Ukioa mtumishi si mbaya maana hata mabinti zetu tunawasomesha pengine wanaweza kuja kupata ajira wakawa chini ya serikali au kampuni binafsi. Itakupasa kukubaliana na yafuatayo.
Pesa yake haikuhusu, ingawa hawezi kumwacha mtoto wake wa kumzaa akikosa mahitaji, hiyo never. Na pengine hapo ndo kuna unafuu kidogo maana anahudumia wanao kwa vitu wanavyovipenda kama nguo, zawadi nzuri na favours nyingine kama visherehe vya siku ya kuzaliwa.
Atarudi amechoka kutoka kazini, hivyo kubali kukosa care kwa mume kama kufuliwa, kupikiwa na mengineyo ukubali kuzopata kwa dada wa kazi,
Huwezi kumwekea mipaka kama mkeo maana kuna maamuzi yatakayoathiriwa na boss wake huko kazini kwake. Yapasa kukubaliana na kitakachopangwa huko kazini kwake mfano safari ya mbali kikazi, kurudi amechelewa kutokana na majukumu ya ziada. Huna sauti utakuwa ni kukubaliana tu.
Watoto wako watatumia maziwa mbadala na muda mwingi watakaa na dada wa kazi kwa sababu ratiba za mkeo haziwezi kumpa nafasi kutosheleza mahitaji ya kihisia na kimwili ya mtoto wenu ambayo ni lazima kwa makuzi ya mtoto.
Mwanamke ndiye huifanya nyumba kuwe nyumbani mfano kelele za watoto na michezo yao, Usafi wa maua yaliyokatwa vyema na kutunzwa vizuri, usafi wa ndani na activities za hapa na pale mfano ubunifu wa mapishi, kukuwakilisha kwenye vikao vidogo vidogo vya kijamii, kukuletea umbea kidogo wa mtaa ambao ni sehemu ya security..
Mengi mengi tu.
Haya huwezi kuyategemea kwa mke mwenye majukumu mengi ya kikazi.
Ukubali pia pamoja na mzigo wote wa kuihudumia familia ambao mkeo anaweza akakuachia lakini hutapata huduma nyingi za mume ikiwemo tendo la ndoa, utakachokiambulia labda ni heshima uchwara ambayo utakuwa ukijipa mwenyewe kuwa unamiliki mke msomi mwenye kazi ambayo kiuhalisiaina mchango mdogo saba kwenye maisha yako.
Haogopi kukupoteza kwa sababu anayo option za wanaume wengi na kipato. Hatahangaika na wewe hasa watoto wake wakikua. Hivyo unapaswa kujiwekewekeza usitumie nguvu zako zote za ujana kumfurahisha ukasahau kujiendeleza kuandaa maisha yako hasa ukiwa mzee maana hata hao watoto watakuwa upande wako kwa asilimia 25 tu 75 kwake.
Kinyume chake ukioa mke asiye na ajira yapo pia unaweza kukutana nayo mfano;
Kama si mcha Mungu kweli atakuroga ili akuweke sawa maana wewe ukikengeuka na wanawake wengine yeye hali kwake ni tete maana anakutegemea kwa mambo yote.
Ila kikubwa utapata heshima na treatment nyingi anazostahili mume maana kazi yake kubwa itakuwa kujifunza kukufurahisha ili asikupoteze
Kila mtu anapaswa kuangalia anahitaji kuishi maisha ya namna gani kabla hajaoa