Wale ambao hatuna Mpango wa kuoa tuendelee kupeana Mbinu za Maisha

Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuleta uzi hapa ni jinsi gani ndoa ni scam, ni jinsi gani ndoa iko pale kumnufaisha Mwanamke.

Siku za karibuni kumezuka matukio kadhaa ya mauaji ya wanandoa, au wanandoa kujiua sababu kubwa ikiwa mifarakano ya ndani ya ndoa.

Kwa Muktadha huo nazidi kushikilia ule msimamo wangu ya kwamba Maisha ya Mwanaume ili yawe Marefu kwa zama hizi aachana na hizi ndoa. Hutoua/Kuuawa/Kujiua.

Je wale wenzangu Lifetime Bachelors tupeane Mbinu zipi katika maisha yetu ya ubachela?

Uzi tayari!

cc: Liverpool VPN
Utakuja kufa peke yako gheto.
 
Na vilevile si wa kuwaamini sana.Anaweza kuwa anahamasisha kutooa kumbe yeye yupo na familia yaje kwa utulivuuu.Anatuchora tu.

Kuna mzee huyo anang’ang’ania kuishi kwetu ashazeeka ,nikamuambia mama yangu ashazeeka hawez kukuhudumia kakae kwa watoto ni kama anajifanya hanisikii anasema akija kwa mama anahudumiwa vizuri eti
Ebo ulikuwa wapi kutengeneza mazingira toka zamani uhudumiwe vizuru
 
Huyo ni kupe.Amevuka unyonyaji wa kawaida.Maisha ya wenza hutengenezwa kwa hatua na hazirukwi.Ndiyo maana huwa wanatafuta hela na kuishia kuibiwa au kutapeliwa.Ndiyo adhabu yao hiyo ya kukiuka maumbile asili ya maisha ya kibinadamu.Let them rot and sink in sorrowful ways!😂😂😂😂
 
Anataka mama amtandikie ,amfulie na mama yangu hawezi ashajichokea akienda kukaa kwa watoto wake eti hawamtunzi vyema 😂😂
 
siku mwili ukianza kunyauka kwa sababu ya uzee na huna mke wa kukutegemeza utakumbuka majigambo yako kwa majuto makali sana. waulize waliozeeka bila kuoa wanavyoteseka.
Kwahiyo mke hawez kufa wa kwanza? Hawez kuishiwa nguv wa kwanza? Hawez kulemaa wa kwanza?
Mleta mada muhim sana uwe na bima za maana utibiwe kama aghakan wanajari kuliko ndugu.
Mleta mada uwe na makaz rafik usikose wa kukaa nae kati ya ndugu, jamaa na marafiki
Mleta mada wekeza vitega uchumi visivyohitaj ufuatiliaji wa kila siku kama real estate, au hisa. Pesa ikukute kitandan.
Mleta mada jenga mahusino mazuri na watu wote na zaid wa dini yako. Mtu mwema hakosag wa kumsaidia.
Mleta mada kama utafit uko sahihi utakufa miaka 5 haraka kabla ya aliyeoa kama ambavyo aliyeoa mke 1 anakufa haraka kabla ya wa wake wengi.
Mleta mada kuoa wakat mwingine huwa ni involuntary action. Unashtukia uko ndoan. Umeshawekwa kwenye sidiria. Nadhan bado u kijana.
Mleta mada nakuhakikishia UTAOA TU! hata iwe wiki 1.
 
Kwahiyo mke hawez kufa wa kwanza? Hawez kuishiwa nguv wa kwanza? Hawez kulemaa wa kwanza?
Mleta mada muhim sana uwe na bima za maana utibiwe aghakan.
Mleta mada uwe na makaz rafik usikose wa kukaa nae kati ya ndugu, jamaa na marafiki
Mleta mada wekeza vitega uchumi visivyohitaj ufuatiliaji wa kila siku kama real estate, au hisa. Pesa ikukute kitandan.
Mleta mada jenga mahusino mazuri na watu wote na zaid wa dini yako. Mtu mwema hakosag wa kumsaidia.
Mleta mada kama utafit uko sahihi utakufa miaka 5 haraka kabla ya aliyeoa kama ambavyo aliyeoa mke 1 anakufa haraka kabla ya wa wake wengi.
Mleta mada kuoa wakat mwingine huwa ni involuntary action. Unashtukia uko ndoan. Umeshawekwa kwenye sidiria. Nadhan bado u kijana.
Mleta mada nakuhakikishia UTAOA TU! hata iwe wiki 1.
We jamaa kichwa chako kimetulia sana, Safi saana.
 
Ninamuona Baba mwenye nyumba wangu ana 50+ hana Ndoa na wala hana huo mpango, ana Mtoto mmoja yupo Marekani,
Anasema shida zake za mwili huzimaliza kwa mwezi mara moja kwa dau la elfu 30 tu hazidishi,

Anajipenda sana, ana ujana mwingi na kwake kapangisha wasela tupu hataki familia,

Nguo anafua kwenye washing machine,
Jioni lazima aende baharini anasema anapata tiba ya akili, "bahari inaongea kama ukisiliza mawimbi vizuri"

Ukimuona ana furaha ila kuna watu wanahisi ni mpweke.
 
Back
Top Bottom