Kuna wazazi ni wazembe sana hasa wa kike,
Jana nimesikia habari Tabora mtoto wa miaka mi3 kafariki Kwa kutumbukia kisimani wakati huo mama yake yupo ndani na mishe zingine, unajua una kisima na mtoto mdogo kwann usikifunike? yaani wamama wengi ni MAJANGA uwezo wao wa kunusa hatar ni mdogo mno.
Juzi kati nimesafiri kutoka Dar kuja Mwanza Kwa bus jirani yangu amekaa na mtoto siti ya mbele dogo ( miaka kama 4) amesimama kwenye mapaja ya mama yake Kila mara anachungulia nje mama hana habari anaona kawaida tu nimemshtua mara 2 kwamba amzuia dogo ni hatar ila annapuuza na mm mwisho nikamwacha sasa lingempata tukio dogo ungekuta mama anaanza kupiga mayowe, ovyo kabisa wazazi wengine.