Wakuu mniombee nafanyiwa upasuaji kesho

Wakuu mniombee nafanyiwa upasuaji kesho

Mungu aliekupa Jicho akakupe Kuona tena hata baada ya upasuaji huo.

Mungu aliekupa Sikio akakupe na Kusikia tena hata baada ya upasuaji unaoenda kufanyika.

Pokea Uzima kwani ni ahadi yake kwetu tukiwa kama watoto wake.

Usiwe na Hofunwala usifadhaike, Bwana Yu pamoja nawe.

Enenda ukiwa na amani na ujasiri wa kuanza na kumaliza salama.

Tunakuombea...
 
Habari za jioni wakuu,.

Nimeogopa isije nikashindwa kurudi tena baada ya mda,.

Mungu akipenda kesho nitakua nikifanyiwa upasuaji wa Jicho pamoja na sikio,. Mniombee nirudi nikiwa salama kama mwanzo,..

Sikua napenda kufanya hivi ila ndio last option niliyobakiwa nayo Baada ya kujaribu na kubadilishiwa dawa for almost miezi miwili,. Madaktari wamesugget nifanye hiyo

Mniombee sio tu nitoke salama,. Pia niweze kupona nisike na kuona kama mwanzo🙏🙏🙏




Mkuu Mimi ntaamka saatisa kamili usiku tufanye Maombi kwa pamoja

Mungu aseme na moyo wako 🙏🏽
 
Back
Top Bottom