugha isiyoeleweka ndiyo unapata thawabu.
 
Mimi nashukuru kwamba ni mtu ambaye naweza kusikiliza hoja za imani nyingine bila kuwa offended.
Mimi mkristo lakini 90% ya marafiki nilionao ni waislamu. Wananifunza mengi ya dini yao mengi hunivutia na pia nahisi nikioa ntaoa binti kutoka upande huo.
 
Safi
 
1)Mtume Muhammad s.a.w aliishi Makka kwa miaka 40. Katika miaka yote hiyo hakuwahi kupigana na yoyote au kumpiga yoyote au kumtusi au kuutweza utu wa mtu.

2)Alipotangaza kuwa yeye ni Mtume wa Mungu watu wa Makka wakaanza kumdhihaki, wakaanza kuwapiga maswahaba zake mitaani, haikutosha wakaanza kuwavamia majumbani mwao na kuwapiga.

3)Mtume akawaagiza maswahaba zake wahame waende Ethiopia kwa Mfalme wa Kikristu ili wakae huko na awahami. Mbali na hilo hakurudisha pigo lolote kutoka kwa hao wanaodhuru maswahaba zake.

4) Walimtenga Mtume Muhammad s.a.w pamoja na familia yake na maswahaba zake na kumwekea vikwazo kwa miaka 3 vya kibiashara, hakuna kuuza wala kununua kutoka kwao. Ilifika kipindi Mtume na maswahaba zake walikuwa wanakula nyasi.

5)Baadaye watu wa Makka wakaweka mpango kabambe kwa makabila makubwa ya hapo Makka wamuue. Mtume akahama kuhamia mji mwengine, mji wa Madina.

6)Wakubwa wa Makka hawakufurahiswa na kitendo cha Mtume kuhama, wakaamua kumfuata huko huko Madina na jeshi kubwa na Mtume hakuwa na jeshi la kupigana wala vifaa vya kijeshi, ila yeye na maswahaba zake wakaamua kupigana hivyo hivyo!

7)Wakati wa vita akawaamuru watu wake wasishambulie watoto, wanawake, wazee, wasikate miti wala kuharibu vyanzo vya maji.

8)Miaka 2 mbeleni watu wa Makka wakaja na jeshi kubwa na kuuzunguka mji wa Madina na kuzuia njia zote za usafirashaji, si chakula wala chochote kikazuiliwa kuingia. Waislamu wakaamua kupigana kwa mbinu ya kuchimba mahandaki.

9)Wakati haya yanatokea, wayahudi waishio Madina ambao waliingia mkataba wa kuishi kwa amani na Mtume na waislamu kwa ujumla walikuwa wakivunja makubaliano ya mkataba pale ambapo waislamu wakivamiwa na majeshi ya nje. Mtume akaamua kupambana nao hivyo hivyo ndani ya mji pia.


Kwa ufupi historia ya Mtume ipo hivyo! Ulitaka afanyaje? Ajilinde vipi yeye na kulinda damu ya watu waliyomuamini na ya akina mama, watoto na wazee?
 
Sijui kwanini masikini wengi kutwa wanabishana kuhusu dini tafuteni hela masikini nyie! Kila mtu aheshimu dini ya mwenzake! Mkibishana kuhusu dini mnapata faida gani? ..........m..B...w..a. Nyie
 
Mkuu mm in mkristo ila hata makanisa ya kilokole ni kero we fikiria wanavyopiga mziki usiku kucha huoni kwamba ni kero. Mfano hapa napokaa kuna kanisa LA kilokole wanapiga mziki na maombi mpaka wanakesha wamekuwa kero
 
Uislam na ukatoliki fate yao inajulikana ni kuzimu ya moto!

Protestants wao ni hit and mis! either you make it or go to hell!!

Wakatoliki ndio waliuanzisha uislam Kwa malengo yao na ibada zao za wafu zinafanana ,na hatma yao ni kuzimu tu hakuna mjadala!!!

Huna sababu za kutetea kitu ambacho ulizaliwa ukakikuta Kwa kuamini maandishi pekee !je alieandika kama alikosea je!!?
 
Ujinga uko kwenye waumini wa dini zote. I always believe hakuna dini inayoweza kuwa na wafuasi kwa asilimia 100%. Na sababu kubwa ni kuwa, kwa mfano Yesu Kristu alipokuja, waumini wa kiyahudi walikataa kumtambua. Hakuja kama vile walivyotegemea. Walitegemea angekuja kwa mabavu na maguvu na kusambaratisha kila kitu. He was humble and simple.
Ila walipomkataa alisema wazi, Ukristu nawapa zawadi watu wengine ambao hawajamjua Mungu wa kweli. Hakuufuta uyahudi, ila aliendeleza kazi yake kama alivyotaka.
Hata crushes za uislamu na ukristu miaka kadhaa baadae, hazikutoa mshindi. Ndio maana mpaka leo ukristu na uislamu upo.
Ni kukosa maarifa kwa baadhi ya watu wanaoamini dini inaweza kuenezwa kwa upanga. Hilo halipo na hiyo sio dini. Ni mauaji.
 
Nikiwa mdogo naona vijana wa kiislamu wanapita mtaani wanapiga dufu wakibisha hodi kukusanya sadaka. Ile plus msikiti wao ulikuwa duni sana, ikanifanya niamini waislamu ni ombaomba. Hata mji wa jirani kuna tajiri alikuwa anawajengea msikiti. Nilianini hawa ni watu duni. Kumbe sio
 
Dini zetu hasa Tanzania ni zao la utumwa na tawala za kikoloni

Fuatilia, sehem zilizotawaliwa na wazungu kasimama mkiristo na palipo na mwarabu kasimama mwisilamu

Kujivunia dini ni kujivunia utumwa
 
Chuki, roho mbaya, roho ya kwa nini, kiburi, dharau, majivuno n.k

Katika dini ya kiislamu hato ni magonjwa makubwa ndani ya nafsi na madhambi yake ni makubwa.

Mimi myislamu nikuchukie wewe nitanufaika na nini? Sipati thawabu ya aina yoyote!

Nikuchukue wewe ili iweje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…