Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Wale mliokimbilia kujenga Dodoma poleni sana

Mmoja basi aje PM ani uzie nyumba au kiwanja DOM
mimi bado napakubali,
nimeishi DAR, TABORA, MORO, MWANZA NA SASA NIKO ARUSHA kote ni kikazi serikalin ila DOM napa penda..
IMG-20211223-WA0028.jpg
 
Ukiona mji unalazimishwa na serikali ili kuuokoa pakimbie.Maana nguvu yakiuchumi ya huo mji itategemea na aina na ushawishi wa kiongozi wa serikali husika.siku akiondoka mji nao unadorora.Kwa mji kama dodoma itachukua miaka mingi mji kukidhi vigezo vya asili vyakuishi watu katika mazingira rafiki na ya asili yanayomvutia kila mtu kiuchumi na kijamii.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nyuzi kama hizi ziwekwe kumbukumbu kwa ajili ya wanaolikashifu jiji/mji mkuu...

Patakua kama uyoga
Kama vile watu walivyoidharau Goba ila baada ya barabara tu imegeuka hotspot
 

Huu uongo unakusaidia nini mkuu..

Karibu Dom mkuu 👇

View attachment 2056780
Sometimes muwe mnaangalia na vya kuwapostia watu kama waleta mada, hivi kwa akili yako unaona huyo jamaa ni wa level wa kulipia hizo lodge. We mtafutie geust house za buku tano, sasa dodoma hizo geust hakuna labda madanguro tu
 
Kabisa vyuo vikifungwa tu dodoma biashara zina chacha
Njia rahisi ya kujua kama dodma kuna mzunguko kwanza ni kuangalia idadi ya abiria wanaoingia kwa siku kutokea sehem kama dar na mikoa mingine. Kwa mtu ambaye alipita dodoma miaka ya nyuma anaweza dhani pamelala, ni wajinga wachache sana wamebaki na hiyo misemo kuwa dodoma hakuna movement. Kuna lodge zilizopo hazitoshi kulingana na idadi ya wageni wanaongia na kutoka . Nyumba ni chache sana kadri siku zinavyozidi kwenda mbele zinakuwa adimu sana sababu watu wanazidi ongezeka. Benki zinazidiwa. Ni dodoma tu ambako utakutana na tawi la crdb ambalo yamepishana mitaa na yote foleni lake la kufa mtu.
Mpaka equity wanafoleni dodoma.
Ni dodoma pekee ambako abiria hawaangalii bei ila huduma, dodoma happy nation ni ngalangala lakini mwanza ni luxury. Dodoma bila basi la choo ndani unafunga biashara.
Sasa fursa zilizopo dom
Kuna uhaba wa nursery shule za private ni chache wakat mahitaji ni mengi, mleta mada hujaiona hiyo fursa? Au unataka fursa za kutembeza vyombo.
Ujenzi upo kwa spind anzisha kabiashsra katofari kama una hela, sisi tunajua huna
Mahindi mengi sana kibaigwa sagisha unga safirisha kwenda dar utawapiga gepu wale wasongea ambao kusafirisha kwa tani wanalipa 120000 wakati dom ni 30000 na utofauti bei ni 100. Yaan dom mahind sasa hivi ni 60000 wakat songea ni 50000 ila kusafirisha mahind toka songea dar utahitaji 3600000 kwa tani 30 wakat dom utalipia 900000. Utofauti wa 1.7mil.

Tafuta hela we bwege uache kuishi kwenye nyumba za uridhi
 
Hata mimi ndio nashangaa kwanza Dodoma kuna vyuo kibao, unakosa hata wanafunzi.

UDOM

Hombolo

Saint John

Mimi nimeishi Dsm na wazazi wangu wapo huko, now naishi Dodoma,ila Dsm ina sifa mbili ambazo sijawahi kuzizoea, joto + foleni... watu wanapoteza muda mwingi sana barabarani.... sehemu ya KM 10 unawezatumia masaa mawili mpaka ma3... hali ya hewa ndio hovyooo kabisaaaa. Huwa nikipangiwa safari ya kwenda Dar nachukia sana, siwezi kutembea bila leso...mji wa hovyo kabisa.
You nailed it. Mwanzo nilikuwa na mawazo ya kama mleta mada tulipohamishiwa dom niliaumu mpaka basi, ikawa kila weekend nipo dar baadae wife nae akahamia dom, miaka ya 2018 hiyo. Basi nikanunua nzuguni eka mbili kwa 1mil. Mwaka jana huu sqm 900 kwa milion 5 kwa viwanja vyote nikala mil 50. Halafu mtu aje ananiambie nihame dom. Kila nikiingia dar natoka vipele vya joto. Watu wamekariri stori za vijiwen.
Dom sasa hivi ni center ya kila sehem.
Dom haina uhaba wa maji kama wanavyodanganyana.
Hali ya hewa dodoma ni nzuri. Kuna wastan wa joto la sentrigedi 24 wakat dar ni 28.
 
Sasa kwanini dodoma isiwe makao makuu, hangaya anapenda tuu kukaa dar ila maamuzi ya kuhamia dodoma yalikuwa sahihi

Maamuzi ya kuhamia Dodoma yalikuwa sahihi enzi ya Nyerere wakati huo technology ya mawasiliano ilikuwa duni lakini sio leo!!!
 
Hii nchi ina watu wapuuzi sana. Dodoma ilikuwa makoa makuu ya nchi miaka mingi sana, ilikuwa serikali ihamie huko miaka mingi sana (yawezekana ulikuwa hata haujazaliwa bado). Wazo la serikali kuhamia Dodoma ni la J.K.Nyerere wala sio la viongozi hawa wa juzi sema tu rais wa awamu ya tano alilitilia mkazo sana ndyo maana watanzania wengi wanahisi ni wazo lake.

By the way hata Dar es salaam ilivyoanza hakuna mtu alitarajia kuwa itakuja kuwa hivyo ilivyo leo. Let things flow on their natural ways!
 
Ni upuuzi uliopitiliza kuwekeza mji mgumu kama Dodoma...nyumba hazina soko kabisa..wawekezaji aka shoppers plaza wanajuta manake manunuzi ni watumishi wa umma ambao matumizi yao ni ya msimu na wana nguvu ndogo...Bakharesa na Mo wameshindwa kuweka depot za maana Dodoma....maji hakuna,vumbi,mpauko...yule mwehu ametupa mateso sana
Naishi Dodoma (siyo mzawa), ukweli ni kuwa bei ya nyumba iko juu sana, na waliowekeza kwenye nyumba wanapata pesa nzuri tu. Kuna changamoto za kufanyia kazi kama barabara na mazingira, ila kwa uwekezaji unaoendelea Dodoma, ndani ya miaka 10 Dodoma itakuwa kitu kingine. Wale wenye uwezo wa kuwekeza wanunue hata viwanja watulie, baadae itajakuwa kama wale wazee wetu waliopewa viwanja vya bure maeneo ya Sinza, wakakataa wakisema ni porini.
 
Back
Top Bottom