Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mimi kila siku huwa naangalia na kusoma vitu anavyopost na kuandika mitandaoni Tajiri Nambari Moja Duniani Elon Musk kupitia mtandao wake wa Twitter maarufu X.
Ambapo amekuwa akipost na kuandika vitu vya kawaida na vyepesi sana ambavyo huwezi kujifunza kitu chochote kile katika maisha. Anaandikaga vitu ambavyo angepost na kuandika kiongozi kutoka Tanzania au mwanasiasa ungeona Wabongo wanavyoleta ujuaji.
Sasa leo Ameposti picha ya pasi ya mkaa tena zile pasi za zamani sana au waweza kusema matoleo ya Mwanzo kabisa. Na katika post hiyo akauliza kama watu wanafahamu matumizi yake.
Shida yetu Wabongo kitu kikifanywa na mzungu kinaonekana ni cha maana sana hata kama kitu na jambo hilo ni la kijinga tu. Tuna kasumba ya kujidharau ,kujishusha thamani ,kujiweka chini na kujiona ni binadamu toleo la Mwisho tusio na thamani.
ndio Maana tunajiweka katika hali ya unyonge sana na kuweka mikono nyuma kwa uoga mbele ya wenzetu.ndio Maana hata mtu akiongea kizungu kama mnavyokiita Ninyi kiingereza anaonekana ana akili na msomi sana.
Ndio Maana unakuta watu na akili zao timamu wanajadili habari za kizungu au kiingereza cha mtu kuwa huyu anajua na huyu hajui na kwamba hana akili.bila kujua mataifa kama Japan au China hawaongei Kizungu lakini wana maendeleo makubwa kabisa na hata wakiwa kwenye vikao na mikutano ya umoja wa Mataifa wanazungumza kwa lugha zao na kushangiliwa
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.