Wakristo wengi wanadanganywa kuwa kupeleka pesa na mali kanisani ndio kumtolea Mungu sadaka!

Status
Not open for further replies.
Ila kupeleka sadaka nyingi kwa waganga wa kienyeji na mizimu ndio sahihi?

Kitu kisicho faida kwako kwa nini kiumize akili yako ilihali unaowazungumzia hakiwapunguzii kitu na maisha yao yangali yanaendelea bila kutembeza bakuli kwako??
🥰🙏
 
Habari,achana na hadithi za kusadika ndani ya biblia huwezi kuishi na kuendesha maisha yako kwa mistari ya kitabu kilocholetwa na wakoloni,huo ni ujinga
Kipi sasa hakikuletwa na wakoloni?
Kuhesabu, kusoma na kuandika vyote ni vililetwa na mkoloni.
Viatu, nguo, sabuni vyote ni project za mkoloni.
Shule, Hospitali, mahakama ni kazi ya mkoloni.
Umeme, simu, magari, computer, nternet ni kazi ya mkoloni.

Sisi vyetu vilikuwa ni kutembea peku, kuishi bila nguo, kujisaidia vichakani na kuzaana kama wanyama.
 
Nani anaweza kufanikiwa bila kutoa sadaka ukiona mtu hatoi sadaka kanisani ujue Kuna mahali anakotoa sadaka
Hoja hapa ni kuhusu utapeli unaofanywa na makanisa kuwapiga waumini pesa na mali zao kiholela huku neno sadaka likitumika. Yale mengi yanayofanyika makanisani ni michango na uporaji lakini kwa mtazamo halisi wa kikristo sio Sadaka.
 
Una hakika huko makanisani watu hawalalamiki kuhusu kupigwa kupitia kichaka cha wizi kinachoitwa Sadaka?
Pita ukaone, ni kilio kupitiliza.

Hakuna kanisa ambalo halina waumuni wasiolalamika kuhusu hizo taratibu za Sadaka zinavyowatesa, kuwaumiza na kuwachosha.
Walishawahi kukulalamikia?

Unafikiri watu waajinga kiasi hiko? Thubutu
 
Naona bado unachanganya vitu hapa.
Madhabahu za madhehebu ni madhabahu za madhehebu, zimejengwa na madhehebu kwa malengo ya hayo madhehebu na hizo sio madhabahu za Mungu alizozijenga yeye kwa gharama ya kumtoa Yesu kristo msalabani.

Mungu sio mjinga kuingia gharama ya kutengeneza madhabahu ndani ya moyo wa mwanadamu ili mwanadamu amuabudu (atoe sadaka) kupitia hizo. (Yohana 4:24). Yaani Mkristo atakuwa ni mpumbavu kabisa kuikwepa kuitumia hiyo madhabahu ya thamani kubwa sana iliyojengwa kwa damu ya Yesu iliyopo ndani yake kutolea sadaka zake ili kwenda kusaka madhabahu za madhehebu.
Nakubaliana na wewe kuhusu mtu binafsi kuwa na madhabahu ndani yake bila shaka, ninachosema ziko madhabahu za jumuiya pia

Na Yesu alisema wakikutana wawili au watatu kwa ajili yangu nitakuwepo katikati yao.

2Wakorintho 6:16... Mungu anakaa ndani yetu NA kati yetu anatembea( kati yetu maana yake ni ndani ya jumuiya/kanisa).

Muhimu ni kuwa ibada ikifanyika kibinafsi au kijumuiya, the centre of focus should be on the person of Jesus. Maana yeye ndiye Kuhani Mkuu, ndiye Dhabihu takatifu, na ndiye Mungu astahiliye ibada.
 
Kama kuna jambo ambalo wakristo wengi wanadanganywa na kuibiwa basi ni kwenye kitu kinaitwa Sadaka.
Kila ujanja ujanja wa viongozi wa kikristo kutaka kuwatapeli waumini pesa na mali zao basi sadaka ndio kichaka cha kwanza na haraka sana kinatumika. Na jambo hili lipo kwenye madhehebu yote ya kikristo na hata dini zingine.

Kupitia mada hii nitaweka sawa kwa uchache mtazamo wa sadaka kulingana na imani halisi ya kikristo kupitia Biblia.

1. Sadaka ni ibada kamili (moyo wa muumini unakwenda moja kwa moja kukutana na Mungu wake), hivyo kabla ya kuitoa jiulize haya maswali makubwa matatu:

(a)Moyo wako ni msafi kiasi gani kumkaribia Mungu kwa njia ya sadaka (yaani uhusiano wako na Mungu wako ukoje wakati ule unapotaka kutoa hiyo sadaka) (Mathayo 5:8)

(b)Mali/Pesa inayotaka kuitoa kama sadaka ni halali kiasi gani katika mtizamo wa neno la Mungu mpaka imfae Mungu. (Yohana 4:24)

(c)Hiari ya kutaka kumtolea Mungu hiyo mali/pesa itokane na kumpenda tu huyo Mungu na sio vingenevyo (2Wakorintho 9:7)

2. Sadaka halisi inatolewa moyoni mwako (yaani dhamira ya hiari kwa kupenda kutoa kitu/kufanya jambo lenye thamani nzuri, kwa kwa lengo la kumrudishia Mungu utukufu). Vitendo vya utoaji wa sadaka ndio wanadamu wanaweza kuviona, na wala hupaswi kulazimisha kutengeneza mazingira ya watu waone au wajue ulichotoa.

3. Tendo la utoaji sadaka (yaani kule kutoa pesa au mali zako) linaweza kufanyika mahali popote pale, wakati wowote ule, kwa mtu yoyote ule, kwa namna yoyote ile, kwa kiasi chochote kile, lengo kuu likiwa ni kumrudishia Mungu utukufu huku ukiufurahisha moyo wako.

4. Michango yoyote ya makanisani au taratibu zote za utoaji mali na pesa makanisani kwa jina la Sadaka, kiuhalisia SIO SADAKA. Hizo ni taratibu za makanisa tu katika kuweza kujiendesha na kufanikisha shughuli zake za kila siku ama watu fulani mahususi wazitumie. Kwanini? Mara nyingi (kama sio mara zote) hizo taratibu hazihoji anayetoa kama ni msafi kiimani, hazihoji uhalali wa kule zilipopatikana na hazipendi kumpa muumini hiari ya moyo wake kuamua kutoa au kutokutoa (muumini atawekewa kiwango, atatishwa kiimani asipotoa atapata madhara au atashawishiwa kuwa akitoa atabarikiwa). Wewe utaambiwa toa tu, tena toa nyingi uwezavyo. Ni unyonyaji kwa 100%.

5. Mwisho kabisa, kila mkristo anapaswa kujua haya:
-Hatuendi mbinguni kwa kutoa sadaka wala kwa kutokutoa sadaka hatukosi mbingu
-Hatununui baraka kwa kutoa sadaka na wala hatuvuni laana kwa kutokutoa sadaka.
-Hatulaaniwi kwa kutokutoa sadaka na wala hatuvunji laana kwa kutoa sadaka.
-Tunapaswa kutoa sadaka (popote pale, kwa namna yoyote ile, kiasi chochote kile) kwa sababu tunampenda na kumfurahia Mungu wetu, tusilazimishwe wala kushawishiwa kiujanja ujanja.
Kichwa cha habari na habari yenyewe viko tofauti, Nikajua wakristo kupeleka sadaka ni utapeli yaani nikajua una andiko linalokataza mkristo kupeleka sadaka kanisani, kumbe hapana, unachojaribu kueleza ni namna sahihi ya mkristo kutoa sadaka mbele za Mungu. Ulichokieleza ni sahihi

Lakini si hoja ya mchungaji kuanza kuchunguza namna mkristo alivyotoa sadaka, sadaka inahusisha mahusiano binafsi na Mungu, wapo watu ambao hawakuwa na mahusiano na Mungu lakini sadaka yao Mungu aliiona soma habari za cornelio alikuwa anasaidia watu kwa moyo mweupe bila kinyongo ila mahusiano yake na Mungu hayakuwepo. Mungu anaangalia unyenyekevu wa Moyo,
 
Bora niwe mkristo mjinga kuliko hao wengine 😁😁😁😁😁
Ujinga sio kichaka cha Mkristo kujifichia. Kataa ujinga wa kiimani uwe huru, maana Mungu amekupa akili katika mambo yote. (2Timotheo 2:7)
 
Soma mada utaelewa.
Pata ufahamu ili utoke kwenye kongwa la kifikra la kidini ambalo linaongeza umaskini kwenye jamii zetu.
Hivi katika Waislam na Wakristo ipi ni jamii ya watu masikini sana, usiwapangie watu jinsi ya kuishi wewe kama unaona ni upuuzi wao wanaona ni ibada kwao, jali imani yako achana na imani za watu wengine ndiyo maana kuna uhuru wa kuabudu.
 
Kichwa cha habari na habari yenyewe viko tofauti, Nikajua wakristo kupeleka sadaka ni utapeli yaani nikajua una andiko linalokataza mkristo kupeleka sadaka kanisani, kumbe hapana, unachojaribu kueleza ni namna sahihi ya mkristo kutoa sadaka mbele za Mungu. Ulichokieleza ni sahihi

Lakini si hoja ya mchungaji kuanza kuchunguza namna mkristo alivyotoa sadaka, sadaka inahusisha mahusiano binafsi na Mungu, wapo watu ambao hawakuwa na mahusiano na Mungu lakini sadaka yao Mungu aliiona soma habari za cornelio alikuwa anasaidia watu kwa moyo mweupe bila kinyongo ila mahusiano yake na Mungu hayakuwepo. Mungu anaangalia unyenyekevu wa Moyo,
Kichwa cha habari kinasema Uongo unaofanywa na makanisa kuwaambia wakristo walete tu pesa na mali zao makanisani kama ndio kutoa Sadaka wakati sio sahihi kwa 100%. Na content yangu imejadili hilo.
 
Kama kuna jambo ambalo wakristo wengi wanadanganywa na kuibiwa basi ni kwenye kitu kinaitwa Sadaka.
Kila ujanja ujanja wa viongozi wa kikristo kutaka kuwatapeli waumini pesa na mali zao basi sadaka ndio kichaka cha kwanza na haraka sana kinatumika. Na jambo hili lipo kwenye madhehebu yote ya kikristo na hata dini zingine.

Kupitia mada hii nitaweka sawa kwa uchache mtazamo wa sadaka kulingana na imani halisi ya kikristo kupitia Biblia.

1. Sadaka ni ibada kamili (moyo wa muumini unakwenda moja kwa moja kukutana na Mungu wake), hivyo kabla ya kuitoa jiulize haya maswali makubwa matatu:

(a)Moyo wako ni msafi kiasi gani kumkaribia Mungu kwa njia ya sadaka (yaani uhusiano wako na Mungu wako ukoje wakati ule unapotaka kutoa hiyo sadaka) (Mathayo 5:8)

(b)Mali/Pesa inayotaka kuitoa kama sadaka ni halali kiasi gani katika mtizamo wa neno la Mungu mpaka imfae Mungu. (Yohana 4:24)

(c)Hiari ya kutaka kumtolea Mungu hiyo mali/pesa itokane na kumpenda tu huyo Mungu na sio vingenevyo (2Wakorintho 9:7)

2. Sadaka halisi inatolewa moyoni mwako (yaani dhamira ya hiari kwa kupenda kutoa kitu/kufanya jambo lenye thamani nzuri, kwa kwa lengo la kumrudishia Mungu utukufu). Vitendo vya utoaji wa sadaka ndio wanadamu wanaweza kuviona, na wala hupaswi kulazimisha kutengeneza mazingira ya watu waone au wajue ulichotoa.

3. Tendo la utoaji sadaka (yaani kule kutoa pesa au mali zako) linaweza kufanyika mahali popote pale, wakati wowote ule, kwa mtu yoyote ule, kwa namna yoyote ile, kwa kiasi chochote kile, lengo kuu likiwa ni kumrudishia Mungu utukufu huku ukiufurahisha moyo wako.

4. Michango yoyote ya makanisani au taratibu zote za utoaji mali na pesa makanisani kwa jina la Sadaka, kiuhalisia SIO SADAKA. Hizo ni taratibu za makanisa tu katika kuweza kujiendesha na kufanikisha shughuli zake za kila siku ama watu fulani mahususi wazitumie. Kwanini? Mara nyingi (kama sio mara zote) hizo taratibu hazihoji anayetoa kama ni msafi kiimani, hazihoji uhalali wa kule zilipopatikana na hazipendi kumpa muumini hiari ya moyo wake kuamua kutoa au kutokutoa (muumini atawekewa kiwango, atatishwa kiimani asipotoa atapata madhara au atashawishiwa kuwa akitoa atabarikiwa). Wewe utaambiwa toa tu, tena toa nyingi uwezavyo. Ni unyonyaji kwa 100%.

5. Mwisho kabisa, kila mkristo anapaswa kujua haya:
-Hatuendi mbinguni kwa kutoa sadaka wala kwa kutokutoa sadaka hatukosi mbingu
-Hatununui baraka kwa kutoa sadaka na wala hatuvuni laana kwa kutokutoa sadaka.
-Hatulaaniwi kwa kutokutoa sadaka na wala hatuvunji laana kwa kutoa sadaka.
-Tunapaswa kutoa sadaka (popote pale, kwa namna yoyote ile, kiasi chochote kile) kwa sababu tunampenda na kumfurahia Mungu wetu, tusilazimishwe wala kushawishiwa kiujanja ujanja.
Wewe ni nani hata uwapangie watu namna ya kutoa sadaka.
Waache watu watimize neno la Mungu kwa kutoa sadaka kwa moyo wa kupenda maana hakuna anayelazimishwa kutoa sadaka.
Hao wanaozitumia hizo sadaka vibaya watahukumiwq kwa matendo yao mabaya kama wanadamu. Kama na wewe unataka kutafuna hizo sadaka kwa nini usianzishe kanisa lako!
 
Hivi katika Waislam na Wakristo ipi ni jamii ya watu masikini sana, usiwapangie watu jinsi ya kuishi wewe kama unaona ni upuuzi wao wanaona ni ibada kwao, jali imani yako achana na imani za watu wengine ndiyo maana kuna uhuru wa kuabudu.
Uislamu umetokea wapi tena kwenye hii mada yangu?
Wapi nimezungumzia uislamu au kutaka kuwalinganisha waislamu na wakristo kwa chochote?
 
Kichwa cha habari kinasema Uongo unaofanywa na makanisa kuwaambia wakristo walete tu pesa na mali zao makanisani kama ndio kutoa Sadaka wakati sio sahihi kwa 100%. Na content yangu imejadili hilo.
Ni uongo kwa namna gani? Ili iwe uongo tuambie kwa maandiko wakristo walitakiwa kupeleka sadaka wapi?
 
Uislamu umetokea wapi tena kwenye hii mada yangu?
Wapi nimezungumzia uislamu au kutaka kuwalinganisha waislamu na wakristo kwa chochote?
Kwa sababu wewe ni Muislamu, hii mada haina tija wewe amini unachoamini utabaki salama kabisa waacchie watu na imani zao.
 
kabla ya kuitoa jiulize haya maswali makubwa matatu:
(b)Mali/Pesa inayotaka kuitoa kama sadaka ni halali kiasi gani katika mtizamo wa neno la Mungu mpaka imfae Mungu. (Yohana 4:24)
Sasa kumbe sadaka ni mali/pesa, umekwepa nini?
 
Wewe ni nani hata uwapangie watu namna ya kutoa sadaka.
Waache watu watimize neno la Mungu kwa kutoa sadaka kwa moyo wa kupenda maana hakuna anayelazimishwa kutoa sadaka.
Hao wanaozitumia hizo sadaka vibaya watahukumiwq kwa matendo yao mabaya kama wanadamu. Kama na wewe unataka kutafuna hizo sadaka kwa nini usianzishe kanisa lako!
Acha kupambana na mimi pambana na Biblia niliyonukuu kuhusu utoaji wa sadaka.
Kama unataka tukuelewe, njoo hapa na useme Biblia (neno la Mungu) ni nini mpaka iwapangie wakristo namna ya kutoa sadaka.
 
Kwanini watoaji wenyewe hawajawahi kulalamika, ila sisi ambao hatujawahi kutoa ndio kutwa kucha tunalalamika?, nitalichunguza hili, huenda kuna faida hawa waumini wanapata.
Kwa hiyo ukimkuta Mtoto anadhalilishwa utamuacha kwa kuwa halalamiki?. Au umkute Mlevi au Mwendawazimu anabakwa utasubiri alalamike ndio uone hatendewi sawa? Ingawa sijasoma andiko lote la Mleta uzi ila kwa kweli nasi tunahitaji ujasiri wa Kagame.
 
Kama kuna jambo ambalo wakristo wengi wanadanganywa na kuibiwa basi ni kwenye kitu kinaitwa Sadaka.
Kila ujanja ujanja wa viongozi wa kikristo kutaka kuwatapeli waumini pesa na mali zao basi sadaka ndio kichaka cha kwanza na haraka sana kinatumika. Na jambo hili lipo kwenye madhehebu yote ya kikristo na hata dini zingine.

Kupitia mada hii nitaweka sawa kwa uchache mtazamo wa sadaka kulingana na imani halisi ya kikristo kupitia Biblia.

1. Sadaka ni ibada kamili (moyo wa muumini unakwenda moja kwa moja kukutana na Mungu wake), hivyo kabla ya kuitoa jiulize haya maswali makubwa matatu:

(a)Moyo wako ni msafi kiasi gani kumkaribia Mungu kwa njia ya sadaka (yaani uhusiano wako na Mungu wako ukoje wakati ule unapotaka kutoa hiyo sadaka) (Mathayo 5:8)

(b)Mali/Pesa inayotaka kuitoa kama sadaka ni halali kiasi gani katika mtizamo wa neno la Mungu mpaka imfae Mungu. (Yohana 4:24)

(c)Hiari ya kutaka kumtolea Mungu hiyo mali/pesa itokane na kumpenda tu huyo Mungu na sio vingenevyo (2Wakorintho 9:7)

2. Sadaka halisi inatolewa moyoni mwako (yaani dhamira ya hiari kwa kupenda kutoa kitu/kufanya jambo lenye thamani nzuri, kwa kwa lengo la kumrudishia Mungu utukufu). Vitendo vya utoaji wa sadaka ndio wanadamu wanaweza kuviona, na wala hupaswi kulazimisha kutengeneza mazingira ya watu waone au wajue ulichotoa.

3. Tendo la utoaji sadaka (yaani kule kutoa pesa au mali zako) linaweza kufanyika mahali popote pale, wakati wowote ule, kwa mtu yoyote ule, kwa namna yoyote ile, kwa kiasi chochote kile, lengo kuu likiwa ni kumrudishia Mungu utukufu huku ukiufurahisha moyo wako.

4. Michango yoyote ya makanisani au taratibu zote za utoaji mali na pesa makanisani kwa jina la Sadaka, kiuhalisia SIO SADAKA. Hizo ni taratibu za makanisa tu katika kuweza kujiendesha na kufanikisha shughuli zake za kila siku ama watu fulani mahususi wazitumie. Kwanini? Mara nyingi (kama sio mara zote) hizo taratibu hazihoji anayetoa kama ni msafi kiimani, hazihoji uhalali wa kule zilipopatikana na hazipendi kumpa muumini hiari ya moyo wake kuamua kutoa au kutokutoa (muumini atawekewa kiwango, atatishwa kiimani asipotoa atapata madhara au atashawishiwa kuwa akitoa atabarikiwa). Wewe utaambiwa toa tu, tena toa nyingi uwezavyo. Ni unyonyaji kwa 100%.

5. Mwisho kabisa, kila mkristo anapaswa kujua haya:
-Hatuendi mbinguni kwa kutoa sadaka wala kwa kutokutoa sadaka hatukosi mbingu
-Hatununui baraka kwa kutoa sadaka na wala hatuvuni laana kwa kutokutoa sadaka.
-Hatulaaniwi kwa kutokutoa sadaka na wala hatuvunji laana kwa kutoa sadaka.
-Tunapaswa kutoa sadaka (popote pale, kwa namna yoyote ile, kiasi chochote kile) kwa sababu tunampenda na kumfurahia Mungu wetu, tusilazimishwe wala kushawishiwa kiujanja ujanja.
Ila mimi binafsi kupitia kutoa Sadaka mbalimbali kama Ujenzi wa Jengo la Kanisa, Uinjilisti wa Maeneo ya Mission, Matendo ya Huruma kwa Wahitaji, Ununuzi wa Vitendea Kazi vya Kanisa e.g Magari n.k Nimebarikiwa mno. Namshukuru sana Mungu kwa kuzipokea Sadaka zangu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom