Wakuu naomba mnieleweshe concept ya Mungu katika ukristo

Wakuu naomba mnieleweshe concept ya Mungu katika ukristo

Mungu nimmoja katika vyeo vitatu mungu mwana,roho mtakatifu,mungu baba......
Mungu baba....muweza wa vyote hana limiti.........
Mungu mwana.....kipenz cha mungu baba ndo kiumbe ambacho mungu baba amekipa mamlaka ya mbinguni na ulimwenguni........
Mungu roho mtakatifu........Mungu katika mawasiliano yaani communication ya mungu na viumbe vyake vyote alivyo viumba.....

Sasa umuelewi nini Mungu hana mshirika katika maamuz tu atakalo amua yeye na kuliwaza basi hufanyika pasipo kushirikisha kiumbe chochote cos yeye ni mkamilifu kupita ukamilifu ila anaserikali ambayo hupokea mapokeo yake na kuwasilisha kwa viumbe wengine...........
 
Naweza nikaingia kwenye ukristo mkuu lengo ni kujua msingi wa dini ya kikristo au nikosa?
Hakuna sehemu nimesema ni kosa. Nimeuliza lengo hasa ni lipi baada ya kujua huo msingi, umejibu unaweza kuingia kwenye ukristo.

Sasa kama kweli unataka kujua msingi, JF sio sehemu sahihi
-Hapa kila mtu anaandika anachoamini hata kama sio sahihi.
-Ukristo ni mmoja ila Wakristo wamegawanyika na kila mmoja ana ufunuo wake.
- Kama kweli lengo ni kujua msingi ili uingie, ni bora uwatafute wahusika kupitia makanisa yao, ufanye research kutokana na maelezo yao, then utapata jibu sahihi.

Nasema hivyo kwa sababu, kupitia hizo comments, nimeona majibu ya madhehebu haya
-Roman catholic
-Jehova witness
-Pentecost
- Na kuna imani mpya wanajiita kanisa la mungu halisi.
Wote nimeona wanakujibu ndio maana unaona majibu yao yanapingana.
 
Utatu mtakatifu ni Siri ambayo hapana mwanadamu atakaye kuja kujua kwa asilimia 100, isipokuwa Roho mtakatifu pekee. Trinity ni asili yake Mungu, ukiondoa mmoja hapana Mungu, asili yake ya utatu inajidhihirisha kwenye uumbaji wa mwanadamu ana miwili, nafasi na roho, vyote vinategemeana, ukitoa kimoja hapana mwanadamu. Hivyo basi kila nafasi ni Mungu na siyo Mungu wa tatu. Imekuwa Siri ksb nyingi, mojawapo ni muweze kumheshimu ksbu anakuwa haeleweki alivyo na ametoka wapi.
Mbona ni nyepesi mkuu. Roho mtakatifu ni roho wa Mungu na Yesu ni neno la Mungu. Simple. Hakuna kitu kigumu hapo. Yote yameelezwa vizuri Ila wanadamu hawataki kujifunza Mambo ya Mungu tangu zamani za kale
 
Mungu nimmoja katika vyeo vitatu mungu mwana,roho mtakatifu,mungu baba......
Mungu baba....muweza wa vyote hana limiti.........
Mungu mwana.....kipenz cha mungu baba ndo kiumbe ambacho mungu baba amekipa mamlaka ya mbinguni na ulimwenguni........
Mungu roho mtakatifu........Mungu katika mawasiliano yaani communication ya mungu na viumbe vyake vyote alivyo viumba.....

Sasa umuelewi nini Mungu hana mshirika katika maamuz tu atakalo amua yeye na kuliwaza basi hufanyika pasipo kushirikisha kiumbe chochote cos yeye ni mkamilifu kupita ukamilifu ila anaserikali ambayo hupokea mapokeo yake na kuwasilisha kwa viumbe wengine...........
Mkuu unanichanganya MUNGU ni huyo MUNGU Baba ambaye amempa Mungu mwana mamlaka au hivyo vyeo ni MUNGU pia?
 
Kuna kitabu nikikumbuka nitakutumia jina.
Kinasema " Jesus is God infinitely but not in personality.

Kusema Yesu ni Mungu,na roho wa Mungu ni Mungu na Baba ni Mungu automatically wanakuwa ni mungu 3 kitu ambacho kwenye biblia hakipo.
Hicho kitabu ukikiweka humu jukwaani unishtue....

Yesu ni 'Neno' la Mungu ila alifanyika mwili tu (yaani alivaa mwili wa kibinadamu).... huwezi kumtenganisha Mungu na 'Neno' lake maana hata Dunia iliumbwa kwa 'Neno'..

Yohana 1
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.

3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.

Hilo fungu la maandiko kutoka Yohana 1:1-4 limejieleza vizuri Sana.

Hili fungu jingine kutoka Yohana 17 limemueleza Yesu ni nani na ana mamlaka Gani ila ni vizuri kusoma Yohana 17 yote Ili uelewe vizuri zaidi.

Yohana 17
5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako.

21 Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.

22 Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja.
 
Hakuna sehemu nimesema ni kosa. Nimeuliza lengo hasa ni lipi baada ya kujua huo msingi, umejibu unaweza kuingia kwenye ukristo.

Sasa kama kweli unataka kujua msingi, JF sio sehemu sahihi
-Hapa kila mtu anaandika anachoamini hata kama sio sahihi.
-Ukristo ni mmoja ila Wakristo wamegawanyika na kila mmoja ana ufunuo wake.
- Kama kweli lengo ni kujua msingi ili uingie, ni bora uwatafute wahusika kupitia makanisa yao, ufanye research kutokana na maelezo yao, then utapata jibu sahihi.

Nasema hivyo kwa sababu, kupitia hizo comments, nimeona majibu ya madhehebu haya
-Roman catholic
-Jehova witness
-Pentecost
- Na kuna imani mpya wanajiita kanisa la mungu halisi.
Wote nimeona wanakujibu ndio maana unaona majibu yao yanapingana.
Sasa mkuu nitajuaje ukweli maana mimi nataka ukristo sitaki dhehebu nataka kujua mafundisho ya kristo kuhusu MUNGU
 
Mbona ni nyepesi mkuu. Roho mtakatifu ni roho wa Mungu na Yesu ni neno la Mungu. Simple. Hakuna kitu kigumu hapo. Yote yameelezwa vizuri Ila wanadamu hawataki kujifunza Mambo ya Mungu tangu zamani za kale
Sawa mkuu

Swali neno la MUNGU ni MUNGU pia au linabaki kuwa neno la MUNGU?
 
Sasa mkuu nitajuaje ukweli maana mimi nataka ukristo sitaki dhehebu nataka kujua mafundisho ya kristo kuhusu MUNGU
Rudia kusoma hiyo comment yangu, imetoa majibu.
Hakuna ukristo bila dhehebu. Ili uwe mkristo lazima uwe kwenye mlengo flani ndio maana na wewe unataka majibu ya hao wenye madhehebu yao ili upate msingi.
 
Mkuu, naomba nikuulize jambo kidogo.
Mtu amegawanyika katika sehemu kuu ngapi?
Najibu hili swali bila mlengo wa dini mkuu mimi naamini mtu amegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni mwili na roho mimi binafsi sioni tofauti ya nafsi na roho.
 
Mungu ni title ya office ya uungu wa Mungu,

Mungu ni office iliyojificha, imekuwa ikijitambulisha Kwa Majina tofauti tofauti kulingana na KAZI tofauti tofauti apendavyo,

AGANO la kale amekuwa akijitamulisha kama "BWANA", NIKO AMBAYE NIKO", "ADONAI", nk nk

Sifa kuu mojawapo ya Mungu, ni uwezo wa kuwa sehemu zote Kwa wakati mmoja,

Mungu pia ana uwezo wa kuvaa mwili wa na maumbo tofauti tofauti Sababu Yeye ni ROHO.

Yesu ndiye Mungu aliyekuja duniani kwa KAZI ya Ukombozi wa mwanadamu,

Mungu Roho mtakatifu, ni ROHO huyo huyo wa Yesu.

Mungu baba ni title pia ya Yesu akiwa Mbinguni katika KITI Cha enzi.

Mungu mwana ndiye pia Mungu Yesu katika mwili wa mwanadamu.

MUNGU ni MMOJA na YESU KRISTO YESHUA HAMASHIACH ndilo JINA lake.

Amen
 
Rudia kusoma hiyo comment yangu, imetoa majibu.
Hakuna ukristo bila dhehebu. Ili uwe mkristo lazima uwe kwenye mlengo flani ndio maana na wewe unataka majibu ya hao wenye madhehebu yao ili upate msingi.
Hakuna ukristo bila dhehebu kwa nini? Mi nafahamu kuna kweli na si kweli hivyo basi hata kuwe na madhehebu 100 basi moja ndio litakuwa la kweli, sasa mkuu hilo mimi ndio nataka mafundisho yake maana huo ndio utakuwa ukristo wenyewe OG
 
Nilichomaanisha huweza kuwa mkristo bila dhehebu.
Mfano hapa unataka watu wakujibu ili upate msingi sahihi, hao wanaokujibu wako kwenye madhehebu yao. Utakaekubali majibu yake maana yake unakubaliana na dhehebu lake lililomfundisha hayo. Umenielewa?
 
Najibu hili swali bila mlengo wa dini mkuu mimi naamini mtu amegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni mwili na roho mimi binafsi sioni tofauti ya nafsi na roho.
Nafsi ni ile sehemu ambayo ina ufahamu wamtu mwenyewe au kiini cha ubinafsi wa mtu. Kazi yake ni:
- Kufikiri – Kutafakari, kuona
-Hisia – Kujisikia kuwa na tamaa na Upendo
-Utashi – Nia, Kuamua.

Roho ni ile sehemu ya mtu yenye ufahamu wa Mungu, ambayo hufanywa hai na hutiwa nguvu na Roho wa Mungu wakati wa Wokovu. Kabla ya mtu Kuokoka, sehemu hii, haifanyi kazi kwa utimilifu kabisa kwa sababu ya dhambi. Dhambi huifanya kuondolewa nguvu ya kutenda kazi sawa sawa, kwa Amani na Roho ya Mungu. Lakini kupitia Ubatizo wa Roho Mtakatifu, mwanadamu hupokea nguvu ya kiroho, inayomwezesha kuishi maisha ya Kristo. Roho inahusika na:-
-Maombi na Ibada na Mungu,-Ushirika na Mungu, -Mapokezi ya karama za Roho,
-Vita vya kiroho,-Kuunda Mawazo na Ndoto,-Dhamira, Kupambanua,-Udadisi, Kuuliza,-Ufahamu, Kutafsiri.
 
Utatu mtakatifu ni Siri ambayo hapana mwanadamu atakaye kuja kujua kwa asilimia 100, isipokuwa Roho mtakatifu pekee. Trinity ni asili yake Mungu, ukiondoa mmoja hapana Mungu, asili yake ya utatu inajidhihirisha kwenye uumbaji wa mwanadamu ana miwili, nafasi na roho, vyote vinategemeana, ukitoa kimoja hapana mwanadamu. Hivyo basi kila nafasi ni Mungu na siyo Mungu wa tatu. Imekuwa Siri ksb nyingi, mojawapo ni muweze kumheshimu ksbu anakuwa haeleweki alivyo na ametoka wapi.
Hebu nisaidie kuelewa hizi concepts,

1. Yesu kabla ya kuzaliwa alikuaje? na sasa ambapo amekaa kwenye kiti cha enzi upande wa kulia wa Mungu baba yupo katika umbile gani?
2. Kwa kitendo cha kukaa upande wa kulia mi ninavyoelewa ni kwamba kimoja lazima kiwe na mwisho kwa pande zote mbili i.e. kulia na kusho hence mwengine afuate baada ya yule wa kwanza katika upande huo.

Sasa how do u reconcile the concept of one God na hii narration inayoonyesha wazi kuwa Yesu yupo upande maalumu kutoka pale alipo Mungu baba? Kuna miungu wangapi hapo? surely one cannot say "Mimi nimekaa upande wa kulia wa mwili wangu"
 
Back
Top Bottom