Wakristo wengi wanadanganywa kuwa kupeleka pesa na mali kanisani ndio kumtolea Mungu sadaka!

Status
Not open for further replies.
Pole sana mkuu. Unaonekana unauelewa mdogo sana juu ya mambo haya. Nakushauri, jikite kwenye mada zingine, ya Wakristo waachie wenyewe.
 
Asante sana 🙏
 
Mzee subiri tende za bute kutoka uarabuni...acha wenye kutoa sadaka waliwe wenyewe. Hayakuhusu
 
...
 

Attachments

  • images - 2025-03-12T195056.186.jpeg
    15.1 KB · Views: 1
  • images - 2025-03-12T195344.083.jpeg
    11.1 KB · Views: 1
  • images - 2025-03-12T195301.353.jpeg
    9.2 KB · Views: 1
Kwanini watoaji wenyewe hawajawahi kulalamika, ila sisi ambao hatujawahi kutoa ndio kutwa kucha tunalalamika?, nitalichunguza hili, huenda kuna faida hawa waumini wanapata.
Wanalalamika sana,wengine hadi kufungua kesi,kutokana na kutoa sadaka wakiwa hawana akili timamu(kuombewa hadi kuchanganyukiwa)baadaye akili zikirejea huzirudia sadaka zao.
Nina ushahidi
 
Nina swali.
Mtu akitoa sadaka ya (mali),baadaye akabaini alikengeuka,anaweza kuirejesha?
 
Kwani watoaji wenyewe wasadaka wanasemaje? Au walikuja kulalamika kwako? Ai wewe umetoa hiyo sadak mara ngapi mpana uone wanadanganywa? Au wewe unajua mawazo au mawasiliano na Mungu wao?
Sadaka atoe mwingine Kwa MUNGU wake ,kulalama alalame mwingine maajabu haya! Acheni kuwagombanisha watu na Mungu wao.
 
Wanalalamika sana,wengine hadi kufungua kesi,kutokana na kutoa sadaka wakiwa hawana akili timamu(kuombewa hadi kuchanganyukiwa)baadaye akili zikirejea huzirudia sadaka zao.
Nina ushahidi
Kwani waliitwa au walifungwa kamba ? Mbisi wanaopeleka Kwa waganga wao sio sadaka.
 

Uliposema "jambo hili lipo kwenye madhehebu yote ya kikristo na hata dini zingine" ndio nimeona hujafanya tafiti zako vizuri. Sio madhehebu yote yanatoza sadaka au kuwalazimisha waumini wao watoe sadaka. Si kweli
 
Unahitaji kujifunza zaidi juu ya hili, bado unajichanganya
 
https://www.facebook.com/
View: https://web.facebook.com/photo?fbid=4077852792446550&set=pb.100006656077131.-2207520000
 
Agano la kale ni kivuli cha agano jipya na ndo maana torati ni takatifu ingawaje hatuko chini ya torati.

Kumbukumbu 12:13,14
"Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo;bali katika mahali atakapopachagua Bwana katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo."

Leo hatutoi sadaka za kuteketezwa lakini uone tahadhari ya kutokutoa sadaka popote pale.

Ni kweli mtu mwenyewe peke yako unaweza kuwa madhabahu ya Mungu lakini kanisa la mahali pamoja pia lina madhabahu yake. Haipaswi kutoa sadaka mahali mradi tu wanajiita kanisa, ni lazima ujue kama kweli wanafundisha neno la Mungu kwa usahihi.
 
Nina swali.
Mtu akitoa sadaka ya (mali),baadaye akabaini alikengeuka,anaweza kuirejesha?
Kama umenisoma vizuri, kwa mujibu wa imani ya Kikristo kupitia Biblia, utoaji sadaka ni suala binafsi, tendo la moyoni kwa hiari ya kupenda na kumfurahia Mungu na sio ile mali halisi inayoonekana ikitolewa.

Hizi blah blah nyingi zinazofanyika makanisani ni michango na kiuhalisia sio sadaka, sasa inategemea wewe mtoaji na ile taasisi mlikuwa na patano lipi ili kutaka kurejeshewa hiyo mali uliyoitoa.
 
Naona bado unachanganya vitu hapa.
Madhabahu za madhehebu ni madhabahu za madhehebu, zimejengwa na madhehebu kwa malengo ya hayo madhehebu na hizo sio madhabahu za Mungu alizozijenga yeye kwa gharama ya kumtoa Yesu kristo msalabani.

Mungu sio mjinga kuingia gharama ya kutengeneza madhabahu ndani ya moyo wa mwanadamu ili mwanadamu amuabudu (atoe sadaka) kupitia hizo. (Yohana 4:24). Yaani Mkristo atakuwa ni mpumbavu kabisa kuikwepa kuitumia hiyo madhabahu ya thamani kubwa sana iliyojengwa kwa damu ya Yesu iliyopo ndani yake kutolea sadaka zake ili kwenda kusaka madhabahu za madhehebu.
 
Habari,achana na hadithi za kusadika ndani ya biblia huwezi kuishi na kuendesha maisha yako kwa mistari ya kitabu kilocholetwa na wakoloni,huo ni ujinga
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…