Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Ukisema Yesu ni Mungu sawa! Roho mtakatifu ni Mungu sawa! Mungu Baba ni Mungu sawa!Ambaye ni YESU?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukisema Yesu ni Mungu sawa! Roho mtakatifu ni Mungu sawa! Mungu Baba ni Mungu sawa!Ambaye ni YESU?
Unajua maana ya neno "mukutadha" au kwa kingereza "context"! Vinginevyo pole!Wakristo hapo ndipo tunapofeli tunafundisha kinyume na Biblia
Biblia inasema wazi Mungu ni mmoja tu hizi mambo za nafsi 3 tunadanganya sana
Na Yesu sio MUNGU
1 Wakorintho 11:3
Neno: Bibilia Takatifu
3 Lakini napenda muelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo
Kwa msingi wa andiko hilo kama Yesu ni sawa na Mungu basi tukubaliane pia mke ni sawa na mume
kwa nini muna muomba sana YESU?Ukisema Yesu ni Mungu sawa! Roho mtakatifu ni Mungu sawa! Mungu Baba ni Mungu sawa!
Wewe hapa hautumii akili ?Wote wako sawa! Huwezi kuwatenganisha! Hata wewe unaweza tenganisha roho, mwili na nafsi? Inaweza kusadikika kuwa roho ina nguvu lakini anayeipa fursa roho ni akili iliyo ndani ya nafsi! Na akili hiko ndani ya ubongo ulio ndani ya mwili!
Haya mambo ukitumia akili za kibinadamu huwezi kuelewa!
Tuonyeshe muktadha wa hilo andikoUnajua maana ya neno "mukutadha" au kwa kingereza "context"! Vinginevyo pole!
Hana nafsi wala yeye ni Moyo ndo maana ametusisitiza kulinda Moyo.sio moyo unaoenda kupasuliwa india.Muumba ni mmoja mwenye nafsi ngapi? Moja au tatu?
Kwa hiyo wapo watatu na sio mmoja tena ?Ukisema Yesu ni Mungu sawa! Roho mtakatifu ni Mungu sawa! Mungu Baba ni Mungu sawa!
Hii nayo ni concept mpya mkuuHana nafsi wala yeye ni Moyo ndo maana ametusisitiza kulinda Moyo.sio moyo unaoenda kupasuliwa india.
Mathayo 5:8
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
Mithali 4:23
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Mi mkuu ndio wamezidi kunichanganya maana sijapata jibu na nilitegemea a straight answerWao wenyewe hawana wanacho elewa.
Mungu ni mmoja ambae ni YESU, ROHO au ROHO MTAKATIFU?Hiyo namba 2 ndiyo sahihi mkuu
Mungu ni mmoja tu
Nina shida kidogo na ongea yangu na andika yangu.. uwa ninaongea na kuandika kimamlaka zaidi ndiyo maana mtu asiyenijua anaweza hisi nafoka kumbe sio.Mbona unaongea kwa mihemko na hasira? Nitakuonyesha maandiko ambapo Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho mtakatifu walikuwa pamoja kwa wakati mmoja na kujidhihirisha:
Mathayo 3:16-17
[16]Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;
[17]na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Sasa hapa unaona:
1. Yesu aliyetoka kubatizwa
2. Roho mtakatifu akishuka kama hua
3. Mungu Baba (katika sauti) kutoka Mbinguni
Mambo ya Mungu hayataki jaziba! Okoka!
Wewe ni mkristo?Mungu hajawahi kuwepo, Hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Mungu ni dhana ya kufikirika tu.
Mimi ni infropreneur.Wewe ni mkristo?
Wakristo pangueni hii hoja fikirishiNina shida kidogo na ongea yangu na andika yangu.. uwa ninaongea na kuandika kimamlaka zaidi ndiyo maana mtu asiyenijua anaweza hisi nafoka kumbe sio.
Nichukulie poa.
Chief,hizo verse ulizotoa hazimsemi Yesu kama ulivyoeleza hapo juu.
Yesu ni mwana wa Mungu hivyo ana uungu. kuna verse nimeisahu Mungu anamuita Yesu Mungu lakini hiyo haina maana kuwa Yesu ndiye yule Mung ambaye biblia inamsema hakuna aliyewai muona akaishi.
Maisha yake yote hapa Duniani yesu alisema Yeye ni mwana wa Mungu na ilo likafanya wayahudi wakataka kumpiga.
Katika biblia tuna Mungu Baba,mwanae Yesu Kristo na Roho wa Mungu.
Roho wa Mungu si Mungu nafsi.
Yesu Kristo si Mungu nafsi.
1Petro 3:22
"ambaye alikwenda mbinguni na sasa amekaa upande wa kulia wa Mungu, anatawala juu ya malaika, wakuu na wenye enzi".
Yesu amakee upande wa kulia wa Mungu,sasa kwanini wewe useme Yesu ni Mungu?.
Kuna kitabu nikikumbuka nitakutumia jina.
Kinasema " Jesus is God infinitely but not in personality.
Kusema Yesu ni Mungu,na roho wa Mungu ni Mungu na Baba ni Mungu automatically wanakuwa ni mungu 3 kitu ambacho kwenye biblia hakipo.
Tuelezee the concept of God in ChristianityMimi ni infropreneur.