Wakuu, nishaurini kuhusu Shule ya bweni kwa mtoto wa nursery

Huyo mkewe hajielewi na ukute hakusoma boarding
 
Yesuu..papai langu nitahangaika nalo hata iwe vipi..siwezi peleka boarding mtoto katika umri huo.
Mpendwa sikushauri tafuta tu namna nyingine ila usijaribu kuweka rehani maisha ya mtoto wako .
Bora kabisaa nihangaike nalo mwenyewe... Na kama ni kuoza liniozee mwenyewe... Siyo kufanya huo upuuzi wa kupeleka mtoto wa NASARE bodingiiiii... Binafsi nauita wehu na kukimbia majukumu
 
Mtu kashasema hana option nyie bado mnampa ushaur mbuzi kwan watoto woooooote wanaosoma boarding wameharibika? Je Hakuna watoto mnaoishi nao majumbani mwenu wameharibika achen izo buana [emoji51][emoji51]
Mbona wewe hujaitaja hiyo shule..? Mshauri wewe... USIDHANI KISA KAOMBA USHAURI BASI TUMWAMBIE TU..!!! INATEGEMEA ANATAKA USHAURI WA KITU GANI...

Nijibu hili,.... Mtu akija kukuomba ushauri wa nini afanye ili aweze kum'baka au kumuua binti yako utampa..!!???
 
Lipi ni jema sasa mkuu, apate elimu hii ya jua kali ili kulinda ukaribu wa mzazi na mtoto na malezi bora au aende akapate elimu itakayonjenga vizuri kuyakabili mazingira yake.
Wengi wetu tumesoma kidumu na mfagio chini ya uangalizi wa wazazi na maisha yanaendelea

Unaamini hatatoboa maisha sababu amesoma kidumu na mfagio?
 
Lipi ni jema sasa mkuu, apate elimu hii ya jua kali ili kulinda ukaribu wa mzazi na mtoto na malezi bora au aende akapate elimu itakayonjenga vizuri kuyakabili mazingira yake.
Hapo kwenye kuyakabili maisha yake, ungemalizia na madhara yake... usiwe biased wa upande mmoja unataja udhaifu na upande mwingine unataja strength....!!!!
 
Kabisa yani. Watu tumesoma kidumu na mfagio tokea nursery hadi university. Sasa kama mzazi hufatilii maendeleo ya mwanao unatagemea mwalimu peke ake ndio afanye kazi hawezi kutoboa kidumu na mfagio. Kwangu mimi bora avuke barabara aende kidumu na mfagio kuliko kupeleka boarding mtoto wa 4 sijui 4 yrs
 
Badala ya kumlea mtoto umeamua kumdhamini.

Malipo yake hayapo mbali
 
Na kuni...
 
Wazungu huwa wanapeleka wa kwao boarding?
 
Kama hakuna option nyingine bora umpeleke kidumu na fagio mbona sisi tulisoma huko na saivi tuko vizuri tu.

Kumpeleka mtoto mdogo boarding ni kumnyima haki yake ya kupata malezi kutoka kwa wazazi na kupata ile Bond. Baadae mtoto anawaona wazazi Kama wageni kwake sababu hakuwa na ile Bond Toka akiwa mdogo.

Unamuamini vipi matron na mwalimu kumpa malezi Bora mtoto wako, wakati Kuna Watoto zaidi hata ya Mia nao wanataka unangalizi. Jamani hapo tunawapa Watoto wetu Emotional torture mtoto anakuwa mpweke na hajui Nani wa kumsaidia

Natamani hata Sheria itungwe marufuku Watoto wa shule ya msingi kupelekwa boarding. Boarding ianzie secondary
 
Wengi wetu tumesoma kidumu na mfagio chini ya uangalizi wa wazazi na maisha yanaendelea

Unaamini hatatoboa maisha sababu amesoma kidumu na mfagio?
Mkuu nina hisia kwamba kizazi kinachokuja baada ya kizazi chetu kitakuwa dominated na vijana wenye ufahamu mkubwa wa mambo, uwezo mzuri wa kujieleza na kujiamini, ambao wengi hawaandaliwi ktk shule zetu hizi.
 
Shule za boarding zina maisha ya upweke sana haijalishi ni ya garama kiasi gani. Mnaenda kutengeneza watoto wasiowez kucommunicate matatizo yao kwa wazazi. Shule za boarding zina bullying za kutosha na unaweza kuta mtoto hawezi sema hata kwa mwalimu bora za kwenda na kurudi akirudi nyumbani mzazi utaweza fatilia.
Na kwa Tanzania hii sasa hivi hamna mkoa utakosa shule inayofundisha hiko kingereza mnachotaka karibu na wewe angalau kwa umbali wa kwenda na school bus.
 
Mleeni binti yenu wenyewe,huko boarding ataenda kubakwa na kuliwa jicho very soon.
Acheni uvivu wa kujifanya mko bize.
 
Mkuu nina hisia kwamba kizazi kinachokuja baada ya kizazi chetu kitakuwa dominated na vijana wenye ufahamu mkubwa wa mambo, uwezo mzuri wa kujieleza na kujiamini, ambao wengi hawaandaliwi ktk shule zetu hizi.
Mkuu ufahamu mkubwa ambao Watoto wa English medium wanao ni kujua lugha ya kiingereza sababu ndio teaching language, that's the only difference na watoto wa kayumba. Sababu syllabus wanayoifuta inatolewa na serikali same na shule za kawaida. Labda umpeleke Cambridge.

Na kitu ambacho jamii haijui Watoto wa shule za kayumba wanafundishwa na walimu qualified kushinda English medium. Mwalimu wa kayumba anatakiwa apate division 4 kuanzia points 27, wakati mwalimu wa English medium yeye hata division sifuri chuoni Cha mafunzo yao wanapokelewa.
 
Mwanangu nilimgomea asomee sehemu za mijini sembuse boarding?[emoji1783]

Yani nilimwambia mama ake wazi kabisa tusifosiane malezi, lete kijana hapa kijijini ajifunze maisha, ajue kushika na jembe, ajue kushika na fimbo akachunge, ajue na lugha ya mababu zake.

Juzi wamefanya mtihani na kameshika nafasi ya 3, na kanayafurahia maisha sana.

Naamini kangekuwa mjini ingekuwa viceversa, kwanza michezo mingi na utukutu wa hapa na pale.

Mwanao kaa naye mpaka atakapomaliza la saba, na mpeleke shule za kawaida ili umuassess intelligent capacity yake. Kama anaperform vzr basi shukuru Mungu maana hautatumia nguvu nyingi kumsupport. Kama ni mzito sasa ndio unaandaa mipango ya kumboost akifika secondary ikiwemo kumtafutia shule nzuri aachane na hizi za kata.
 
Mkuu nina hisia kwamba kizazi kinachokuja baada ya kizazi chetu kitakuwa dominated na vijana wenye ufahamu mkubwa wa mambo, uwezo mzuri wa kujieleza na kujiamini, ambao wengi hawaandaliwi ktk shule zetu hizi.
Muandae wewe mtoto, unaweza kupeleka huko na asiwe na huo uwezo wa kujiamini!

Mjengee uwezo wewe kama mzazi, mtoto atakuwa vizuri. Usitegemee walimu wawe wazazi wa mwanao! Wakujengea matarajio na matamanio ya mtoto wako.
Psychological trauma ya separation, anxiety utakapomuacha bila yeye kuwa na uelewa wa kwanini mmemuacha utamuelezaje??

ZINDUKA LEA MWANAO!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mkuu nina hisia kwamba kizazi kinachokuja baada ya kizazi chetu kitakuwa dominated na vijana wenye ufahamu mkubwa wa mambo, uwezo mzuri wa kujieleza na kujiamini, ambao wengi hawaandaliwi ktk shule zetu hizi.
Mpeleke basi boarding

Si ni wa kwako.
 
Wazazi vilaza wakishagundua wote ni vilaza wanajua lazima tu watazaa kilaza

Sasa wakishaazaa ili kuforce king wanataka wapeleke mtoto shule za kizungu wakiamini ni bora

Kama shida ni kizungu mtoto bright anaweza kusoma kayumba na akakijulia University
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…