Wakuu wa mikoa hatujawapeleka huko kuwa wafalme bali kuwa watumishi wa wananchi - Rais Samia

Wakuu wa mikoa hatujawapeleka huko kuwa wafalme bali kuwa watumishi wa wananchi - Rais Samia

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi waliopishwa hususan Wakuu wa Mikoa kwenda kutekeleza majukumu yao kwa kujiamini na kuchukulia dhamana waliyopewa kama wajibu wa kusimamia shughuli zote za Serikali katika maeneo yao.

Rais Samia amesema hayo leo Jumatano, Septemba 2, 2026, Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, mara baada ya kuwaapisha viongozi wateule.

Amesema uteuzi wao ni ishara ya imani kubwa waliyopewa na Serikali, hivyo wanapaswa kutumia nafasi hizo kuhakikisha matatizo ya wananchi katika maeneo yao yanapatiwa ufumbuzi.

“Kikatiba Rais amekasimu madaraka yake katika eneo lililokatwa linaloitwa Mkoa. Nawe Mkuu wa Mkoa jichukulie kama ndio Rais wa eneo lile, kwamba yote yanayokuja kwa Rais katika eneo hilo, ni ya kwako,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia amewakumbusha viongozi hao kuwa dhamana waliyopewa si ya kuwa wafalme wa maeneo wanayoyaongoza, bali ni ya kuwa watumishi wa wananchi.

“Hatujawapeleka kuwa wafalme wa maeneo hayo, bali kuwa watumishi wa kutumikia watu,” amesema.

Amesema Mkuu wa Mkoa anapaswa kuona mkoa anaouongoza na watu wake kama sehemu ya wajibu wake mkubwa, akisisitiza kuwa changamoto zinazowakabili wananchi zinapaswa kuchukuliwa kama changamoto za kiongozi mwenyewe.

“Nendeni mkachape miguu kwelikweli katika kuwatumikia wananchi, matatizo ya mkoa ni ya kwenu,” amesisitiza Rais Samia.

Rais Samia amewataka viongozi hao kutekeleza majukumu yao kwa uzalendo, uwajibikaji na kujali maslahi ya wananchi.
 
Back
Top Bottom