Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kama kuna jambo ambalo wakristo wengi wanadanganywa na kuibiwa basi ni kwenye kitu kinaitwa Sadaka.
Kila ujanja ujanja wa viongozi wa kikristo kutaka kuwatapeli waumini pesa na mali zao basi sadaka ndio kichaka cha kwanza na haraka sana kinatumika. Na jambo hili lipo kwenye madhehebu yote ya kikristo na hata dini zingine.
Kupitia mada hii nitaweka sawa kwa uchache mtazamo wa sadaka kulingana na imani halisi ya kikristo kupitia Biblia.
1. Sadaka ni ibada kamili (moyo wa muumini unakwenda moja kwa moja kukutana na Mungu wake), hivyo kabla ya kuitoa jiulize haya maswali makubwa matatu:
(a)Moyo wako ni msafi kiasi gani kumkaribia Mungu kwa njia ya sadaka (yaani uhusiano wako na Mungu wako ukoje wakati ule unapotaka kutoa hiyo sadaka) (Mathayo 5:8)
(b)Mali/Pesa inayotaka kuitoa kama sadaka ni halali kiasi gani katika mtizamo wa neno la Mungu mpaka imfae Mungu. (Yohana 4:24)
(c)Hiari ya kutaka kumtolea Mungu hiyo mali/pesa itokane na kumpenda tu huyo Mungu na sio vingenevyo (2Wakorintho 9:7)
2. Sadaka halisi inatolewa moyoni mwako (yaani dhamira ya hiari kwa kupenda kutoa kitu/kufanya jambo lenye thamani nzuri, kwa kwa lengo la kumrudishia Mungu utukufu). Vitendo vya utoaji wa sadaka ndio wanadamu wanaweza kuviona, na wala hupaswi kulazimisha kutengeneza mazingira ya watu waone au wajue ulichotoa.
3. Tendo la utoaji sadaka (yaani kule kutoa pesa au mali zako) linaweza kufanyika mahali popote pale, wakati wowote ule, kwa mtu yoyote ule, kwa namna yoyote ile, kwa kiasi chochote kile, lengo kuu likiwa ni kumrudishia Mungu utukufu huku ukiufurahisha moyo wako.
4. Michango yoyote ya makanisani au taratibu zote za utoaji mali na pesa makanisani kwa jina la Sadaka, kiuhalisia SIO SADAKA. Hizo ni taratibu za makanisa tu katika kuweza kujiendesha na kufanikisha shughuli zake za kila siku ama watu fulani mahususi wazitumie. Kwanini? Mara nyingi (kama sio mara zote) hizo taratibu hazihoji anayetoa kama ni msafi kiimani, hazihoji uhalali wa kule zilipopatikana na hazipendi kumpa muumini hiari ya moyo wake kuamua kutoa au kutokutoa (muumini atawekewa kiwango, atatishwa kiimani asipotoa atapata madhara au atashawishiwa kuwa akitoa atabarikiwa). Wewe utaambiwa toa tu, tena toa nyingi uwezavyo. Ni unyonyaji kwa 100%.
5. Mwisho kabisa, kila mkristo anapaswa kujua haya:
-Hatuendi mbinguni kwa kutoa sadaka wala kwa kutokutoa sadaka hatukosi mbingu
-Hatununui baraka kwa kutoa sadaka na wala hatuvuni laana kwa kutokutoa sadaka.
-Hatulaaniwi kwa kutokutoa sadaka na wala hatuvunji laana kwa kutoa sadaka.
-Tunapaswa kutoa sadaka (popote pale, kwa namna yoyote ile, kiasi chochote kile) kwa sababu tunampenda na kumfurahia Mungu wetu, tusilazimishwe wala kushawishiwa kiujanja ujanja.