MUNGU HANA NAFSI TATU
Leo watu wanapotea kutokana na mapokeo waliyokuta katika madhehebu yao mfano karika suala hili la ''Utatu'' yaani MUNGU kuwa na nafsi tatu sasa tuangalie kulingana na Biblia inasemaje?;
1)MUNGU anasema ana nafsi moja Isaya 45:21-23
[21]Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonyesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.
[22]Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.
[23]Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
Unaona katika mstari wa 23 MUNGU mwenyewe anasema ana nafsi moja.
Pia tuone andiko jengine Waebrania 6:13-14
[13]Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,
[14]akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza.
Vile vile unaweza kusoma maandiko mengine kuthibitisha
Zaburi 11:5
[5]BWANA humjaribu mwenye haki;
Bali nafsi yake humchukia asiye haki,
Na mwenye kupenda udhalimu.
Maandiko yapo mengi zaidi ya hayo yanayothibitisha kuwa Mungu ana nafsi moja tu .
Sasa acha kwa ufupi tuone nafsi nini kulingana na Biblia ;
Nafsi kwa namna ya kuelewa kirahisi ni Mtu mwenyewe Mwanzo 2:7
[7]BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Sasa tunaweza kusema mfano kuna watu wawili maana yake ni nafsi mbili yaani watu wawili Mwanzo 46:15
[15]Hao ndio wana wa Lea, aliomzalia Yakobo katika Padan-aramu, na Dina, binti yake. Nafsi zote za wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu.
Kutoka 1:5
[5]Na nafsi zile zote zilizotoka viunoni mwa Yakobo zilikuwa ni nafsi sabini; na huyo Yusufu alikuwa huko ndani ya Misri tangu hapo. Unaona katika maandiko badala ya kusema watu inasema ''Nafsi'' maana vyote ni sawa na ndio maana sisi tumeumbwa kwa mfano wa MUNGU yeye ana nafsi moja na sisi tuna nafsi moja.
KWA HITIMISHO ;Huyo MUNGU Mwenye nafsi moja si mwingine bali ni BWANA YESU KRISTO Tito 2:13-14
[13]tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
[14]ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
NB Ndugu zangu leo hii madhehebu ndio njia shetani anatumia kuwapoteza watu mapokeo hayaokoi bali ni Neno la MUNGU la kweli lisilo pita.