Wale ambao hatuna Mpango wa kuoa tuendelee kupeana Mbinu za Maisha

Ndio mjipange
 
Ukifa peke yako geto kuna utofauti gan na ambaye hajafa peke ake geto? Wote si mnaenda kuoza au???
Utofauti ni mkubwa mno. Mkiwa wawili hadi ufe utakuwa umeshafanyiwa taratibu za matibabu. Mpengine upone. Peke yako unazima tu kama mshumaa
 
[emoji1787][emoji1787]
 
Dangote,mike adenuga,chief adeleke, prince Ned nwoko(ndoa ya mkataba na wake 6 no assets will be lost in divorce) hao ni Nigeria ambayo ni Africa haya bongo (mondi,Fred vunjabei,Rostam) hio ni bongo haya worldwide (Elon musk,bezos,bill gates,) bado unapinga na wengine shida si famous hata nikikutajia huta wajua #Kaa CHONJO#
 
Kwa kweli mimi hapo nimeishavuka maana nimeishaoa na watoto ninao
nimelazimika kuandika maana nina watoto na kwa kuwa jf tunatumia fake ID
huenda aliyeandika ni mwanangu hivyo nimelazimika kushauri yafuatayo:

1. Baba yako au mama yako wangeogopa ndoa kwa misingi hiyo huenda usingezaliwa au ungezaliwa na single mother,usingesaidiwa hadi uwe na ufahamu wa kutumia kompyuta au simu
2. Wasiooa,wasiokuwa na wake zao hawana tofauti na wanyama mfano mzuri ni mbuzi
anafanya mapenzi mara nyingi na ndevu anazo lakini hana familia.
3. Maisha ya wanandoa yapo kila siku ila hivyo visa vya kujiua kuuawa kwa sababu ya ndoa ni nadra kivisikia ukilinganisha na wingi wa wanandoa ulimwenguni kote.
4. Waliopo kwenye mahusiano bila ndoa,wapo kwenye risk kubwa ya kuumizana kimapenzi kuliko waliopo kwenye ndoa

Naomba niishie hapa,mimi binafsi sijawahi kujuta kwanini nilioa.
 
Asante familia hutengenezwa tokea kwenye mzizi ukitengeneza familia yako vizuri watoto wako hawatakutupa au mkeo
Vijana siku hizi wanaogopa majukum na kulea familia
majukumu ya kulea familia hayaogopwi mkuu, wanawake wa wakati huu na wa zamani tofauti, wasasa wamezidi wana gharama sana, Unakuta mwanamke anataka atoke droo na Mke wa Cristiano wa portugal wakati mumewe ni hohehahe mwisho wa siku mwanaume lazima akimbie majukumu.... Kuliko upigane ukang'ata bora ukimbie, na kama ukiona game huiwezi basi usikunje ngumi, Woga kwa vijana unasababishwa na mabinti wa sasa.
 
Kuna kiburi Cha uhai na kiburi Cha kuwa na afya Ila Mungu alijua wapi atukamatie utaruka ruka wee hujui ni kuanzia miak 27 au 30 au 60 afyayako itakuwa haieleweki na hizo pesa hujui utakuwa umepata au lah
Kwahiyo mwanaume akiwa na mke nakuwa na guarantee ya kuyaepuka yote hayo?

Yani mke ana play part ipi haswa katika kuyaepusha?
 
Kwahiyo mwanaume akiwa na mke nakuwa na guarantee ya kuyaepuka yote hayo?

Yani mke ana play part ipi haswa katika kuyaepusha?
Sijasema mwanamke anazuia hayo ila kunawakat inabidi tusione kupumua ni kitu Cha kutupa kiburi sana au tukajiona magenius sana

Offcourse faida za ndoa zinaeleweka na zipo kilichobadilika ni hiz nyakt tulizonazo na lifestyle ila maana ya ndoa na malengo ya ndoa hayajabadilika na haiwez badilika tunajitoa tu ufahamu

Sabbu ya watu kuuana Haina mashiko kupinga ndoa Kwan watu wanagongwa na magar na wanakufa mbona hatuachi kutembea barabarani tukakaa tu ndani tuepuke kufa
 
Kuoa au kuolewa ni maamuzi ya mtu binafsi, watu wasitishane. Mbona mapadre na masista hawaoi wala kuolewa na hatuwaoni wakiteseka huko uzeeni?.

Ukiishi maisha ya ubachela ishi kwa nidhamu na mikakati. Jiunge na mrengo kwenye dini yako, jiunge club moja wapo unayoishi msimamo wao, fanya kazi au biashara zako vizuri. Kusanya utajiri na uutumie huo utajiri.

Kama una mtoto au watoto wape elimu nzuri, pia tafuta vijana kadhaa wanaotoka familia masikini ila wana hari na elimu kisha wapige sapoti kama wanao, hao ndio hadhina yako huko uzeeni.

Sasa watu wanadhani tukiamua kuishi maisha ya ubachela basi ni wasela wasela, ubachela hadi dini zipo zinazouelewa na kuufanya ngazi ya kiimani.

Kuwa bachela, fanya wajibu wako kwa Mungu na jamii. Utaishi kwa furaha sana.
 
Well said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…