Binadamu kagawanyika makundi 3 yanayounda mtu mmoja kamili! Mwili ni sehemu ya mtu inayoweza kujigawa! Roho ni sehemu ya mtu inayoweza kujigawa! Nafsi ni sehemu ya mtu inayoweza kujigawa!
Mtu anapokuwa amelala, roho hailali usingizi bali mwili! Ikitokea ukajeruhiwa na vitu kama mapenzi na dhuruma, kinachoumia ni nafsi bali mwili na roho vinashiriki kuugulia kwasababu nafsi, roho, na mwili kwa mtu aliyehai vyote viko pamoja kwa umoja!
Na Mungu ndo hivyo hivyo! Mungu Baba, Mungu mwana, Mungu Roho mtakatifu!
Kwa umoja huu ndo Mungu!
Japo wewe sio Mkristo lakini Biblia imeliweka wazi!
"NA TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU"
Mwanzo 1:26
[26]Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Kwahiyo, ndani ya Mungu kuna uwezo wa kujifanya mwili (ndivyo alivyofanya Yesu), Mungu ni Roho ndivyo alivyo (hata Yesu alivyotaka kufa yeye mwenyewe) alitoa Roho yake akafa mwili akafanya aliyoyafanya alafu akautwaa mwili uleule akafufuka na huo mwili anao mpaka leo. Ndani ya Mungu kuna huwezo wa kimamlaka (Mungu Baba) kama ilivyo ndani ya mwanadamu nguvu ya kimamlaka ni hile roho inayotawala nafsi!
Naishia hapa! Kama unataka mafunuo zaidi okoka! Mkiri Yesu Kristo kuwa ni BWANA! Na alikufia msalabani ili akurudishe kwa Mungu kwasababu hapo ulipo umepotea