Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili
KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
0
1. Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza,na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!
1
2. Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikishayeyote na Mola wetu Mlezi.
2
3. Na kwa hakika utukufu wa Mola wetu Mlezi umetukuka kabisa; hanamke wala mwana.
3
4. Na kwa hakika wapumbavu miongoni mwetu walikuwa wakisema uwongoulio pindukia mipaka juu ya Mwenyezi Mungu.
4
5. Nasi tulidhani kuwa watu na majini hawamzulii uwongo MwenyeziMungu.
5
6. Na hakika walikuwako wanaume katika watu walio kuwa wakitafutakujikinga kwa wanaume wa kijini; kwa hivyo wakawazidisha madhambi.
6
7. Na kwa hakika wao walidhani, kama mlivyo dhani nyinyi, ya kuwaMwenyezi Mungu hatamleta Mtume.
7
8. Nasi tulizigusa mbingu, na tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvuna vimondo.
8
9. Na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza;lakini sasa anaye taka kusikiliza atakuta kimondo kinamvizia!
9
10. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanao kaa kwenye ardhiau Mola wao Mlezi anawatakia uwongofu.
10
11. Na hakika katika sisi wamo walio wema, na wengine wetu ni kinyumena hivyo. Tumekuwa njia mbali mbali.
11
12. Nasi tulijua kuwa hatutomshinda Mwenyezi Mungu duniani, walahatuwezi kumponyoka kwa kukimbia.
12
13. Nasi tulipo usikia uwongofu tuliuamini. Basi mwenye kumuaminiMola wake Mlezi basi haogopi kupunjwa wala kudhulumiwa.
13
14. Na hakika wamo katika sisi Waislamu, na wamo kati yetu wanaoacha haki. Basi walio silimu, hao ndio walio tafuta uwongofu.
14
15. Na ama wanao acha haki, hao watakuwa kuni za Jahannamu.
15
16. Na lau kama wangeli simama sawasawa juu ya njia tungeli wanyweshamaji kwa wingi,
16
17. Ili tuwajaribu kwa hayo. Na anaye puuza kumkumbuka Mola wakeMlezi atamsukuma kwenye adhabu ngumu.
17
18. Na hakika misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msimuabudu yeyotepamoja na Mwenyezi Mungu.
18
19. Na hakika Mja wa Mwenyezi Mungu alipo simama kumwomba, wao walikuwakaribu kumzonga!
19
20. Sema: Hakika mimi namwomba Mola wangu Mlezi, wala simshirikishiYeye na yeyote.
20
21. Sema: Mimi sina mamlaka ya kukudhuruni wala kukuongozeni.
21
22. Sema: Hakika hapana yeyote awezae kunilinda na Mwenyezi Mungu,wala sitapata pa kukimbilia isipo kuwa kwake Yeye tu.
22
23. Ila nifikishe Ujumbe utokao kwa Mwenyezi Mungu na risala zake.Na wenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika hao watapataMoto wa Jahannamu wadumu humo milele.
23
24. Hata watakapo yaona wanayo ahidiwa, ndipo watakapo jua ni nanimwenye msaidizi dhaifu, na mchache wa idadi.
24
25. Sema: Sijui kama yapo karibu hayo mnayo ahidiwa, au Mola wanguMlezi atayawekea muda mrefu.
25
26. Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siriyake,
26
27. Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia. Naye huyo humwekea walinzimbele yake na nyuma yake.
27
28. Ili Yeye ajue kwamba wao wamefikisha ujumbe wa Mola wao Mlezi,na Yeye anayajua vyema yote walio nayo, na amedhibiti idadi ya kila kitu.
28
hindio tafsiri ya surati jini.wewe unasikiatu kunasura inaitwa surati jini ujawai kuisoma .