Wakuu mwenye uelewa na hii fursa nasikia mwisho Feb 28 mwezi huu watu wanakuwa matrilionea

nilikuwa mtu wa mwanzo kabisa kufanya KYC
Duh hongera sana mkuu, kimzaha mzaha mnaweza okota dodo kama wale walioiwahi Bitcoin. Mimi hii nimeifaham miaka mitatu nyuma kutoka kwa mtu wangu wa karibu lkn nilikuwa nampuuzia nimesanuka juzi juzi ananionesha kwenye sim kwamba wamebakiza siku chache wavune coins zao. Ikabidi nichimbue nikakuta kama Kuna ukweli flani japo Sina uhakika.
 
Mie sikutaka kupuuza kwa sababu sina ninachopoteza nilijaribu na nilipuuzwa lakini walionipuuza sasa hivi ndo wapiga debe wa hii Pi 😂, na kuhusu swala la taarifa binafsi za watu sikuwa na wasiwasi kwa sababu mimi sio double agent. Ni swala la muda tuu ngoja tuone kama tutachimba forever maana kuna jamaa mwanza alikuwa nazo 7000 alifariki last year, kitu bado hakina dalili ya kuingia sokoni kwa upande wake ni kama kachimba forever
 
Mimi nimeomba KYC lkn mpk sasa hawajaniverify yaani wallet balance naiona kabisa ila KYC sasa dah
Una muda gan umejiunga na wallet Ina Pai ngap boss, kupata kYC hasa kwa account za hivi karibuni ni mbinde sana
 
Halafu kamilisha usajiri wako zinatakiwa tick 5 hapo zikamilike tofauti na hapo unamaliza bando lako bure, wanadai mwisho kukamilisha KYC ni trh 28 mwezi huu. Ukichelewa hutaweza kunitumia hizo coins
Ngoja nicheki hizi mambo huwenda ndio zinanicheleweshea kyc
 
Ninaamini pesa inakuja kwa kufanya kazi kwa bidii na nidhamu tu.
Hakuna miujiza kwenye mafanikio zaidi ya bidii na nidhamu.
Online zipo pesa nyingi tu wenye akili hawahitaji hio bidii na nidhamu bali Wana risk na wanatoboa wakiwa wamelala kitandani
 
Hizo coin ukizipata unazifanyaje ili kupata pesa..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…