Wakristo wengi wanadanganywa kuwa kupeleka pesa na mali kanisani ndio kumtolea Mungu sadaka!

Status
Not open for further replies.
Ni uongo kwa namna gani? Ili iwe uongo tuambie kwa maandiko wakristo walitakiwa kupeleka sadaka wapi?
Nimefafanua kwenye mada yangu kwa kina.
Kwa kifupi, Sadaka ni ibada kwa 100%, na kwa uhalisia ni ile hiari ya moyo wako kutoa au kufanya jambo kwa kupenda huku ukifurahi kwa lengo la kumrudishia Mungu utukufu (Yohana 4:24).

Sasa kwa mfano, kama jirani yako hana nguo au chakula na wewe kwa hiari yako mwenyewe (sio kwa kutishwa, kuchochewa, kupangiwa au kushawishiwa) ukatoa pesa zako kwa furaha kumpa ili apate Chakula au nguo kwa lengo la kumrudishia Mungu utukufu basi hapo ndio umetoa sadaka.

Hivyo, Sadaka (lile tendo la kutoa mali/pesa zako), inaweza kutolewa mahali popote, saa yoyote, kwa mtu yoyote pale kikubwa tu Moyo wako uwe umeguswa kwa hiari, kupenda na kufurahi huku ukidhamiria kumrudishia Mungu utukufu.

Hizi blah blah zingine makanisani ni michango tu ambayo inalazishwa itolewa kwa kivuli cha kichaka cha kuitwa Sadaka lakini kwa hakika sio Sadaka 100%.
 
Sadaka zipo za aina nyingi naona umezijumla kama ni aina moja.
Rudi shule ukasome zaidi kuhusu sadaka ni nini
 
Hakuna Imani bila sadaka hata kwa shetani ili uwe viwango vya juu sadaka ni lazima tena kule wanatoa asilimia 60% ya ulichopata.
 
Mtoa mada tusitoe sadaka halafu tusali chini ya miti kwenye vumbi?
au tusubiri mfalme wa Morocco aje atujengee msikiti kinondoni?
 
Historia ya sadaka imeanzia mbali sana tangia agano la kale.
Makabila 12 ya wana Israel kati yake makabila 11 yalipewa ardhi kwenye nchi ya ahadi Canaan. Kabila moja la Lawi halikupewa ardhi wao waliachwa maalum kwa ajili ya ukuhani. hivyo hayo makabila mengine yote yalikuwa yanatoa sadaka hekaluni na makuhani kabila la Lawi waliishi kupitia sadaka za makabila mengine.
Soma agano la kale usikurupuke.
 
Isaya 1:11
Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani?

Amosi 5:22
Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…