Wakuu tuwe makini lock milango kabla ya kuanza kuendesha gari

Wakuu tuwe makini lock milango kabla ya kuanza kuendesha gari

Sijawahi kua na amani wala kuvumilia pale ninapoongozana na gari inayoendeshwa na mwanamke. Lazima nimkate au nipaki tu nimuache aende. Na sijawahi kurndesha na mwanamke zaidi ya umbali wa 20km. Siwaamini kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Wanambo mengi Hawa focus.
 
Mbona gari ikifika 25kph hivi inajilock yenyewe milango, na huyo dereva kama mlango haujafungwa haoni warning light kwenye dashboard?.
Sio gari zote mkuu. Probox na nduguze hata ufike 180 kama haujalock manually itaendelea kuwa wazi. Na wanawake huwa hawazingatii dashboard signs
 
Hapo angekuwa dereva mwanaume angeshambuliwa kwa maneno makali pengine kipigo na kulala selo. Ila kwakuwa ni mwanamke, eti nguvu za kusimama kakosa. Yeye na mtoto nani aliyeumia hata ashindwe kusimama? Aliyedondoka na kugongwa kasimama na kuzungukazunguka, aliyedondosha akakosa nguvu za kusimama.
Hakika Mkuu alipata mshituko wa hatari anasema naomba mnambie mwanangu Kama yupo salama nitakufa mimi .
 
Ni ujumbe mzuri unaoelimisha ila hiyo ya kua hiyo imetokea kwenye safari zako umetupiga mkulungwa.

Hiyo clip ipo ni ya muda mrefu.
 
Habari wana JF.

Leo nikiwa kwenye safari zangu mjini Dar es salaam Kuna gari ilikuwa inazunguka round-about, ghafla mlango wa nyuma ulifunguka na akadondoka mtoto umri kama miaka 4 hivi.

Na dereva aliyekuwa anaendesha hilo gari hajajua kwamba mtoto kadondoka, Kwa nyuma pia kulikuwa kuna gari nyingine inakuja ikamgonga mtoto kwakumpush na kufunga break haraka maana alikuwa hajamuona mtoto.

Yule mtoto akasimama amechanganyikiwa analia anazunguka zunguka. Kuna bodaboda akalikimbiza lile gari alilotoka yule mtoto na kumsimamisha. Dereva alikuwa ni Mdada boda akamwambia umemdondosha mtoto nyuma pale Mdada anashangaa.

Boda akamwambia unaendesha gari hauku lock milango wakati unaendesha mtoto kachomoka nje Dada kaanza kupiga kelele kilio kizito hata kusimama hawezi.

Wakuu tuwe makini lock milango kabla ya kuanza kuendesha gari. Ukiwa na watoto makinika zaidi sio unachezea simu tu.

Na hii ni Kwa wote wewe uliye na gari hata wewe usiye na gari kwasasa ukija kuwa nalo hapo mbeleni kumbuka hilo lock milango punguza kuchezea simu.
Story ya kutunga hii uongo mtupu
 
Aise ndio ninachoipendea JF umetoa angalizo zuri sana ahsante.
Mimi nina mtoto ambaye ana tatizo la akili kidogo japo ukimuona huwezi amini
Siku moja akaniambia baba kuna wakati natamani nifungue gari niruke nife mimi naona sina faida dunia hii.
Toka siku hiyo nikiwa naye siachi ku lock milango hata dereva wangu nimempa hilo angalizo
 
Aise ndio ninachoipendea JF umetoa angalizo zuri sana ahsante.
Mimi nina mtoto ambaye ana tatizo la akili kidogo japo ukimuona huwezi amini
Siku moja akaniambia baba kuna wakati natamani nifungue gari niruke nife mimi naona sina faida dunia hii.
Toka siku hiyo nikiwa naye siachi ku lock milango hata dereva wangu nimempa hilo angalizo
Hongera Sana Mkuu Kwa kuwa makini watoto hawatulii ndani ya gari.
 
Back
Top Bottom