Wale ambao hatuna Mpango wa kuoa tuendelee kupeana Mbinu za Maisha

Wale ambao hatuna Mpango wa kuoa tuendelee kupeana Mbinu za Maisha

I'm glad I've wrote one the greatest thread.
Kichwa cha uzi kinasema "tupeane mbinu za kuendelea kuishi kibachela " afu kuna wajinga wanakuja kusema "kuoa n lazma" hv hawa watu naona ndoa zmetikisa kabisa mizizi ya akili zao. Hawajaitwa ila wanakuja wamejaa povu.

kama mshadakwa mkaingia ndoan endeleeni kupambana
 
Dangote,mike adenuga,chief adeleke, prince Ned nwoko(ndoa ya mkataba na wake 6 no assets will be lost in divorce) hao ni Nigeria ambayo ni Africa haya bongo (mondi,Fred vunjabei,Rostam) hio ni bongo haya worldwide (Elon musk,bezos,bill gates,) bado unapinga na wengine shida si famous hata nikikutajia huta wajua #Kaa CHONJO#
No assets will be lost in divorce

Hiki ndo tunakitaka kije bongo!
 
Kuna kiburi Cha uhai na kiburi Cha kuwa na afya Ila Mungu alijua wapi atukamatie utaruka ruka wee hujui ni kuanzia miak 27 au 30 au 60 afyayako itakuwa haieleweki na hizo pesa hujui utakuwa umepata au lah
Fear of Insecurities inakusumbua
 
Kwahiyo mwanaume akiwa na mke nakuwa na guarantee ya kuyaepuka yote hayo?

Yani mke ana play part ipi haswa katika kuyaepusha?
Yaan hawa pro marriage wanaruka ruka tu kuokoteza point hawana lolote[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mara miaka 25 utaugua, mara uzeen utakosa msaada yaan hawajui nn wanakiongelea
 
Huu Uzi nausoma tu.

Nilikuwa team A saivi nimehamia Team B baada ya kupata kimwana mtoto aliyetayari kuishi na Mimi kwa shida na Raha

Anyway itabidi niwe observer Siwezi tia neno kwa Sasa. I need to experience this other side of life. I never know something good will happen to me

Never say never.
Kaa chonjo
 
Wazazi pia wao ndio uchangia talaka kwa watoto wao sababu ya malezi mabovu kwa watoto wao. Mzazi mtoto sio wa kwako mtoto kwa mzazi ni mpangaji thus akifika umri anaondoka nyumbani, wewe umepewa na Mungu umlee tu kwa mda, mtoto sio wa kwako. Mtoto yeyeto uliyenae ni mme au mke wa mtu mtarajiwa na kwako yupo tuition kile unachomfunza ndicho anakwenda kupractice kwenye ndoa yake. Ndoa ni copy na paste ya jinsi wazazi walivyoishi labda tu kwa wale wenye hekima ( hekima means MUNGU ndani ya mwanadamu UTU ).Unapomuharibu mtoto means unaharibu ndoa yake atakuwa na tabia ngumu zisizovumilika kifuatacho ni talaka ( shetani ).Na lengo la talaka ni kuharibu future ya watoto au mtoto, shetani Katu hawezi leta talaka bila kuchungulia kesho ya mtoto watoto itakuaje, ukiona talaka tambua kuna mtoto au watoto wako kesho yake ni nzuri ana kipaji talanta ukubwa au kipawa fulani Ili kukisambaratisha shetani uleta talaka wazazi wakishatengana atawawini watoto au mlengwa kwa kukosa malezi ya wazazi (saikolojiko balance) mtoto akikosa malezi ataingia kwenye ulevi, uvutaji, umalaya, ushoga, wizi, nk Ili apate balance. Wote waliongia huko ( inaitwa kuuza nafsi yako kwa shetani ) wamekosa parental control wanafanya hivyo Ili kuitafuta ile saikolojiko balance ( utulivu wa nafsi, amani ya moyo ) Ulezi au uwepo wa baba na mama ni tiba ya magonjwa ya saikolojia kwa watoto na uwafanya wabalance. So lengo la talaka behind the scenes ni kuvuruga kipawa alichonacho mtoto, thus kwa study ni ngumu Sana kupeana talaka kabla amjabahatika kupata watoto au mtoto. Roho ya talaka huwa inakuja kuanzia miaka 5 ya ndoa kuanzia mtoto mmoja maadamu tu awe na kitu Mungu kaweka ndani yake, au unaweza ukazaa watoto wengine mkawq shwali mwenye kipawa akawa mtoto wa nne au kuendelea.Kama Hakuna mtoto mwenye kipawa ndani yake ni ngumu Sana talaka kujitokeza.
So usione hawa machizi, mateja, vibaka, nk mtaani hawa shetani kachukua vipawa vyao na kuwapa wafuasi wake wanufaike navyo kwa kuwaibia wengine.
 
Kuoa au kuolewa ni maamuzi ya mtu binafsi, watu wasitishane. Mbona mapadre na masista hawaoi wala kuolewa na hatuwaoni wakiteseka huko uzeeni?.

Ukiishi maisha ya ubachela ishi kwa nidhamu na mikakati. Jiunge na mrengo kwenye dini yako, jiunge club moja wapo unayoishi msimamo wao, fanya kazi au biashara zako vizuri. Kusanya utajiri na uutumie huo utajiri.

Kama una mtoto au watoto wape elimu nzuri, pia tafuta vijana kadhaa wanaotoka familia masikini ila wana hari na elimu kisha wapige sapoti kama wanao, hao ndio hadhina yako huko uzeeni.

Sasa watu wanadhani tukiamua kuishi maisha ya ubachela basi ni wasela wasela, ubachela hadi dini zipo zinazouelewa na kuufanya ngazi ya kiimani.

Kuwa bachela, fanya wajibu wako kwa Mungu na jamii. Utaishi kwa furaha sana.
Hii dini ya bachellors hapa bongo ipo?? Nataka nijoin asap
 
Laiti kama watu wote wasingekuwa wanaficha tabia zao uchumbani kitu kinachoitwa talaka kisingekuwepo. Au wazazi wangekuwa wawazi kueleza tabia za watoto upande wa pili watu wasingeharibu vyeti vyao vya ndoa.
Unakuta mtu anajifanya malaika akiingia tu kwenye ndoa anageuka shetani hadi unajuta, anakuwa na tabia nje ya mkataba. Wewe kama ni mlevi, mzinzi, tapeli, muongo,mgomvi,mpigaji, hasira, mchawi nk onyesha weakness zote kwa mwenza wake hata wazazi nao waeleze weakness za watoto wao upande wa pili Ili mtu aamue kuchukua goma au kuacha kwa kupima anaweza himili tabia hizo?
Maana hata ukijifanya ndoa Hakuna feki life kule ni real, kama ulikuwa unaazima pamba, badili magari Ili kumvuta mtu itajulikana, kama ulimdanganya wewe ni meneja kumbe ni mlinzi, mhudumu tu haijifichi hio vitaonekana kifuatacho ni kuachana kwann usiwe muwazi tangu mwanzoni?.
Unakuta binti KILA binti wa ibada kweli , anakataa pesa ingia nae kwenye ndoa SAsa na kanisa kwake kituo cha police, anasachi hadi chenji mfukoni ukirudi.
Uchumbani binti nyumba safi usafi KILA kona baada ya ndoa KILA kitu kaachiwa dada unapishana na nguo chafu koridoni,mke yupo bize na chating siku hizi wanawake hawafanyi wajibu wao ndani,wameachia kina dada KILA kitu dada wao wanaogopa kuharibu makucha na makeups zao za kishetan.
Haya mambo ndio uleta kuachana. Ukiingia kwenye mkataba wa ndoa na mtu aitakiwi ubadilike kama alivyokupenda uchumbani uwe hivyo hivyo ndoani. Hii itaepusha talaka.
Wazazi msifiche tabia za watoto wenu upande wa pili, sio kusherekea tu send off na harusi mkijua awafiki mbali, talaka ni aibu kuliko hata kuchelewa kuoa/ kuolewa. Thus unakuta mwezi tu watu wameachana.
Wajibu wa mke ndani ya nyumba ni zaidi ya ngono,ngono hata nje unanunua,wajibu ni kuangalia familia,mke ni katibu wa mume,Kazi ya mume ni kutunza familia ( kutafuta pesa) . Mwanaume ni ATM ya familia na ATM ikikosa pesa ni SAwa na gari zuri lisilo na mafuta.
WATU WASIJUFANYE MALAIKA KISHA UGEUKA SHETANI.
 
Miaka kadhaa nyuma niliwahi kuleta uzi hapa ni jinsi gani ndoa ni scam, ni jinsi gani ndoa iko pale kumnufaisha Mwanamke.

Siku za karibuni kumezuka matukio kadhaa ya mauaji ya wanandoa, au wanandoa kujiua sababu kubwa ikiwa mifarakano ya ndani ya ndoa.

Kwa Muktadha huo nazidi kushikilia ule msimamo wangu ya kwamba Maisha ya Mwanaume ili yawe Marefu kwa zama hizi aachana na hizi ndoa. Hutoua/Kuuawa/Kujiua.

Je wale wenzangu Lifetime Bachelors tupeane Mbinu zipi katika maisha yetu ya ubachela?

Uzi tayari!

cc: Liverpool VPN
Ndoa ni taasisi nyingine ya kimaisha kama familia hata taifa. Ukiingalia kwa ufinyu na upande wa mabaya utaichukia kwa sababu ya uvivu wa kufikiri au sababu fichi. Kwanini uchukie ndoa na si binadamu? Kwanini huangalii wale ambao ndoa zimewakoa na kuwakuza? Huwezi kuhukumu taasisi nzima kwa sababu ya matukio machache na ufinyu wa kuyadurusu mambo. Kama hivyo, jichukie wewe kwa vile nawe ni mwanadamu? Je ulizaliwa nje ya ndoa? Kama la hasha, fikiria ungekuwa wapi bila ndoa.
 
Ndoa ni taasisi nyingine ya kimaisha kama familia hata taifa. Ukiingalia kwa ufinyu na upande wa mabaya utaichukia kwa sababu ya uvivu wa kufikiri au sababu fichi. Kwanini uchukie ndoa na si binadamu? Kwanini huangalii wale ambao ndoa zimewakoa na kuwakuza? Huwezi kuhukumu taasisi nzima kwa sababu ya matukio machache na ufinyu wa kuyadurusu mambo. Kama hivyo, jichukie wewe kwa vile nawe ni mwanadamu? Je ulizaliwa nje ya ndoa? Kama la hasha, fikiria ungekuwa wapi bila ndoa.
Mahakama inapomhukum mtuhumiwa kwenda jela miaka 100 huwa inafocus kukomesha lile kosa au kumkomesha mtuhumiwa?

Kama vile mahakama inavolitazama kosa, (na sio mkosaji) bas na sie tunaitazama taasisi ya ndoa na sio watu binafsi (wanandoa)
 
Mahakama inapomhukum mtuhumiwa kwenda jela miaka 100 huwa inafocus kukomesha lile kosa au kumkomesha mtuhumiwa?

Kama vile mahakama inavolitazama kosa, (na sio mkosaji) bas na sie tunaitazama taasisi ya ndoa na sio watu binafsi (wanandoa)
Nyie akina nani? Mahakama inamhukumu mtu na si kosa. Hujaelewa vizuri. Mahakama inamtazama mkosaji siyo kosa. Ndiyo maana ili kosa la jinai kutendea lazima kuwepo na mambo mawili yaani mens rea au nia ovu na actus reus au kitendo ambavyo vyote ni vya mkosaji na si kosa alilotenda. Nadhani kwa maelezo mafupi haya utakubaliana nami kuwa tuangalie wahusika na si taasisi.
 
Nyie akina nani? Mahakama inamhukumu mtu na si kosa. Hujaelewa vizuri. Mahakama inamtazama mkosaji siyo kosa. Ndiyo maana ili kosa la jinai kutendea lazima kuwepo na mambo mawili yaani mens rea au nia ovu na actus reus au kitendo ambavyo vyote ni vya mkosaji na si kosa alilotenda. Nadhani kwa maelezo mafupi haya utakubaliana nami kuwa tuangalie wahusika na si taasisi.
Rudia kusoma Ulichokiandika afu nambie,, kina tofauti na nlichoandka mm?
 
Rudia kusoma Ulichokiandika afu nambie,, kina tofauti na nlichoandka mm?
Sema hujanielewa unataka nitafune umeze. Mazingatio yetu ni tofauti kama usiku na mchana. Unasema sheria inaangalia kosa badala ya mkosaji nami nasema hasha. Hapa kifani kiko wapi? Au unatafuta namna ya kuficha uso?
 
Back
Top Bottom