Wale ambao hatuna Mpango wa kuoa tuendelee kupeana Mbinu za Maisha

Wale ambao hatuna Mpango wa kuoa tuendelee kupeana Mbinu za Maisha

Hao mbona nimesema hapo kwamba walifanya kosa la kiufundi. Usifanye masikhara pesa kwa mwanaume ni kila kitu. Utatekeleza vipi majukumu yako ya msingi kama kiongozi wa familia bila pesa?

Tena ukiwa mzee pesa ndio muhimu zaidi. Mwanaume haupaswi kuweka rehani kwa watoto wako siku zote hakikisha unapoihudumia familia una-backup financial plan incase mke wako akihamia kwa watoto wake uzeeni.
Ndio mjipange
 
Ukifa peke yako geto kuna utofauti gan na ambaye hajafa peke ake geto? Wote si mnaenda kuoza au???
Utofauti ni mkubwa mno. Mkiwa wawili hadi ufe utakuwa umeshafanyiwa taratibu za matibabu. Mpengine upone. Peke yako unazima tu kama mshumaa
 
Duh! Umeandika nini hapa? Wewe utakuwa mwanamke.

Vitu pekee vinavyosimama na mwanaume mpaka kaburini ni Mungu na pesa yake tu. Hivyo vingine havina guarantee. Usije ukafanya kosa la kiufundi kama mwanaume uanze kuwa unasumbua wanao na simu za vizinga ukifika miaka 60.
[emoji1787][emoji1787]
 
Maliza kwanza chuo, uje uraiani kupata true taste of life. Mkikaa kwenye hayo ma group yenu ya vijana mnaishia kulishana habari za kufikirika.

Wote mnaopinga kuoa mnatumia mifano ya watu ambao hawapo kwenye jamii inayowazunguka, maana yake mmekosa mifano hai kutoka kwenye your immediate surrounding, sasa sijui hamjagundua kwamba mna tatizo sehemu au mmeamua kujizima data.
Dangote,mike adenuga,chief adeleke, prince Ned nwoko(ndoa ya mkataba na wake 6 no assets will be lost in divorce) hao ni Nigeria ambayo ni Africa haya bongo (mondi,Fred vunjabei,Rostam) hio ni bongo haya worldwide (Elon musk,bezos,bill gates,) bado unapinga na wengine shida si famous hata nikikutajia huta wajua #Kaa CHONJO#
 
Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuleta uzi hapa ni jinsi gani ndoa ni scam, ni jinsi gani ndoa iko pale kumnufaisha Mwanamke.

Siku za karibuni kumezuka matukio kadhaa ya mauaji ya wanandoa, au wanandoa kujiua sababu kubwa ikiwa mifarakano ya ndani ya ndoa.

Kwa Muktadha huo nazidi kushikilia ule msimamo wangu ya kwamba Maisha ya Mwanaume ili yawe Marefu kwa zama hizi aachana na hizi ndoa. Hutoua/Kuuawa/Kujiua.

Je wale wenzangu Lifetime Bachelors tupeane Mbinu zipi katika maisha yetu ya ubachela?

Uzi tayari!

cc: Liverpool VPN
Kwa kweli mimi hapo nimeishavuka maana nimeishaoa na watoto ninao
nimelazimika kuandika maana nina watoto na kwa kuwa jf tunatumia fake ID
huenda aliyeandika ni mwanangu hivyo nimelazimika kushauri yafuatayo:

1. Baba yako au mama yako wangeogopa ndoa kwa misingi hiyo huenda usingezaliwa au ungezaliwa na single mother,usingesaidiwa hadi uwe na ufahamu wa kutumia kompyuta au simu
2. Wasiooa,wasiokuwa na wake zao hawana tofauti na wanyama mfano mzuri ni mbuzi
anafanya mapenzi mara nyingi na ndevu anazo lakini hana familia.
3. Maisha ya wanandoa yapo kila siku ila hivyo visa vya kujiua kuuawa kwa sababu ya ndoa ni nadra kivisikia ukilinganisha na wingi wa wanandoa ulimwenguni kote.
4. Waliopo kwenye mahusiano bila ndoa,wapo kwenye risk kubwa ya kuumizana kimapenzi kuliko waliopo kwenye ndoa

Naomba niishie hapa,mimi binafsi sijawahi kujuta kwanini nilioa.
 
Asante familia hutengenezwa tokea kwenye mzizi ukitengeneza familia yako vizuri watoto wako hawatakutupa au mkeo
Vijana siku hizi wanaogopa majukum na kulea familia
majukumu ya kulea familia hayaogopwi mkuu, wanawake wa wakati huu na wa zamani tofauti, wasasa wamezidi wana gharama sana, Unakuta mwanamke anataka atoke droo na Mke wa Cristiano wa portugal wakati mumewe ni hohehahe mwisho wa siku mwanaume lazima akimbie majukumu.... Kuliko upigane ukang'ata bora ukimbie, na kama ukiona game huiwezi basi usikunje ngumi, Woga kwa vijana unasababishwa na mabinti wa sasa.
 
Kuna kiburi Cha uhai na kiburi Cha kuwa na afya Ila Mungu alijua wapi atukamatie utaruka ruka wee hujui ni kuanzia miak 27 au 30 au 60 afyayako itakuwa haieleweki na hizo pesa hujui utakuwa umepata au lah
Kwahiyo mwanaume akiwa na mke nakuwa na guarantee ya kuyaepuka yote hayo?

Yani mke ana play part ipi haswa katika kuyaepusha?
 
Kwahiyo mwanaume akiwa na mke nakuwa na guarantee ya kuyaepuka yote hayo?

Yani mke ana play part ipi haswa katika kuyaepusha?
Sijasema mwanamke anazuia hayo ila kunawakat inabidi tusione kupumua ni kitu Cha kutupa kiburi sana au tukajiona magenius sana

Offcourse faida za ndoa zinaeleweka na zipo kilichobadilika ni hiz nyakt tulizonazo na lifestyle ila maana ya ndoa na malengo ya ndoa hayajabadilika na haiwez badilika tunajitoa tu ufahamu

Sabbu ya watu kuuana Haina mashiko kupinga ndoa Kwan watu wanagongwa na magar na wanakufa mbona hatuachi kutembea barabarani tukakaa tu ndani tuepuke kufa
 
Kuoa au kuolewa ni maamuzi ya mtu binafsi, watu wasitishane. Mbona mapadre na masista hawaoi wala kuolewa na hatuwaoni wakiteseka huko uzeeni?.

Ukiishi maisha ya ubachela ishi kwa nidhamu na mikakati. Jiunge na mrengo kwenye dini yako, jiunge club moja wapo unayoishi msimamo wao, fanya kazi au biashara zako vizuri. Kusanya utajiri na uutumie huo utajiri.

Kama una mtoto au watoto wape elimu nzuri, pia tafuta vijana kadhaa wanaotoka familia masikini ila wana hari na elimu kisha wapige sapoti kama wanao, hao ndio hadhina yako huko uzeeni.

Sasa watu wanadhani tukiamua kuishi maisha ya ubachela basi ni wasela wasela, ubachela hadi dini zipo zinazouelewa na kuufanya ngazi ya kiimani.

Kuwa bachela, fanya wajibu wako kwa Mungu na jamii. Utaishi kwa furaha sana.
 
majukumu ya kulea familia hayaogopwi mkuu, wanawake wa wakati huu na wa zamani tofauti, wasasa wamezidi wana gharama sana, Unakuta mwanamke anataka atoke droo na Mke wa Cristiano wa portugal wakati mumewe ni hohehahe mwisho wa siku mwanaume lazima akimbie majukumu.... Kuliko upigane ukang'ata bora ukimbie, na kama ukiona game huiwezi basi usikunje ngumi, Woga kwa vijana unasababishwa na mabinti wa sasa.
Well said
 
Back
Top Bottom