Hicho kitabu ukikiweka humu jukwaani unishtue....
Yesu ni 'Neno' la Mungu ila alifanyika mwili tu (yaani alivaa mwili wa kibinadamu).... huwezi kumtenganisha Mungu na 'Neno' lake maana hata Dunia iliumbwa kwa 'Neno'..
Yohana 1
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Hilo fungu la maandiko kutoka Yohana 1:1-4 limejieleza vizuri Sana.
Hili fungu jingine kutoka Yohana 17 limemueleza Yesu ni nani na ana mamlaka Gani ila ni vizuri kusoma Yohana 17 yote Ili uelewe vizuri zaidi.
Yohana 17
5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.
21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
Sina shaka na haya maandiko hayo,ninashaka na kile ninachokiita unbiblical doctrines.
Mleta mada anataka kujua Mungu wa biblia ni watatu ama mmoja.
1kor 8:6 "lakini kwetu sisi Mungu ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake; yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo".
Biblia inamtaja Mungu Baba na Yesu Kristo.Katika biblia nzima Yesu haitwi Mungu Baba bali Baba wa milele,Why Baba wa Milele na wakati si Mungu Baba.
1Waebrania 2:14-14
“Nipo hapa, na pamoja si wapo watoto
niliopewa na Mungu.”
14 Watoto hawa ni watu walio na miili ya damu na nyama".
So, Yesu ni Baba yetu kwa kupewa na Mungu ambaye ni Baba yake.
So,
mimi sipingi Yesu kuitwa Mungu,napiga Yesu kuitwa Mungu (nafsi) kitu ambacho kwenye biblia hakimo.
Yesu ni Mungu kwa asili na sio Mungu NAFSI.
Kumuita Yesu Mungu si Dhambi ni sahihi kwa maana amerithi Jina Baba yake so ana haki ya kutumia Jina ilo.
Ndiyo maana waliomjua Yesu ni nani walimuabudu.aliabudiwa na wanafunzI wake,watu na Malaika.
Mtoto wa Mungu ni Mungu ila huyo mtoto si Baba.
Kukazia maelezo yangu nimenukuu Quran As Zhukruf 83
Muhammad anasema" Say:
"If (Allah) Most Gracious had a son, I would be the first to worship."
Hapo Muhammad hasemi kuwa Mungu ana mwana ila anasema"kama Mungu angelikuwa na Mwana,yeye(Muhammad) angelikuwa wa kwanza kumuabudu mtoto huyo maana mtoto wa Mungu ni Mungu".
Sasa sisi katika Biblia Mungu ana mwana,na huyo mwana alifanyika mwili, so mkristo kumuabudu Yesu si dhambi,si dhambi maana ana uungu anauungu ndani yake japo si Mungu Baba.
Wafilipi 2:6
"Alikuwa sawa na Mungu katika namna zote,
lakini hakufikiri kwamba kuwa sawa na Mungu
kilikuwa kitu cha manufaa kwake"
Yesu alikuwa sawa na Mungu,kumbe kuna Mungu ambaye Yesu alikuwa nae sawa".
Sasa huyo Mungu ambaye Yesu alikuwa nae sawa ndiyo bibilia inamsema hakuna aliyewai wai muona na akaishi".
Yesu ametoka ndani ya Mungu(mzaliwa wa kwanza).
Sisi tumeumbwa(viumbe) na tumepewa nafasi ya kufanyika kuwa wana Mungu kupitia Yesu Kristo ila yesu ni mzaliwa wa Mungu,Yeye hafanyiki kuwa mwana wa Mungu bali yeye ni mzaliwa.
Yeye amekuwepo na Baba kabla ya Dunia na vitu vyote kuumbwa.
Yohana 17 :3."Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma".